Hali ya kibiashara itakuwa vipi baada ya makao makuu kuhamia Dodoma?

Hali ya kibiashara itakuwa vipi baada ya makao makuu kuhamia Dodoma?

RICH GANG LIFESTYLE

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2016
Posts
256
Reaction score
192
Habari za jioni wadau

Mimi ni mfanyabiashara wa kati hapa dar

in short wote tunafahamu jiji la dar liko vizuri kibiashara kwasbb ya uwepo wa ofisi kuu za serikali hapa moja ya point inayochangia kunifaisha jiji kibiashara

Swali langu ni kwamba endapo hizi ofisi za serikali zikihamia Dodoma je jiji letu la dar litaathirika kibiashara? Au litaendelea kuwa stable?
 

Inategemea biashara ya aina gani? Wewe unazungumzia biashara ya aina gani?
 
Usijali mkuu akuna atakayeweza kuubadilisha uchumi wa dar kwa sasa ata ofisi zikiamia Dodoma jua siyo zote kwa sababu makampuni makubwa hayawezi hamia Dodoma wananchi siyo wote watahamia Dodoma biashara zitaendelea kama kawa
 
Dsm itabaki kua jiji kuu la kibiashara Tz kutokana na kua na fursa nyingi zinazochangia ukuaji wa kibishara hasa wingi wa watu..bandari na kiwanja cha ndege cha kimataifa..

kwahiyo usihofu Dodoma utakua mji kwajili ya shughuli za kiserikali Dsm itakua ni business as usual
 
Mjifunze kutafuta biashara na sekta binafsi.

Kwa mwendo wa serikali hii mwelekeo ni kuwa na watumishi wachache, wenye weledi, wanaofanya kazi kwa ufanisi na kiteknolojia zaidi.

Serikali imeanza juweka fedha zake benki kuu na sio benki za biashara, kutumia miundombinu na taasisi zake kupata Huduma/bidhaa mfano kumbi zake zenyewe n.k

Vilevile, uamuzi wa kupunguza matumizi ya fedha za kawaida hasa posho na safari zisizo na tija utaondoa/punguza hicho unachoita biashara dar kutegemea taasisi za serikali. Hilo linaenda sambamba na kuongezeka kwa bajeti ya maendeleo ambayo kwa sehemu kubwa itaenda maeneo nje ya dar.

Uamuzi wa kuhamia Dodoma utaleta ubunifu kwa sekta binafsi kujitanua nje ya dar, kutotegemea sana serikali kibiashara, kuchukua fursa kutoa huduma mbadala kwa wananchi
 
Wenye nyumba zetu dodoma tunasubilia kwa hamu iyo ahadi itimie
 
Na miji ya jirani kama Iringa, Babati, Gairo na Singida/ Manyoni itanufaika sana kuwa karibu na jiji la Dodoma
 
Back
Top Bottom