Hali tete kwa wakulima, mbolea kg 50 yafikia 120,000

Yote hii inasababishwa na matumizi ya anasa ya serikali, na Ufisadi wa baadhi ya viongozi

Kunatakiwa uwajibikaji kwa viongozi... KATIBA MPYA
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Wewe una utaalam wowote katika kilimo mkuu?

Au, wewe kweli ni mkulima? Maana lugha yako haieleweki kabisa!

Kama ulishakaa ndani ya darasa na kujifunza mambo ya kilimo, halafu matokeo yake ndiyo kama uliyoeleza hapa, hili taifa litakwenda wapi?

Naona una 'Bemendazole' hapo, sasa sijui uko kwenye mifugo? Maana hata kwa binaadam isingekuwa hivyo!
 
Asee ni wazi kabisa kwamba mkulima hana chake kwenye hii nchi
 
Wewe una utaalam wowote katika kilimo mkuu?

Au, wewe kweli ni mkulima? Maana lugha yako haieleweki kabisa!

Kama ulishakaa ndani ya darasa na kujifunza mambo ya kilimo, halafu matokeo yake ndiyo kama uliyoeleza hapa, hili taifa litakwenda wapi?

Naona una 'Bemendazole' hapo, sasa sijui uko kwenye mifugo? Maana hata kwa binaadam isingekuwa hivyo!
Acha longo longo. Lima alizeti/ ufuta, uondokane na umaskini. Mahindi sio ndugu yako. Kwa nini unang'angania kuyalima? Utakufa masikini.
 
Wakulima watalima vipi kipindi hiki mbolea ambayo tulinunua kwa elfu 60 Sasa imefikia elf 95 laki mpaka laki na ishirini.

Sasa najiuliza itakuwaje kama Sasa hivi gunia la mahindi kwa eneo nililopo ni elf 24 wakati Bei ya mbolea ni laki na ishirini.

Kwamba unatakiwa kuuza gunia 5 Za mahindi ili kununua mbolea mfuko mmoja .

What a failed state!!!
Mkuu

Mbona kuna mdau alishusha uzi humu akisifia kwamba rais ameshusha bei ya pembejeo kwenye korosho kama mbolea na madawa kumbe alikuwa anawaandaa watu kisaikoloji?

Maisha kwa sasa yamekuwa magumu sana kuliko wakato wowote maana unamkuta mtu kamaliza chuo cha UDSM kazi ambayo zamani ilikuwa haiwezekani na ni mtaalamu wa uhandisi mawasiliano, sheria, mazingira, uahasibu nk..

Kupata kiwanja Dsm kwa sasa kwa viwango tofauti ni kuanzia milioni 2 ukubwa wa 15 kwa 10, 15 kwa 18, 20 kwa 20, 20 kwa 25) hadi milioni 100 eka moja hadi tano. Kwanja cha milioni moja, milioni moja na laki tano utapata nje ya Dar hasa wilaya ya Chalinze, Kisarawe, Mkuranga na kwa uchache baadhi ya sehemu za Bagamoyo kule Fukayosi, Makurunge na Mwavi lakini sio Bagamoyo karibu na mji au Kiwangwa au Msata huko ni balaa.

Maisha yataendelea kuwa magumu lakini wanasiasa wataendelea kuwakejeli wananchi mpaka uchaguzi ukikaribia wanajifanya kuja kuwapigia magoti wapiga kura kwa kuwapa zawadi ndogo ndogo kuwasahaulisha mateso waliyowapa kwa kushindwa kuwasikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi mara moja.
 
Acha longo longo. Lima alizeti/ ufuta, uondokane na umaskini. Mahindi sio ndugu yako. Kwa nini unang'angania kuyalima? Utakufa masikini.
Wewe ni kilaza kwelikweli. Unataka wakulima wote Tanzania wahamie kulima hayo mazao pekee, itawezekana wapi hiyo kama sio kujitoa akili kichwani.

