Hali ya Jack gerezani Macau siyo nzuri

Hali ya Jack gerezani Macau siyo nzuri

Rich Pol

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2013
Posts
7,874
Reaction score
5,685
UNAWEZA kusema ni majanga juu ya majanga yanazidi kumkumba modo wa Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack' baada ya wiki iliyopita kushindwa kupanda kortini kufuatia kutetereka kwa afya yake bila kufafanuliwa. Mbali na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za msingi za kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya mtu aliye kifungoni.

Akizungumza juzi jijini Dar, mtu anayejitolea kumpa msaada na kumtembelea Jack mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda- alisema Jack anaumia kwa kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona bora hukumu yake ipite ajue moja. "Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.

"Halafu kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama mahabusu na amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi hiki wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo labda kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana uwezo.

"Wabongo wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo kidogo wanakwenda kumtembelea siku mojamoja," alisema Matilda.
Juni 20, mwaka huu, Mbongo Fleva anayedaiwa ni mtu wa karibu na Jack, Juma Khalid ‘Jux' na kumuuliza kwa nini hajawahi kwenda kumtembelea ‘bebi' wake mahabusu kama wanavyofanya Wabongo ambao wako Macau, akajibu: "Sipendi kusikia ishu yoyote inayomuhusu Jack kwani nina mambo mengi ya kuongelea na si ishu za Jack kila kukicha.

"Kwa kipindi hiki sitahitaji mtu aniulize ishu za Jack, zinanitibua sana na kama kuongelewa zimeshaongelewa hivyo sioni kipya." Hii ni mara ya tatu kwa Jack kupanda mahakamani, mara ya kwanza ilikuwa Aprili 10, mwaka huu kosa likiwa kukutwa na madawa ya kulevya tumboni aina ya heroin kete 57 au kilo 1.1 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 223. Mara ya pili ilikuwa Mei 23, mwaka huu
 
Ahaa ashukuru yuko macau china bongo hapa wenzie wananyea kwenye ndoo
 
Hivi nae ni mmoja kati ya wale 65 wanaotarajiwa 'kunyongwa' huko china?

Serikali ya GREENLABEL haijatoa tamko lolote juu ya hawa wananchi mpaka sasa?

Mbona nchi nyingine zinawatetea raia wake mpaka kwenye makosa mazito sana? iweje Tanzania?

Kwanini uongozi wa GREENLABEL uko kimya jamani juu ya watu wake ambao wanakaribia 'kukatwa vichwa' karibuni?
 
Hivi nae ni mmoja kati ya wale 65 wanaotarajiwa 'kunyongwa' huko china?

Serikali ya GREENLABEL haijatoa tamko lolote juu ya hawa wananchi mpaka sasa?

Mbona nchi nyingine zinawatetea raia wake mpaka kwenye makosa mazito sana? iweje Tanzania?

Kwanini uongozi wa GREENLABEL uko kimya jamani juu ya watu wake ambao wanakaribia 'kukatwa vichwa' karibuni?

serikal imechoka kubadilishana wafungwa wake na rasirimal mwisho zitaisha sasa kila mtu akishikwa serikal itoe mgod ili aachiwe....
 
Tujiulize, Jack ana umuhimu gani hapa Tanzania mpaka serikali ya GreenLabel itutelekeze tena kwa kugawa mali ghafi zetu kwa mtu kama Jack? Kiukweli serikali imechoka kwani wakiendelea kutetea wauza unga kwa rasilimali zetu hii nchi itazidi kujaa wawekezaji wa kuuza kahawa, kandambili mtaani, na wa kufyeka majani wakati majirani zetu wana wawekezaji wa viwanda sie tunajaza machinga.
 
Hivi nae ni mmoja kati ya wale 65 wanaotarajiwa 'kunyongwa' huko china?

Serikali ya GREENLABEL haijatoa tamko lolote juu ya hawa wananchi mpaka sasa?

Mbona nchi nyingine zinawatetea raia wake mpaka kwenye makosa mazito sana? iweje Tanzania?

