Hali ni Ngumu Sana; Nimeulizwa Swali, Je Christmas ipo Mwaka huu au Imeahirishwa?

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
40,455
Reaction score
73,145
Yaweza kuonekana ni story ya kutunga na hata mie nilidhani nataniwa. Lakini ugumu wa maisha ya Mtanzania ulimfanya mtoto wa rafiki yangu around 12yrs aniulize "baba mkubwa mwaka huu Christmas ipo au imeahirishwa?

Mbona kila mtu yuko kimya na hamna hata maua?"

Ni kweli, wazazi wengi sasa hivi ni wanyonge kwa kushindwa kutimiza waliyokuwa wanatimiza kwa familia zao miaka ya nyuma. Lakini kwa wale waliokuwa tangu hapo kale ni mambo magumu tuu wanafuraha ya ajabu kuwa bora tuwe wote masikini, kwa kindengereko wanaita hali hiyo ni poverty mentality.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza, Sikuu ya Uhuru iliahirishwa kwa tangazo, Christmas inaweza kuahirishwa kwa mzunguko wa fedha.

Kuna muandishi mmoja alikuwa anaandika kuhusu Uganda siku za utawala wa Idi Amin.

Akasema alivyofika Uganda ya Idi Amin aliona nchi tofauti. Waganda kawaida ni wacheshi, watu wenye furaha, lakini Uganda ya Idi Amin ilikuwa tofauti, imejaa majonzi na woga.

Sasa hivi mzunguko wa fedha mgumu.

Sawa, ndugu zenu tulioondoka hapo tuko nje tukawa tunadunduliza na kutuma hela kusaidia. Ukimtumia mtu dola za Marekani mia moja au mbili muda huu wa sikukuu anaweza kufanya maarifa makubwa ajisikie na yeye anaishi.

Mara paap, Benki Kuu imekata nafasi za kutuma hela moja kwa moja MPesa.

Tumewekewa masharti mapya kutuma pesa mpaka uruke viunzi kibao, utume picha na ID card. Hata maelezo yenyewe hayako clear.

Ili mradi usumbufu tu, hata kwa mtu anayetaka kutoa msaada.

Tanzania kwa sasa unaweza kusema unataka kuleta matrekta ya bure kusaidia wakulima, serikali ikakudai kodi hapo hapo!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aisee kama upo nje ya nchi basi nakuomba usirudi huku bongo maana haya sio maisha ni motoni....nawasihi mlioko huko nje endeleeni Kula maisha Tu
Siku hizi hata likizo ni visiwa vya Turks and Caicos tu.

Unaweza kusema urudi likizo wiki mbili, ukapewa kesi ya mtandao ya kumkashifu Mtukufu ukapotezwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie endeleeni na ujinga wenu, wenzenu wanakula bata na hawana wasi

Hamuoni abiria walivyoongezeka? Mabasi hayashikiki! Treni inajaza na kujaza.ki ufupi hakuna tashwishwi. Fungua hiyo video ujionee maajabu na ndio utajua christmass ipo au umeamua kuiahirisha kiuchwara

MATAGA
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiranga, Sasa nimeelewa kwa nini tunaongoza kwa kuwa nchi ya watu wasio na furaha.
Kumbe imefikia Kiranga huko nje ukitaka kumpa furaha ndugu yako kwa vidola kadhaa unakumbana na vikwazo kama unataka kusaidia magaidi?
Mbona nchi kama Nigeria au Kenya RAIA wake walio nje ni moja ya vyanzo vikuu vya kuingiza fedha za kigeni? Hizi sio dalili kuwa serikali hii ya CCM haipendi watu wake? Kwa nini isiwalegezee masharti ya kuleta fedha nyumbani na wanyumbani kufaidika na ndugu zao walio nje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa mmoja alikuwa naibu waziri wa madini, alikwenda kwenye migodi ya madini huko kati, nafikiri ilikuwa Kahama.

Akawa anawalalamikia wawekezaji wa nje kwenye sekta ya madini, kwamba wanalipa Watanzania mishahara mikubwa sana. Wapunguze mishahara. Mishahara ile si sawa kwa levels za Watanzania.

Wakati ile kampuni hata hiyo mishahara iliyoonekana mikubwa, kwao ingejulikana ingeonekana scandal, kwamba wanawafanyisha watu kazi kwa kutumia mishahara midogo sana, wanatumia cheap labor.

Kuna kipindi serikali inapiga domo kuhusu kuleta maendeleo, kumaliza umasikini, wakati inajua kwamba haitaki kuleta maendeleo ya kweli, haitaki kumaliza umasikini.

Ikimaliza umasikini itakosa kazi. Umasikini ni mtaji wa serikali kuendelea kuwepo.

Serikali ikimaliza umasikini, watu watajua haki zao, watapata elimu, watai challenge, hawatakubali kuibiwa, serikali itaondolewa.

Hivyo, seruikali haipigi vita kuondoa umasikini, inapiga vita vita ya kuondoa umasikini.

Ndiyo maana unaona serikali inabana mzunguko wa fedha, tukija watu wa diaspora tunataka kusaidia, wakiona kuna watu wanatumiwa hela na ndugu zao walio nje, na sisi tunawekewa viunzi kibao tusitume hela.

Wajanja kibao, tunaenda kuchagua gubegube Magufuli liwe rais!

Tunajiwekea umasikini wenyewe kimfumo.
 
Kiranga,

Hakuna usumbufu wowote ule katika kutuma hela ndogo ndogo Tanzania, hususan kutuma kutoka Marekani.

Sehemu nyingi tu siku hizi wana omba uonyeshe ID.

Karibu sehemu zote za MoneyGram au Western Union, ukienda kumtumia mtu hela wanakuomba ID!

Kuonyesha ID ni standard procedure ya sehemu nyingi tu!
 
Different strokes for different folks.

Mimi libertarian. Hata kuwa na ID tu ni usumbufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi niko Marekani miaka kibao maisha yangu hayamtegemei Jiwe, na sina mpango wa kuja Bongo hata likizo miaka ya karibuni, likizo naishia Marakesh na visiwa vya Turks and Caicos, kulimia meno kwa minajili ya Jiwe naanzia wapi wakati huku matrekta mpaka ya kuendesha kwa computer kutumia Bluetooth yapo?

Yani kuwahurumia waliopo Bongo wanaolalamika tu ushatuona wote tuna shida?
 
unatetea ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…