Ni kama hiyo 'Bemendazole' yako, unataka minyoo ya aina zote itibiwe na bemendazole badala ya "mebendazole" ?
Ukweli ni kwamba hakuna lolote unalolijua. Ni ubabaishaji tu, uliojaa siku hizi kila mahala ndani ya nchi hii. Kila mtu anajifanya mjuaji kwenye jambo ambalo hana chochote anachokijua.
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Achana na hizi theory mfu ni zao gani sasa hivi lina bei kubwa?
 
Wewe ni kilaza kwelikweli. Unataka wakulima wote Tanzania wahamie kulima hayo mazao pekee, itawezekana wapi hiyo kama sio kujitoa akili kichwani.

Ni kama hiyo 'Bemendazole' yako, unataka minyoo ya aina zote itibiwe na bemendazole badala ya "mebendazole" ?
Ukweli ni kwamba hakuna lolote unalolijua. Ni ubabaishaji tu, uliojaa siku hizi kila mahala ndani ya nchi hii. Kila mtu anajifanya mjuaji kwenye jambo ambalo hana chochote anachokijua.
Ndiyo maana serikali ya Siro haitaki vyama vya siasa kufanya mikutano ya siasa.
 
Nilikuwa morogoro mwez uliopita nikakuta mbolea ni elf82 kutoka tshng 52,

Alafu gunia moja la mpunga ni elf60, wananchi wamechoka kinoma aisee
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Tatizo kubwa la bei ya mahindi linatokana na serikali kuingikia na kuvuruga soko.

Tangu Majaliwa alipovuruga soko la mahindi mwaka 2018, mpaka leo hakujawahi kuwa na bei nzuri.

Viongozi wetu wana upeo mdogo sana kuhusu biashara na uchumi. Hawajui kuwa masoko yanatafutwa, yakipatikana yanalindwa. Umetafuta soko la nje, kukitokea tu upungufu wa mahindi ndani ya nchi, utasikia Serikali imezuia kupeleka mahindi nje! Yakiwa mengi, utasikia kuwa Serikali imeruhusu kuuza mahindi nje! Ni upumbavu mkubwa! Hivi huko nje walikuwa wamekaa kusubiria mahindi ya Tanzania?

Bila ya kupata viongozi wenye upeo mkubwa, nchi haitakuja kufika popote kiuchumi.
 
Mkuu

Mbona kuna mdau alishusha uzi humu akisifia kwamba rais ameshusha bei ya pembejeo kwenye korosho kama mbolea na madawa kumbe alikuwa anawaandaa watu kisaikoloji?

Maisha kwa sasa yamekuwa magumu sana kuliko wakato wowote maana unamkuta mtu kamaliza chuo cha UDSM kazi ambayo zamani ilikuwa haiwezekani na ni mtaalamu wa uhandisi mawasiliano, sheria, mazingira, uahasibu nk..

Kupata kiwanja Dsm kwa sasa kwa viwango tofauti ni kuanzia milioni 2 ukubwa wa 15 kwa 10, 15 kwa 18, 20 kwa 20, 20 kwa 25) hadi milioni 100 eka moja hadi tano. Kwanja cha milioni moja, milioni moja na laki tano utapata nje ya Dar hasa wilaya ya Chalinze, Kisarawe, Mkuranga na kwa uchache baadhi ya sehemu za Bagamoyo kule Fukayosi, Makurunge na Mwavi lakini sio Bagamoyo karibu na mji au Kiwangwa au Msata huko ni balaa.

Maisha yataendelea kuwa magumu lakini wanasiasa wataendelea kuwakejeli wananchi mpaka uchaguzi ukikaribia wanajifanya kuja kuwapigia magoti wapiga kura kwa kuwapa zawadi ndogo ndogo kuwasahaulisha mateso waliyowapa kwa kushindwa kuwasikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi mara moja.
Kwenye korosho hapana maana pembejeo bei zimeongezeka mara 2, ukiachilia mbali uwepo wa pembejeo feki, zilizoexpire na kutofika kwa wakati
 
Inategemeana na vitu Kama mvua,mbegu,palizi,Aina ya udongo nk.hakuna jibu sahihi hapo.
Kama unataka kulima kitaalam, ekari moja inatumia mifuko 3 ya kupandia, 3 kukuzia mara ya kwanza, na mitatu mingine kukuzia mara ya pili. Jumla mifuko 9. Utahitaji mbegu za kisasa nadhani kama kilo 40.

