Hali tete chuo cha ualimu songea, wizara ya elimu yambeba mkuu wa chuo.

Joined
Mar 23, 2012
Posts
64
Reaction score
13
Ni takribani miezi nane sasa tangu nianze kufuatilia uendeshaji wa chuo cha Ualimu Songea kama kinaweza kuendana na kauli mbiu ya sasa ya Serikali ya Big Result Now (Matokeo Makubwa Sasa)

Nimelazimika kukifuatilia Chuo hicho kutokana na mgogoro mkubwa uliopo kati ya wafanyakazi (wakufunzi) na mkuu wao wa chuo Ubaya Suleiman.

Mgogoro huo umetokana na uongozi mbovu usiozingatia misingi ya uongozi na Demokrasia katika vyuo vya ualimu Tanzania kwani Mkuu huyo wa chuo amekuwa na lugha za matusi,vitisho kwa wafanyakazi na wanachuo, kutopokea ushauri kwa washauri wake, mbinafsi, kutowaamini watendaji wake kwa nafasi alizowateua, kufanya kazi kwa kutumia vyanzo visivyo rasmi, Matumizi mabaya ya fedha za Serikali na vyombo vya usafiri

Pamoja na hayo mkuu huyo wa chuo amediriki kuwapeleka baadhi ya wafanyakazi wake kwenye vyombo vya dola (polisi) (kuwatishia) akiwatuhumu kuwa wanataka kumuua. Baada ya mgogoro huo kutopata suluhu kupitia vikao vya ndani, Jitihada zifuatazo zilifanyika na wafanyakazi wa chuo hicho ili kuleta hali ya amani na utulivu wa chuo;

Tarehe 27/04/2013 walifanya kikao na mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti, tarehe 15/05/2013 na tarehe 01/06/2013 walifanya kikao na Bodi ya ushauri ya Chuo, hata hivyo suluhu ya mgogoro huo haikupatikana.

Kutokana na hali hiyo Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Sifuni Mchome aliunda tume ya watu watano ikiongozwa na Mkaguzi Mkuu wa shule na vyuo wa nyanda za juu kusini ambaye alifahamika kwa jina moja la Lyapambile, kuja kufanya utafiti wa chanzo cha mgogoro, lakini mpaka sasa tume hiyo haijatoa majibu ya uchunguzi wa jambo hilo

Tume hiyo haikuishia hapo tarehe 13/08/2013 wafanyakazi walifanya kikao na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu, ambaye baada ya kusikiliza mgogoro huo aliahidi kuleta suluhisho la kudumu mapema iwezekanavyo ili kuleta amani na utulivu(peace and Tranquility) chuoni hapo. Lakini cha kushangaza hadi sasa yapata miezi mitatu hakuna kilichofanyika hali ambayo imeendelea kuwavunja moyo wafanyakazi wa chuo hicho.

Licha ya jitihada zilizofanywa, Mkuu huyo wa Chuo Ubaya Suleiman anaendelea kuwanyanyasa wafanyakazi wake na kusema pigeni kelele lakini wakuning’oa mimi hapa hayupo na lugha zingine ambazo sio za ustaarabu anazitoa, na kuwafanya wafanyakazi wenzake wahoji nguvu aliyonayo katika utendaji, mfano wa lugha zake mbovu ni “kwani mizizi yangu ni mirefu”. Kitendo hicho kinawafanya wafanyakazi wa chuo na wadau wengine watilie mashaka juu ya sifa za uteuzi wake kushika nafasi kubwa kama hiyo.

Tunamuomba Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Shukuru Kawambwa na Naibu wake Philipo Mulugo kumuondoa mkuu huyo wa chuo madarakani na kumtafutia shughuli nyingine ya kufanya kwa ustawi wa chuo cha ualimu songea, taaluma ya ualimu Tanzania na ili kuleta ufanisi wa kauli mbiu ya serikali ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now)

