OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 426
- 685
Mmoja kati ya wachumi duniani anasema tupo katika Enzi ya Taarifa ‘Information age’ (O’Connor, 2005) kwa kiasi kikubwa huyu bwana ameonyesha namna ambayo taarifa zinavywaajiri watu. Katika hilo amezungumzia zaidi technolojia na mapinduzi yake tangu mwaka 1946 ilipoanza ENIAC Kwa kiasi kikubwa amezungumzia masuala ya ICT
Ni kwa namna hiyo hiyo (Goodman, 2015) ameelezea namna ambavyo makampuni ya teknolojia na taarifa yanakuwa ni makampuni ya bilions.
Japo anaheshimu uchumi wa viwanda lakini wasomi wameshaona kwa sasa taarifa ndio kitu kinachotengeneza pesa zaidi, thus mitandao kama Facebook nk inatengeneza billions of money, na Apps zikinunulika kwa hela nyingi japo yenyewe inatumiwa bure na watumiaji wake, wanapataje hela? Ni swala la taarifa
Kwa waafrika ambao mchango wetu kwenye tecknolojia ni mdogo hatuko nyuma kwenye kutengeneza pesa kupitia taarifa na maarifa, mfano watu wenye Page za instagram zenye followers wengi wamekuwa wakijipatia pesa kwa kupewa matangazo na baadhi ya watu na wao wakaweza kusukuma siku
Ama kwa hakika dunia ilionyesha mwanga wa kujiajiri kwa vijana ambao wamekuwa wakifundishana kwa makundi ya whatsapp kwa ujira kidogo wa kupata elimu mbalimbali za kutengeneza vitu mbali mbali au techniques za maisha
Hapo hatujazungumzia waliokuwa wanapata hela kidogo kwa kuwa na blogs au youtube channels ambazo zingeweza kuja online Tv na vijana kujipatia ajira nk. Kifupi ni kuwa, Hii zama za taarifa zimekuwa ni chanzo cha ajira kwa waliowengi katika nchi zinazoendelea
Sheria ya mtandao ya mwaka 2018 ilisababisha majanga kwa baadhi ya watu na watu wakajitune kivingine, lakini pia kwa sheria ya makosa ya mtandao ya mwaka 2020 imezidi kuwa mwiba kwa kuwazuia vijana hao kuweza kujiajiri bila gharama kupitia mitandao ambayo inawaruhusu kushare taarifa.
Kwa sheria mpya ni kwamba hata mtu mwenye kundi la whatsapp aliyekuwa anafundisha kutengeneza vipodozi, atashindwa kuendelea kufanya hivyo hadi awe na kibali maalumu. Sijui sheria inalenga nini lakini kwa kiasi kikubwa sheria hizi zimeathiri uwezo wa vijana kujiajiri kwa kuwa mambo yaliyokuwa yanawafanya wajiajiri kwa sasa imekuwa jinai.
NB: Najua kuna mashauri ya kiuchumi yanafanyika kwa serikali mimi niwakumbushe tu kuwa tafiti zinaonyesha kuwa ukizidisha kodi, au ukitaka mapato mengi, mapato hupungua kwa kuwa watu huziepuka kodi zaidi wakiona zinazidi kuwabana (Montiel, 2008).
Sasa kwa kuwa watu wataepuka kodi hizo na kupunguza mapato ya serikali, tutazidi kuwapeleka watu jela au kuendelea kufanya majadiliano na DPP ili kulipa fedha ambazo haziko mikononi mwa watu. Kwa mwendo huo basi aidha shughuli haramu ziongezeke, au unemployment iongezeke kwa kasi.
Matokeo ya ugumu kiuchumi yana impact mbaya kisiasa, sheria huwa haifanyi kazi raia wanapoona wamechoka.
Haya ni maneno yangu kwa serikali yangu tukufu ili waweze kujua kuwa vijana hawataweza kujiajiri kama sheria inawabana kwa kiasi kikubwa namna hii, na ikiwa ajira zilizopo haizendani na idadi ya watu waliopo.
Ninayo mengi ila kwa leo niishie hapo.
Signed
OEDIPUS
References
Goodman, M. (2015). Future Crimes. New York: Doubleday.
Montiel, P.-R. A. (2008). Development Macroeconomics. Princeton: Princeton University Press.
O’Connor, D. E. (2005). The Basics of Economics. London: GREENWOOD PRESS.