Gharama:

Mbolea sh 9×120,000=1,080,000
Mbegu sh 40×8,000 = 480,000
Kulima ekari 1 sh 80,000
Kupalilia mara 2 sh 100,000
Kuvuna, kupukuchua na kusafirisha sh 200,000

Jumla ya gharama sh 1,940,00

Mapato:
Mavuno magunia 20
Fedha magunia 20×24,000 = 840,000

Jumla ya mapato sh 840,000

Lazima uwe kichaa kulima mahindi.
 
Tatizo kubwa la bei ya mahindi linatokana na serikali kuingikia na kuvuruga soko.

Tangu Majaliwa alipovuruga soko la mahindi mwaka 2018, mpaka leo hakujawahi kuwa na bei nzuri.

Viongozi wetu wana upeo mdogo sana kuhusu biashara na uchumi. Hawajui kuwa masoko yanatafutwa, yakipatikana yanalindwa. Umetafuta soko la nje, kukitokea tu upungufu wa mahindi ndani ya nchi, utasikia Serikali imezuia kupeleka mahindi nje! Yakiwa mengi, utasikia kuwa Serikali imeruhusu kuuza mahindi nje! Ni upumbavu mkubwa! Hivi huko nje walikuwa wamekaa kusubiria mahindi ya Tanzania?

Bila ya kupata viongozi wenye upeo mkubwa, nchi haitakuja kufika popote kiuchumi.
Sio Majaliwa. Wa kulaumiwa ni Mzitto Kabwela aliyekuja na propaganda kuwa kuna njaa nchini. Wakatengeneza na picha kuonesha watu wanakula nzige. Majaliwa alichofanya ni kucheza part yake ya kuhakikisha kuwa kuna stock ya kutosha.
Nakumbuka that time when I saw him 'scrambling' a small plane to Katavi to verify if there were enough stock on national reserve!
 
Wewe ni kilaza kwelikweli. Unataka wakulima wote Tanzania wahamie kulima hayo mazao pekee, itawezekana wapi hiyo kama sio kujitoa akili kichwani.

Ni kama hiyo 'Bemendazole' yako, unataka minyoo ya aina zote itibiwe na bemendazole badala ya "mebendazole" ?
Ukweli ni kwamba hakuna lolote unalolijua. Ni ubabaishaji tu, uliojaa siku hizi kila mahala ndani ya nchi hii. Kila mtu anajifanya mjuaji kwenye jambo ambalo hana chochote anachokijua.
Kwa hiyo wewe mjuaji unatushauri nini mara baada ya kumaliza kunikandia? 😀
 
Hatimae mimi nimevuna gunia 6 za mahindi ndani ya hekari moja uku gharama nilizotumia zikiwa juu kuliko mapato
 
Tatizo la bei ndogo ya mahindi ni tatizo la miss divesification/ crop miss rotation au mono cropping kwa lugha rahisi. Hii inatokea pale wakulima wengi wanapoamua kulima zao la aina moja. Iwapo wakulima wengi wangejikita kwenye kilimo cha fursa, huenda wangelima mazao kama alizeti na ufuta ambayo yana bei nzuri sokoni na kulima mahindi kidogo kwa ajili ya chakula.
Sio kweli mkuu nimepita baadhi ya maeneo mengi mwaka huu zao la mahindi halijatoka kwa kiwango chakuridhisha shida ni bei ya soko ,mahindi yalikuwa hayatoki kwenda nje kwa sasa yanatoka ila still bado bei hairidhishi ingali bei ya mbolea inazidi kupanda mara dufu huku nikisikia kenya kuna njaa na bado kwao mbolea ni bei ya chini ikiwa urea kg 50 ni elfu 60 huku kwetu ni zaidi ya elfu 80 nishauri tuu tuuze mahindi kenya wao wauze mbolea kwetu
 
Back
Top Bottom