Sababu zinazopelekea hilo ni nyingi ila kwa sasa nitazitaja chache ili kuweka kumbukumbu sawa, ya kwanza Novemba 1, 2013 Mkuu huyo wa chuo bila kuwasiliana na Mtaaluma wake wa Chuo Maiko Luoga, alidiriki kuwaandikia Barua Wakufunzi kuwataka watunge Mtihani wa Moko wa Ualimu viwango vya Baraza la Taifa la Mitihani(NECTA) kwa lugha ya kejeri hali ambayo imesababisha maudhi na utulivu wa akili miongoni mwa wafanyakazi katika kufanikisha utungaji wa mitihani hiyo

Kitendo hicho licha ya kuwa ni kinyume na utawala bora , lakini pia kimekiuka maagizo ya Bodi ya Chuo ambayo yalitolewa tarehe 28/8/2013 (……. mambo yote yanayohusu fedha yaendeshwe kwa uwazi na ushirikishwaji mkubwa miongoni mwa wanaidara / taasisi kwani inaonekana mambo yanaenda kwa usiri mno).Sababu ya pili amekuwa na vitisho vingi katika utendaji wake na maneno ya kuudhi dhidi ya viongozi wenzake , mfano wa maneno yake ambayo anayatamka huku akigonga meza kuashiria ubabe na kiburi cha madaraka ni kama vile,(…. Ukiingia ndani ya kumi na nane zangu nakumaliza, Angalieni msije mkaumia wengine tunambavu za chuma, Nipo tayari kuua inzi kwenye kioo cha TV hata kama itavunjika potelea mbalimbali raha yangu ni kuhakikisha inzi amekufa, Mkitoboa mtumbwi nitahakikisha kabla sijazama mimi nawazamisha ninyi kwanza, Angalia wengine watakaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune, Amekuwa akitishia kung’oa mtu kwa kumwendea (kumpandia)wizarani ndani ya siku mbili na kumchukulia barua ya uhamisho kwenda vyuo vya pembezoni mwa Tanzania, Mimi nafanya haya hata niking’olewa kwa muda mfupi potelea pote nitakuwa nimejenga historia)

Sababu ya tatu ni kutokuwa na uwazi, ukweli na ushirikishwaji kwa njia ya kidemokrasia miongoni mwa idara zake katika chuo hicho na hasa katika fedha ambazo zinakuja kwa ajiri ya manunuzi ya vitu mbalimbali, fedha ya kuendeshea mafunzo ya ualimu kwa vitendo(BTP)

Fedha hiyo licha ya kuchelewesha kuitoa kutokana na ufisadi wake lakini pia hakuitoa yote na wala hakueleza kwa uwazi na ukweli, hali ambayo haikuwezesha wakufunzi kwenda kufanya kazi stahiki kwenye maeneo kusudiwa ya kuwatahini wanachuo ambao walikwenda kwenye shule mbalimbali kwa ajili ya mazoezi ya kufundisha kwa vitendo.

Sababu ya nne ni uwezo wake wa kiuongozi kwani kumekuwepo na mashaka mengi katika Wasifu wake wa kielimu na kiutendaji, hali inayopelekea kuendesha Chuo katika misingi binafsi bila kuzingatia Kanuni, Sheria na Taratibu za Wizara.

Kutokana na hayo yote Chuo hicho kimejikuta kikiingia kwenye mgogoro wa muda mrefu na mkubwa na kupelekea shughuli zote za kiutendaji chuoni hapo kutofanyika katika viwango vyenye ubora na kwa wakati na hasa pale anaposafiri mambo huwa yanasimama, kwani mara nyingi utendaji wote anaufanya yeye mwenyewe na wakati mwingine huwa anajiita Chief Accountant na kumuona Makamu wake kuwa hana uwezo wala mamlaka ya kutoa maamuzi kwa mustakabali wa chuo

Ni mengi ambayo nimeyabaini na ushaidi upo wazi kuwa Mkuu huyo wa Chuo hafai kuendelea kuongoza Chuo hicho kwani Wakufunzi, Wafanyakazi na Wanachuo hawana imani nae, na wanafanya mambo mengi bila morari ya utendaji kutokana na mazingira mabovu ya utendaji kazi katika chuo hicho

Nimefanya jitihada za kukutana na baadhi ya Wakuu wa Idara Chuoni hapo na kupata majibu ambayo yanaonyesha ukataji wa tamaa kutokana na mazingira mabovu ya kiutawala ambayo yanaonyeshwa na Mkuu wa Chuo hicho katika kufanikisha mpango mkakati wa matokeo makubwa sasa,

