Mjifunze kutafuta biashara na sekta binafsi.
Kwa mwendo wa serikali hii mwelekeo ni kuwa na watumishi wachache, wenye weledi, wanaofanya kazi kwa ufanisi na kiteknolojia zaidi.
Serikali imeanza juweka fedha zake benki kuu na sio benki za biashara, kutumia miundombinu na taasisi zake kupata Huduma/bidhaa mfano kumbi zake zenyewe n.k
Vilevile, uamuzi wa kupunguza matumizi ya fedha za kawaida hasa posho na safari zisizo na tija utaondoa/punguza hicho unachoita biashara dar kutegemea taasisi za serikali. Hilo linaenda sambamba na kuongezeka kwa bajeti ya maendeleo ambayo kwa sehemu kubwa itaenda maeneo nje ya dar.
Uamuzi wa kuhamia Dodoma utaleta ubunifu kwa sekta binafsi kujitanua nje ya dar, kutotegemea sana serikali kibiashara, kuchukua fursa kutoa huduma mbadala kwa wananchi