GE2025 Hali ya kiafya ya John Heche yazidi kuzorota huko Mtumba, anyimwa haki ya dhamana na matibabu

GE2025 Hali ya kiafya ya John Heche yazidi kuzorota huko Mtumba, anyimwa haki ya dhamana na matibabu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Its Tesha

Senior Member
Joined
Oct 6, 2025
Posts
168
Reaction score
608
Siku ya 13 katika mikono ya polisi Ndugu WATANZANIA na wapenda Haki wote Ninasikitika kuwajulisha kuwa

Ndugu na kiongozi wetu John Heche amenitumia taarifa ya masikitiko kuhusu hali yake ya kiafya kuwa inaendelea kuzorota na hakuna dalili zozote za yeye kupata Haki ya dhamana ama ya matibabu ambayo ni Haki ya kikatiba na ya kuishi kwa pamoja.

Amekuwa akipata huduma za kwanza tu lakini zimeshindwa kubadili hali yake ya kiafya inayohitaji vipimo na matibabu ya ziada na ya kina sasa ambapo mwili unaendelea kudhoofu zaidi

Amenielekeza niwajulishe kuwa amekwishampatia OCCID (mkuu wa upelelezi ) taarifa kuwa sasa kama lengo ni kumuumiza yeye kuanzia kesho atasitisha kula ikiwa atapoteza maisha iwe furaha ya watawala na iwe hivyo.

Maana anajua na mbele za Mungu hana kosa la kusababisha kuwekwa kizuizini bila mashtaka muda wote wa siku 13 ambazo ni zaidi ya saa 312 ikiwa watawala walikuwa na sababu walipaswa kumfikisha mahakamani sio mateso.

Naomba pia wenye uwezo wa kumuita Mungu katika kusimama na hujuma hizi tuungane kumuita bila kusita.


Mwl. Chacha Heche
Ndugu na Katibu wa familia
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mara
 
Aisee Mungu ampe nguvu,ila tutaelewana tu na hawa madhalimu
 
Ngoja afie mikononi mwao tuone Wakurya wataamua nini huko Tarime!
 
Back
Top Bottom