Pia nimebahatika kuwauliza viongozi wa Bodi akiwemu Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo ambaye amejitambulisha kwa jina la H,Lugome naye pia ameonyesha masikitiko makubwa sana juu ya utendaji wa Mkuu wa Chuo hicho

Lakini pia Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti ambaye pia ameshiriki kusuluhisha mgogoro huo katika kikao chake cha April 27, 2013 lakini ameshindwa na kukata rufaa kwa kulipeleka swala hilo kwa Mkuu wa Mkoa ili aweze kuliingilia kati

Naye Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu Philipo Mulugo alipo tafutwa kupitia simu yake ye kiganjani yenye namba hii 0754315922 alijibu kuwa swala hilo bado halijafika mezani kwake na endapo likifika basi atachukua hatua stahiki za kinidhamu na kisheria dhidi ya Mkuu yoyote wa Chuo ambaye atakwamisha malengo na ufanisi wa kazi nchini

Kutokana na hayo na mengine mengi ni dhahiri kuwa utendaji wa kazi katika chuo cha Ualimu Songea kilichopo eneo la Matogoro Mkoani Ruvuma wilayani Songea ni mgumu miongoni mwa Wafanyakazi na kusababisha hali ya sintofahamu katika Saikolojia zao na mustakabali wa Elimu ya wanachuo

Ni vema sasa mamlaka zinazohusika zikachukua hatua stahiki za kumaliza mgogoro huo ikiwemo na kumuondoa Mkuu huyo wa Chuo ili kurudisha Amani na Utulivu chuoni hapo miongoni mwa wanajumuia wanaokizunguka chuo hicho ili kuweza kufanikisha mikakati mbalimbali iliyopo nchini ya kuhakikisha kuwa elimu bora inafikiwa nchini hapa

Mwandishi wa Makala hii
Anapatika kwa 0755-335051 AU 0715-335051Barua pepe,stephano12mango@yahoo.com
 
Mhmhmh hii kali ya mwaka, inaonekana huyu jamaa ni bedui kishenzi! Lakini haiwezekani akafanya madudu yote hayo kisha akafumbiwa macho tu. Nachelea kusema huyu jamaa lazima atakuwa analindwa na vigogo huko wizara ya elimu maana kwa majanga uliyoyasema hapo juu kama ni kweli lazima atakuwa anashirikiana na Amimu a.k.a mzee wa zimbambwe na zanzibar!
 
Nilisoma hapo ila hakukua na madudu hayo! Is only when he thinks he wont die let him behave that way.
 
Ahsante sana Bw. Mango kwa makala yako yenye kutufumbua macho sisi wadau wa elimu hapa nchini, lakini ukiwa kama mwandishi mwenye weredi wa uandishi wa habari mbona huja balance story yako kwa kumtafuta huyo Mkuu wa Chuo cha Ualimu Songea ili athibitishe ukweli wa tuhuma hizi na badala yake umeongea na Mkuu wa Wilaya ya Songea na Naibu Waziri wa Elimu. Sitaweza kuamini hizi shutuma moja kwa moja kwani umekuwa biased mno.
 
Wabogojo......wewe huyu ubaya ni jamaa yako au?? mwache jamaa wamchane bana....maana yaonekana huyu jamaa ni kauzu sana! huyu jamaa yaonekana!
 
Tarizo la wakuu wa vyuo ni kuwa hawana elimu ya kiuongozi.... Hawalijuwi walitendalo!!! Ni kero kwenye vyuo vya ualimu'!!!

Wanatumia zaidi andalio
La somo kuongoza watu!!! Badilikeni, wizara iteuwe watu wenye japo postigraduate studies za taalumA za uongoz kama MBA, MPA , HRM na zingine!!!! 90% ya wakuu wa vyuo wote ni matutusaa!!!! Mbululaz....
 
