Pre GE2025 Hali ya internet ikoje maeneo ulipo? Unaweza kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii bila shida?

Pre GE2025 Hali ya internet ikoje maeneo ulipo? Unaweza kuperuzi kwenye mitandao ya kijamii bila shida?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndio Kuna changamoto ya mtandao ila kwako kama imezidi hv au
😀😀 naona ndio hali halisi, labda kwasababu natumia sana telegram na JF hivyo kila mtandao unavyoyumba lazima nii-experience
 
Mimi natumia fiber ya tigo yani since last week imekuwa shida.... ina upload speed kubwa ya over 30mbs lakini download speed inachechemea sana kiasi kwamba wakati mwingine kupakua pages ni shida.
Pole sana Mkuu
 
Mtandao umekuwa changamoto kubwa sana, kama kwangu Voda, Tigo na Airtel imekuwa shida kubwa kuingia Jukwaani na Telegram.

Nalazimika kuzima na kuwasha VPN Ili kupata huduma
Telegram kufanyaje??😵
 
Wakuu salam,

Hivi karibuni internet imekuwa changamoto kweli, wakati mwingine unakuwa huwezi kufanya chochote zaidi ya kucheza game. Kadri siku zinavyoenda hali inazidi kuwa mbaya

Na hii ni kwenye mitandao yote, unataka kununua umeme unaambiwa mtandao unasumbua, una ka intavyuu ka mtandaoni siku hiyo internet hakuna, wakati mwingine huwezi kutumia baadhi ya sites mpaka utumie VPN.

Wakati huu ambao mambo mengi yanaishia kufanyika mtandaoni inakuwa kero na vitu vinakwamba.

Voda waliahidi huduma zao kurejea vizuri katikati ya November, mmeona mabadiliko yote? Juzi tu hapa Mpesa iligoma siku nzima, imagine ndio una dharura!

Vipi upande wako, hali ikoje?
usjali mkuu uchaguzi wa serikali za mtaa ukiisha mambo yakua poa kama mwanzo,,then uchaguzi mkuu mambo takuwa zaidi ya haya!!!''''''''wapinzani wanabanwa wasiwasiline kirahisi!!!!,,,,,,wee unafanya mchezo nini!
 
Telegram kufanyaje??😵
Kupata habari na taarifa mbalimbali kama ilivyokuwa mitandao mingine ila huku hakuna mbambamba zile zinazotokea watsap na insta kuzimwa au kutopatikana mara kwa mara, unaweza kuchat na mtu bila kukeep convo (ukaweka muda wa kupotea na mtu hana uwezo wa kuchukua risiti, etc) unadhani kwanini Gen Z Kenya walikuwa wanaitumia sana kipindi cha maandamano?
 
Back
Top Bottom