Najua kutokana na kiwango kibaya cha masomo Bongo, watu hata wale unaodhania kidogo wameelimika , kama wale wanaochangia humu, huonesha dhahiri kiwango kibovu cha elimu. Mfano nimesoma mchango wa mtu anayeandika laisi (rahisi au rais),hatali, aluki (haruki), lizika (ridhika), galama (gharama) n.k. Ajabu ni kuwa mara nyingi hawafanyi makosa hayo wanapoandika Kiingreza! Nataka kumsahihisha Kivumah juu ya kauli mbiyu ya zamani ya TANU. Ili tuendelee....' ya mwisho ni UONGOZI BORA na si UTAWALA BORA. Katika Kiswahili, tofauti ya utawala na uongozi ni kubwa. Utawala ni ule unaofanywa na mgeni juu ya wazalendo. Iwapo mtawala ni mzalendo, yeye huitwa kiongozi na 'utawala wake' huitwa uongozi. Vijana wa siku hizi hawapambanui kati ya haya. Utawakuta wanasema, utawala wa Kikwete!