MWANAKA, Sio kila post lazima uchangie ili na ww uonekane upo JF. Japokuwa mimi si mchangiaji mzuri sana wa posts za JF ila kukuthibitishia kuwa post hii unaukweli ndani yake ni kwamba kwa mara ya kwanza nimeiona post inayofanana na hii yenye ujumbe kama huu katika mtandao wa kijamii wa TANURI LA FIKRA yapata miezi miwili iliyopita. Hivyo basi tuepuke kubwabwaja midomo kama alivyofanya ndg. MWANAKA ili mradi tu eti tuonekane kwenye JF, JF si mahala pa majungu na kama mtu akifanya mzaha au uzushi basi lazima adabishwe kwa njia yoyote ili ajifunze na asirudie tena.

Mengi yamezungumzwa kuhusiana na huyo Principal wa Chuo Cha Songea coz hata FB kulikuwa na mada inasema "WELEDI WA WAKUU WA VYUO VYA UALIMU NA UTEUZI WAO" ambayo ilikuwa inazungumzia mapungufu yanayo onekana wazi kabisa kutoka kwa wakuu wa vyuo vya Ualimu vya serikali ambapo ilionekana Wanaowateua ndio chanzo cha matatizo yote haya kwani ilisemekana kuwa wengi wanateuliwa kulingana na sifa nje na taaluma na uwezo wa mtu binafsi kiuongozi, yaani uteuzi unatokana na ukaribu, undugu, urafiki, rushwa, kufahamiana, n.k. Wachangiaji wa mada ile walipendekeza nafasi kama hizo za UKUU WAVYUO zitangazwe na wajiriwe wenye sifa tu na si vinginevyo; Katika mada hii gumzo alikuwa huyo Principal wa Songea T.C kwani ilionekana yeye ndio kinara wa madhaifu miongoni mwa wakuu wa Vyuo hao.
MIMI BINAFSI niseme kuwa kama jamii yote unayoiongoza pia unatofautiana nayo basi ww si Kiongozi na kwa busara omba kuachia ngazi au omba kuhamishwa kituo cha kazi. Haingii akilini eti madhaifu yoote yaliyoonekana au kuonyeshwa bado aliyemteua (Mkurugenzi-Wizara ya Elimu) bado anamlinda kwa kusema hana hatia, IDIOT wakuu wote wenye hulka na maamuzi kama hayo!!!!
Elimu yetu haiwezi kuinuka kama wakuu wa Vyuo Vya Ualimu wako hivyo tunavyo sikia, hawa ndio huzalisha walimu wa S/M na Sekondari wasio na uwezo na kupelekea kudidimia kwa elimu yetu. Pia nilipata kusikia seke seke la Chuo Cha Ualimu Korogwe ambapo baada ya kuwatimua walio aminika kuwa walikuwa chanzo cha kupotea kwa morali za watumishi kufanya kazi kwa kujituma lakini Principal aliyepewa madaraka yasemekana kuwa yy ndio hakuna kitu kabisaa (source: Tanuri la Fikra). Kupitia ushahidi huu naunga mkono hoja ya nafasi ya Principals lazima zitangazwe na kuajiri watu wenye sifa na si kuteuana kama ambavyo inafanyika sasa.
CONCLUSION: Ikibainika yote yaliyozungumzwa na mwandishi kuwa yana ukweli kwa 1oo% basi huyo Mr. Ubaya afukuzwe kazi kwa masilahi ya Umma, yaani Hafai kuwa kiongozi wala kuwa Mwalimu
fanyeni kazi muache majungu
 
Intellectual unatakiwa kuchukua atua,sio kulalamika,,nilikuwa hapo kipindi cha mboza,,tulienjoy sanaaaaaaaaaaaaaaaaa,,,du! Majanga
 
Huna ulijualo ndio maana unabwabwaja tu, hivi hata kusoma hujui?? Katika taarifa hapo juu hujaona jinsi Wakufunzi walivyo-struggle japokuwa haijawa bahati yao?? Read and think before talking!!!!!

