Hali ni mbaya sana, nazidi kudhoofika

Njoo cotex mkuu kazi zipo na huku family pia kazi za kumwaga tu
 
Sasa ndio ushangae maana hao MURZAH wanatengeneza mafuta ya kula, tambi na sabuni.

Ina maana soko limeshuka mpaka wafunge kiwanda au kupunguza Uzalishaji ??
Kama watu wamepunguza milo toka 3 Hadi mmoja au wanapiga deshi Hadi kesho sababu mzunguko wa pesa mtaani umekufa sababu ya sera mbovu za kuwafanya watu wawe masikini ili uwatawale Ili upate furaha,wakizalisha bidhaa nyingi kuliko uhitaji zitaexpire madukani hasara kwao.
 
Pole sana ndugu yangu naomba nikushauri jaribu kukubali kuanzia chini juu ya kile unachokiwaza usiwazie sana ajira. Mimi nipo huko huu ni mwaka wa 11 sasa lakini ninayo hadithi ya kuwahadithia wengine yenye kichwa kinachosema " Ajira haikuandaliwa kumtajirisha mwajiriwa".Ni kifungo hatari sana ukiingia...nafahamu wapo watakaonielewa.

Upo maeneo gani ndugu? Mimi nipo Geita karibu tunaweza tukafanya chochote ukaendelea na maisha usiwaze sana ukafikia maamuzi magumu kama waliyoyachukua baadhi ya ndugu zetu humu.

Naandika kwa huzuni sana kwa sababu kuna mtu humu aliwahi kuandika tukadhani anatani na wapo waliomkejeli lakini cha ajabu mtu yule alifikia hatua ya kujinyonga halafu walewale waliomkejeli wakati anaomba msaada wanaandika R.I.P...daah..so sad Mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…