DOKEZO Hali ni mbaya sana kwa walemavu tuliosoma, Si Serikali wala kampuni binafsi ambazo ziko tayari kutuajiri. Tunabaguliwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kweli hili ni changamoto maeneo mengi, japo miaka ya karibuni kwenye majengo ya Umma hasa ya Serikali wameanza kuweka accessories za kuweza kuwa accommodate watu wenye ulemavu pia

Ni mwanzo mzuri kwa kuanzia
Ndio na kwenyewe ni kwa mbinde. Yaani tofauti na mahospitali maeneo mengine ni shida.

Kwingine ni changamoto mpaka vyoo si rafiki kwa ndugu zetu.
 
Ndio na kwenyewe ni kwa mbinde. Yaani tofauti na mahospitali maeneo mengine ni shida.

Kwingine ni changamoto mpaka vyoo si rafiki kwa ndugu zetu.
Nakiri wazi, hii changamoto bado ipo

Nadhani wenye mamlaka Wana wajibu wa kuhakikisha mazingira rafiki Kwa hawa ndugu zetu yanawekwa

Ukienda Mlimani City pale wamejitahidi kiasi chake ila maeneo mengine bado nguvu kubwa inahitajika
 
Nadhani kuna kupuuza ukizingatia namba yao ni ndogo mno.
 
Pole sana Mkuu...

Kama una hoja unayotaka imfikie, sio lazima iende kwake.

Waweza ukai-channel Kwa Waziri husika.

Hopefully Waziri atakuwa na nafasi kubwa kukujibu kuliko huyo Mbunge.
Tunaichannel vip mkuu
 
Nakiri wazi, hii changamoto bado ipo

Nadhani wenye mamlaka Wana wajibu wa kuhakikisha mazingira rafiki Kwa hawa ndugu zetu yanawekwa

Ukienda Mlimani City pale wamejitahidi kiasi chake ila maeneo mengine bado nguvu kubwa inahitajika
Ni kimataifa pale kwahio wamezingatia hilo
 
Dah! Inasikitisha sana. Hizi ajira hizi, hali tete si kidogo.
 
Walemavu mna nguvu sana.
Na kuajiriwa sio kuwa na akili tu basi.
Kuajiriwa kuna kutembea sana, kubeba mizigo.
Kukimbiza mafaili
Kupanga mafaili kwenye makabati.
Kuitwa ofisi ya Mkurugenzi zaidi ya mara kumi kwa siku na yupo ghorofa ya tatu ambayo haina lifti.

Hivyo waajiri wanawaonea huruma kwa kimbiza kimbiza.
Ndio maana wanawakataa kwa mantiki ya kushindwa kufikia ufanisi wa kazi.

Walemavu mnanguvu sana basi msomee kazi za binafsi ambazo hazi hitaji kutembea tembea kama ufundi CHALAHANI.

Kwa wanawake wajifunze mambo kama ya Saloon na ususi na mapambo. Nk.

Nadhani mumeelewa
 
Nafikiri hakuna mtu anaezuiwa kusoma anachopenda!.. Kama wew umependezwa na ufundi cherehani ni heri kwako!!..

Kuna ambao akili zao zikitumika vzuri hawa hawa unaowaona hawawezi kuwabebea mafaili.. mtakaa chin na kujuta kwann siku zote mlikuwa hamuwaajiri kwa kisingizio Cha kuwatuma kupeleka mafaili
 
Ndo umejua leo kwamba Mimi ni mpumbavu?

Utazaa mtoto mwenye ulemavu au kama sio wewe ni mwanao SAVE HII.
 
Mwalimu wangu Mr. Kaluhawe alikuwa na ulemavu wa kutoona. Akiwa anatoa lecture pale M9 SAUT mida baada ya lunch, ungemsikia anasema, "I see you sleeping"! Ahahahahaha! Alikuwa mwamba sana!
 
Hakika, nafikiri watazingatia kwenye ajira mpya walizotangaza hivi karibuni za TRA
Japo nataman kuwepo na system maalumu ya kuwajiri wenye ulemavu, ili isije ukawa hawa wakaajiri kwakuwa tu watu wamepaza sauti, then mwakani makosa yakajirudia vilevile kwakuwa labda hakuna wa kusema hili.

System nzuri ya kuajiri, hata wakiwa na namna Yao ya kuwa recruit itapendeza sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…