Mkuu hebu nitake radhi kwanza kwa kunisakama
Pili kumbuka jf ni jukwaa huru ambako kila mdau anaeleza kile anachokiona kwa fikra zake. Hebu rudia kulisoma bandiko lako na madai lukuki uliyoyatoa Bila shaka wadau watakubaliana nami kwamba maelezo yako yamekaa kiudakuudaku hivi kwa sababu mpaka sasa bado najiuliza msomi kama wewe kuwa mtu wa kulalamika wakati unajua fika kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na zipo mamlaka kibao za kuripoti hayo malalamiko yako
Acha kulalamika ndo maana kikasema fanyeni kazi acheni majungu
 
Tarizo la wakuu wa vyuo ni kuwa hawana elimu ya kiuongozi.... Hawalijuwi walitendalo!!! Ni kero kwenye vyuo vya ualimu'!!!

Wanatumia zaidi andalio
La somo kuongoza watu!!! Badilikeni, wizara iteuwe watu wenye japo postigraduate studies za taalumA za uongoz kama MBA, MPA , HRM na zingine!!!! 90% ya wakuu wa vyuo wote ni matutusaa!!!! Mbululaz....
HR, MBA aongoze chuo, taasisi ya kitaaluma? Sidhani kama ataweza Labda awe amesoma usimamizi na uongozi katika elimu sifa ambayo wakuu wengi wa vyuo wanayo.
 
MWANANKA, Sikutaki radhi kwa sababu yaonyesha ww ni slow learner. Kwanini nimesema wewe ni slow learner, anzia hapo kwenye nyekundu; mimi si mtoa mada hii.
Hapo kwenye blue;Nani kakudanganya kuwa ni rahisi kama unavyofikiri?? hata hivyo mtoa mada anasema kuwa Wafanyakazi wa Chuo husika waliweza kukaa vikao mbali mbali kuanzia ngazi ya Chuo, Bodi ya Chuo, Ngazi ya Wilaya, Ngazi ya Mkoa mpaka ngazi ya mwajiri wao (Wizara) lakini katika maamuzi Mr. Principal alibebwa kimaamuzi ndio maana Hii mada imefika hapa JF otherwise isingefika hapa. Je utawala wa sheria na mamlaka unazozizungumza wewe katika utumishi ni zipi kama suala limepita nyanja tajwa zote bila mafanikio???
Hapo kwenye Kijani; bwana mdogo nataka nikuelimishe kuwa laiti kama watu wasingekuwa wanalalamika na kupiga kelele kupinga mambo maovu na yasiyofanyika ipasavyo basi haya unayo yaona yakitekelezwa aidha na watu binafsi au Serikali basi yasingeweza kuibuliwa na kufanyika hata siku moja. Yaani sawasawa na Mabadiliko ya utendaji na uwajibikaji katika utumishi wa umma na Serikali kwa Ujumla yanavyofanyika kwa sasa baada ya kuwepo na upinzani unaoibua madhaifu yanayoshughulikiwa.
Yawezekana bado hujaingia katika system ya utumishi wa Umma hata Utumishi katika mashirika binafsi. UKIKUA UTAELEWA TU NGOJA KWA SASA NIKUACHE TU.
Mkuu hebu nitake radhi kwanza kwa kunisakama
Pili kumbuka jf ni jukwaa huru ambako kila mdau anaeleza kile anachokiona kwa fikra zake. Hebu rudia kulisoma bandiko lako na madai lukuki uliyoyatoa Bila shaka wadau watakubaliana nami kwamba maelezo yako yamekaa kiudakuudaku hivi kwa sababu mpaka sasa bado najiuliza msomi kama wewe kuwa mtu wa kulalamika wakati unajua fika kwamba nchi yetu inaendeshwa kwa utawala wa sheria na zipo mamlaka kibao za kuripoti hayo malalamiko yako
Acha kulalamika ndo maana kikasema fanyeni kazi acheni majungu[/QUOTE]
 
Huna ulijualo ndio maana unabwabwaja tu, hivi hata kusoma hujui?? Katika taarifa hapo juu hujaona jinsi Wakufunzi walivyo-struggle japokuwa haijawa bahati yao?? Read and think before talking!!!!!