Kwanini uongozi wa GREENLABEL uko kimya jamani juu ya watu wake ambao wanakaribia 'kukatwa vichwa' karibuni?[/QUOTE
Japokuwa ni sehemu za kiutawala za jamhuri ya watu wa china, Macau na Hongkong wao hawanyongi, ila china mainland wao ni kitanzi tu, ashukuru walimnasa Macau, maana alipokuwa anaelekea Guanzhou sehemu ya mainland huko pangechimbika
 
itabidi wa TZ tumuombee shujaa huyu wa Taifa jamani

Weeeeee!!!! Kwa ushujaa gan zaid n mmoja kat ya watu wanaopoteza nguvu kaz kwa madaw!!! Wenzio wananyea debe huku. Afanye tu kaz hzo aache ulele mama.altumwa abebe hzo heroin..mxyuuuuuuu
 
Akisalimika akarudi nchini sujui kama atakuwa punda tena, mala nyingi wanaacha, na kama hajawekaza lazima aanze kujiuza, inaonekana relationship yake na Jux it's Over! What goes around comes around, yametimia, alichomfanyia mume wake wa ndoa nae yamemtokea, kweli adhabu siku hizi ni hapa hapa duniani.
 
Wabongo baadhi hatiuko wavumilivu wakati wa shida, akibahatika kutoka Jux atarudi tena na "Baby am sorry let's forget the past.
 
Ujinga wake ndio ulimpeleka huko, No fast money. Fanya kazi ule sasa wewe hufanyi kazi unategemea nini.
Tena wakunyonge kabisa
 
serikal imechoka
kwa kazi ipi iliyofanya? serikali hii hii ambayo inaendeshwa kwa mipasho na majungu? lazima kuwe na plan ya kuinua maisha ya wananchi wake na kuwamalizia kama si kuwapunguzia matatizo wananchi wake!!! Serikali yetu imeoza, ka,a si kunuka kabisa! kuna nchi ngapi wananchi wake wanauza madawa lakini serikali zinafanya jitihada za kudhibiti?

Hivi inakuwaje mheshimiwa R anasema eti 'mjisalimishe baada ya wiki' ? badala ya kuwakamata baada ya wiki?
that means kuna vitu vingi sana anavifahamu lakini anamezea tu kwa vile familia yake haiguswi, inaishi kwa neema za kodi za wananchi!


kubadilishana wafungwa wake na rasirimal
hapa unamzungumzia nani mkuu? tafadhali sema ukweli, kuna ishu inanuka tu hapa mtaani, sina uhakika nayo sana.. mwaga info kama unazo!

mwisho zitaisha sasa kila mtu akishikwa serikal itoe mgod ili aachiwe
rasilimali za nchi zinazidi kuteketea kwa mipango mibovu ya serikali pamoja na mikataba feki feki inayosain kila siku!
mpaka wananchi wenyewe hawajafunzwa jinsi ya kutumia rasilimali hizo kwa usahihi, unadhani watajua nini kinachowazunguka??? nchi inatafunwa na hao wanaojifanya wanatutetea!
 
Duuh Lukuvi na kimbelembele chake yuko wapi.? Masogange ule mpododo ulimpa utetezi mwe..! Hivi Lukuvi hajaupumulia kweli?
 
demu yupo katika kipindi kigumu... jux kamkimbiaa na gereza hilooo linamuita :A S 109:
 
Bora anyongwe tu kijulikane kuliko kumtesa mtoto wa watu....

Tuungane kumuombea kijana mwenzetu hukumu yake yKunyongwa iwahishwe apumzke tu 😡
 
Serikali ya tanzania ingekuwa inasheria kali kama za china pengine matatizo ya madawa yangepungua sana.huyu ni mmoja wa waathirika wa madawa ya kulevya hapa china.nlimkuta amekaa pembeni ya barabara hapa kitongoji cha xiaobei mjini guangzhou.kama mnavyomuona ameisha kabisa na kubaki mifupa mitupu,pengine jack patrik angefanikiwa kupita pale macau na kuingia huku mainland huyu nae angekuwa mmoja ya watu ambao wangeutumia huo mzigo aliokuja nao.hawa wauza unga si wakuonewa huruma kabisa sababu ni wauaji wanaangamiza maisha ya vijana kama huyu.kesho kutwa wabongo zaidi ya hamsini wananyongwa huku.tuacheni tamaa jaman.tutafute rizki za halali
 

Attachments

  • 1403870830658.jpg
    1403870830658.jpg
    37.4 KB · Views: 994
Back
Top Bottom