Hali ni tete Mtwara Leo, Sakata la Gesi

Hali ni tete Mtwara Leo, Sakata la Gesi

Hahahahaha ndo kazi iliyobakia kwa hawa polisi wetu,ila nadhani kuwalaumu pia sio sawa kwani waliapa kuilinda katiba ya tanzania na pia kutii amri za wakuu,so wako sawa kabisa nadhani sio sahihii kabisa kuwalaumu hawa watu

Acha kufikiri kama mtoto wewe. kutii amri haina maana kila unachoambiwa nikusema ndio ila inamaana amri halali tu. huwezi ukaambiwa mpige risasi kila utakayemwona then useme nilipewa amri nifanye hivyo. Jifunze kuvikiri vyema
 
Taifa la Israel linaendelea kuwepo kwa sababu linalindwa na mmarekani, vinginevyo lingekuwa na hali ngumu mno.

Unacheza ww,hakuna mwny uwezo wa kulifuta taifa la israel,hyo ni kutoka kwa Mungu,ipo kwny maandiko
 
Kama samaki nchanga wameamua na wanaitetemesha nchi, sijui itakuwaje siku wale wenye hasira (WATU WA MKOA WA MARA) wakiamua maana naamini mpaka Ikulu itachomwa moto.
Uhuru wa Tanzania uko karibu sana kuliko tulivyodhani.
 
Baada ya samaki Mwanza kupungua na hapo mwanzo na mpaka sasa kupanda bei kw mkoa huu. Wametutenga wala neno samaki halisikiki mara kwa mara. Wametuacha Masikini tofauti na tulivyotegemea. Sasa Mtwara wanataka kufanyiwa the same2 kama Mwanza japo watu wa Mwanza hawakuandamana, sasa ges itoke Mtwara ikasafishiwe na kufanyiwa paking Dar. Ipite tuuuuuu kwenye mabomba kwenda Dar inauma sana. Kwa nini tusipigie kelele katka mtandao huu wa kile kilichotokea leo Mtwara Kuwa ni Sahihi au lha!!!! Karibuni!!!
 
Unacheza ww,hakuna mwny uwezo wa kulifuta taifa la israel,hyo ni kutoka kwa Mungu,ipo kwny maandiko

Ni taifa gani ambalo linaweza kufutwa? Na ukumbuke sijasema lingefutwa, nimesema lingekuwa na hali ngumu. Unakumbuka Adolf Hitler aliwafanya nini? Mataifa mengine yasingeingilia kati huoni kwamba Israel wangekuwa na hali ngumu?
 
Ahaaaa. Kumbe matangazo ya TBC1 yamezimwa kwenye Satellite toka juzi kama sikosei ili Wanamtwara wasiweze kupata hotuba ya Wizara ya Nishati na madini? Maana nimepanda ngazi ili kurekebisha dish nikidhani limeyumba kumbe hapa, chaneli zingine zinaonekana kama kawaida tena kwa signal nzuri isipokuwa TBC1 hadi dakika hii naandika posti hii TBC1 bado haipatikani. Mimi niko Mbeya.
 
Ahaaaa. Kumbe matangazo ya TBC1 yamezimwa kwenye Satellite toka juzi kama sikosei ili Wanamtwara wasiweze kupata hotuba ya Wizara ya Nishati na madini? Maana nimepanda ngazi ili kurekebisha dish nikidhani limeyumba kumbe hapa, chaneli zingine zinaonekana kama kawaida tena kwa signal nzuri isipokuwa TBC1 hadi dakika hii naandika posti hii TBC1 bado haipatikani. Mimi niko Mbeya.

Afadhali mimi miaka tatu sasa niliondoa tbccm kwenye dish langu
 
Kipindi hiko nilikuwa bado kijana mdogo mwanafunzi sikuwepo Mtwara kipindi hiko sikuwa na access ya kuzipata Habari vizuri nilikuwa nasikia sikia tu.

Naomba anayejua vizuri Hizo fujo za gas anisimulie zilianzaje, zilidumu siku ngapi na madhila yaliyoachwa.
 
Ilikuwa noma ila ukijichanganya hii mikoa ya pwani unapewa kesi ya ugaidi, ilikuwa noma mpaka Dangote akatoa ahadi ya ujenzi wa kiwanda.
 
Kipindi hiko nilikuwa bado kijana mdogo mwanafunzi sikuwepo Mtwara kipindi hiko sikuwa na access ya kuzipata Habari vizuri nilikuwa nasikia sikia tu. naomba anayejua vizuri Hizo fujo za gas anisimulie zilianzaje zilidumu siku ngapi na madhila yaliyoachwa
Nakumbuka vurugu hizo zilianza muda mfupi baada ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kuwasilisha bajeti ya wizara yake bungeni.

Na vurugu zile zinahusishwa na madai ya muda mrefu sasa ya wananchi wa mkoa huo kupinga ujenzi wa bomba la gesi iliyogunduliwa mkoani humo kusafirishwa hadi Dar es Salaam, kaskazini mwa Mkoa wa Mtwara, kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme.

Nakumbuka uharibifu mkubwa ulitokea kwenye majengo ya serikali kama mahakama, nyumba za watendaji wa Serikali, baadhi ya majengo ya chama tawala na nyumba za watu binafsi.

Na watu zaidi ya 90 walikamatwa kwenye tukio lile, siku hiyo Jakaya alihutumia kupitia TBC 1, na alisisitiza walio kamatwa wangeshtakiwa.
 
maandamano-gesi.jpg

Gesi haitoki Mtwara.jpg
 
Back
Top Bottom