Wewe ni mtu mwenye uwezo mdogo sana wa kufikili,,sasa unaleta story badala ya fact!umekutana na muhusika?sasa hizo habali zako inawezekana umezitunga tu,,be critical,,,hizi sio dhama za kulalamika katika vyombo vya habari,,,au mitandao ya kijamii,,,mkuu wa chuo awezi kufanya mambo haya ambayo wewe unasema,,taasisi yoyote ya serikali inataaratibu zake za kiutawala,yaani we,,nenda kawadanganye fb huko,,,,,
 
#KG .KASELO, nipo hapa kwa ajili ya kuwaweka sawa watu kama ww, wachangiaji wakurupukaji; Kwanza kabisa nasikitika kusema kuwa hujui kiswahili soma kwenye hayo maandishi mekundu then ujipime kuwa ww ni mtu wa level ipi interectually, kama mm nina uwezo mdogo basi tambua kuwa ww ni sifuri kabisaaaa..... Term CRITICAL characterized by careful, exact evaluation and judgement etc. kwa kumsaidia Mwandishi wa thread hii kaonyesha yoote yaliyofanyika kuanzia ngazi ya chini mpaka kwa Mwajiri wao therefore kwa kufuatia mtiririko huo at least yupo very Critical kwa sababu hii habari kaipata ktk level ya primary source kwa kuletewa au kuwauliza wale walioonewa na kunyanyasika.
Ulivyo hujui hata kusoma umeshindwa hata kumtambua Mwandishi wa hii thread nani angali kaweka hata jina lake na mawasiliano yake barabara, huyu bwana ni Mwandishi na si mpika taarifa kama ww.

Soma hapo kwenye Blue; kwanza kabisa nakana kuwa mimi ndio mwenye hii thread la hasha, pili nimetambua kuwa ww bado bwana mdogo sana ambaye hujui A wala B za utumishi wa umma ndio maana Mkuu wa Chuo unamuona ni Mungu Mtu ambaye hawezi kufanya haya yaliyoelezwa na mpasha habari, ukiingia katika utumishi aidha wa Umma au Taasisi/NGO binafsi ndio utapata ushahidi kuwa haya ambayo unabisha kufanyika basi ni mambo ya kawaida sana kwa watu ambao wanapewa fursa/Madaraka kama Mkuu wa Chuo tena mwenye Cheo cha Kuteuliwa. Naomba nimpongeze mtoa thread hii kwa kusema ndugu #GK .KASELO, Mwenye thread katoa habari ambayo mimi na wachangiaji wengi tu tunaamini kuwa yanafanyika/yamefanyika, ni wakati wako sasa kukanusha critically ili tutambue kuwa huu ni uzushi ambao unatakiwa ukanyike hukooo FB, GK.KASELO my friend otherwise NO EVIDENCE NO RIGHT TO SPEAK PUBLICALLY. Ahsante

Lakini nadhani,message yangu umeipata,,,mimi ninachokishangaa ni kwamba,,unadai vikao vimefanyika,,ngazi zote chuo,,i mean mkuu na wafanyakazi wote,,mkuu wa wilaya anajua,wa mkoa anajua,,,hivi watu wote hawa,,awajachukua maamuzi yoyote?ok.kama ni hivyo kwa nini hawa subordinates wasipeleke taarifa idala ya utumishi wa uma?wewe unadhani kunakiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kubuluza wenzio kama mbwa?pamoja na kwamba unadharau mchango wangu,inawezekena mimi nafahamu sana mazingira ya hapo,,lakini unachokisema na unachotaka watu wakiamini,kama ni kweli,,basi chuo cha ualimu songea kitakuwa ni cha mtu sasa.na sio cha serikali.mimi binafsi msimamo wangu ni kwamba kuna waandishi wengi sana hapa Tz,kama wewe,kazi yao ni kudanganya uma,na kuvuruga wananchi.acha hizo,,,kama wewe,hiyo ni taaluma yako!basi ludi darasani tena kajifunze maadili ya taaluma hiyo.:A S-confused1:
 
Kwa kukusaidia tu, ww ndiye unayetakiwa kurudi Darasani,tena ukaanze na kusoma lugha nyepesi ya Kiswahili kwa kuanzia na maneno yaliyoandikwa kwa wino mwekundu. Infact mimi si Mwandishi wa Habari...Professionally mimi ni IT Engineer brother hapa ni mchangiaji wa kawaida tu kama wewe. Ila kwa sasa naomba nikuache coz you are not ready to learn.

Back
Top Bottom