Habari zenu wakongwe..!?
Kuna hii hali ambayo huwa inanitokea mara kwa mara,yaani huwa inanikera ile mbaya..!
Yaani kuna wakati nikiwa napumua huwa nahisi hewa inataka kupitia kwenye masikio,yaani ni kama vile nasikia upumuaji wangu kupitia masikio..!
Mara nyingi huwa nahisi hii hali kama nimetembea mwendo mrefu,ila kuna wakati inakuja ghafla tu..!
Hii ni nini maana yake,ni tatizo la kiafya..?
Wataalamu naomba mnisaidie kupata majibu katika hili,maana hii hali ikitokea huwa inanikera sana..!