Hali ya biashara ya daladala mkoa wa Lindi ikoje?

Hali ya biashara ya daladala mkoa wa Lindi ikoje?

upeo

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2013
Posts
369
Reaction score
218
Wakuu nataka kuhamishia gari yangu aina ya costa mkoa wa Lindi.

Je, biashara ya daladala inalipa huko?

Nimesikia kwa siku unalaza laki je ni kweli?

Naomba wakaazi wa Lindi wanipe ufafanuzi wa hili kabla ya kuihamishia gari yangu huko.

Asanteni wakuu.
 
Mkuu katika biashara usisikilize maneno ya watu kulaza Laki kwenye daladala ni kawaida sana nilishawahi kuwa konda kipindi nasubiria majibu yangu ya kidato cha Nne huko dodoma tulikuwa tunalaza mpaka laki na 80 boss anapewa yake 50 inabaki laki na 30
Mafuta ya elfu 50 inabaki elfu 80 tunagawana na dereva .

ila ndio ile kitambo sasa hivi biashara ni ngumu bajaji,bodaboda zimeharibu sana tripu za daladala kwa mikoani ila ukikaza sana unapiga yulo kiroho safi .

Hapa cha kukushauri nenda .mwenyewe mpaka lindi kacheki trip au kipande kama kina urefu kiasi gani? Changamoto ya barabara na bei ya vituo then ndio uangalia kama unaweza kupeleka costa yako na kupata faida.
 
nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom