TikTok2020
JF-Expert Member
- Oct 20, 2022
- 1,816
- 3,150
Kwa masikitiko makubwa naomba serikali iingilie kati suala la VIVUKO VYA KIGAMBONI kutokana na hali ya uchakavu iliyopo katika VIVUKO hivyo ili kunusuru majanga yanayoweza kutokea.
Tangu hii wiki ianze wananchi wamekuwa wakiteseka sana pale kwa foleni ndefu magari na mlundikano mkubwa kwenye zile sehemu za kukaa abiria kitu ambacho si salama kiafya lakini inaonekana hakuna hata mtu anaejali kuhusu hilo.
Leo jioni kumetokea sintofahamu kwenye Mv Kigamboni kuzima katikati ya maji na kulazimika kurudi Kivukoni na kushusha abiria.
Kinachosikitisha zaidi huwezi kukutana na habari hii kwenye chombo chochote cha habari nadhani wanasubiri taarifa za maafa ndio wazipe kipaumbele.
Serikali tunaomba muingilie kati hili suala