Hali ya kutokewa na mizimu inadhihirisha wazi kuwa kuna maisha baada ya kifo

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,156
Reaction score
10,974
Let say somebody you know interiorly has fallen into the bad land (Being burried), baada ya mazishi na maziko, huna hili wala lile umechil, hujavuta bangi, hujanywa pombe, huna stress za ziada ukitoa maziko, unashangaa mwanga huoooo, unaskia sauti "Shiuuuuu", kuangaza kwa umakini huyoooooo!

Anakutokea akiwa amevaa mavazi meupe peee aina ya kaunda suti ama kanzu, ama yale ya kinaijeria akiwa anakulilia na kukwambia "fulani ndiye aliyepelekea kifo changu" au "kuna 1m ipo ndani, chini ya debe la unga wa mtama, kachukue ukafanyie maisha". Au kuna ile situation ya mnasafirisha maiti kuipeleka usukumani, gari linagoma kuwaka, ila mkielekezea njia ya kwenda Sinza linawaka

Kupitia hili still hamuamini kuwa kuna maisha baada ya kifo? Japo sijawahi kutokewa na mzimu but huwa nasikia kwa watu tu ukiachia mbali bongo movie!

Naombeni kuwasilisha hoja
 
Hamna Mizimu Bali ni majini yanayochukua Sura za wapendwa wetu wanapokufa ili yajimilikishe Familia fulani au ukoo fulani ili yaanze kuabudiwa ni kweli katika Familia zisizo mjua YESU KRISTO zimekua zikiabudu kitu kinachoitwa mizimu wakati ni majini
 
Inadhihirisha kuna majini na mapepo na ni viumbe vinavyoweza kuvaa sura za watu na kukurudia. Sio muhusika halisi
 
Hujawahi tokewa na mizimu sababu Haipo. Hujawahi shuhudia uchawi sababu haupo. Zote huwa ni hearsay stories za watu wajinga.
 
Hakunaga mizimu wala majini.

Hivi kwa nini watu mnakuwa waongo sana, wewe ulishawahi kuyaona majini wapi?, au limzimu.
Uso kwa uso nilikutana na jitu refu mti wa mnazi mfupi.
Ilikuwa 2004 saa 5 usiku baada ya mvua kubwa kukatika.
Mijitu hii nadhani si watu wa kawaida.
Niliukadiria urefu wake zaidi ya mita 40 kwendq juu.
Tusipuuze.
 
Hamna Mizimu Bali ni majini yanayochukua Sura za wapendwa wetu wanapokufa ili yajimilikishe Familia fulani au ukoo fulani ili yaanze kuabudiwa ni kweli katika Familia zisizo mjua YESU KRISTO zimekua zikiabudu kitu kinachoitwa mizimu wakati ni majini
Uliwahi kusikia mtu ameacha maelekezo Kisha yanakiukwa. Mwenyewe anawatokea na kusema Yale aliyoyaelekeza?

Unafahamu watakatifu na nguvu zao?

Kama hujui basi penda pia kujifunza. Sio Kila roho inayozungumza nawe ni pepo. Maana ulokole umefanya Kila kitu ni pepo chafu, uzee pepo chafu, malaria pepo chafu, n.k
 
Uso kwa uso nilikutana na jitu refu mti wa mnazi mfupi.
Ilikuwa 2004 saa 5 usiku baada ya mvua kubwa kukatika.
Mijitu hii nadhani si watu wa kawaida.
Niliukadiria urefu wake zaidi ya mita 40 kwendq juu.
Tusipuuze.
Mbona hayo majitu marefu yapo tu kila siku tunayaona hadi maonyesho ya ngoma za kisukuma?

Una umri gani kwanza? Nisije nikakuhukumu bure kumbe shida ni umri.
 
Ukikuwa utajua ulikuwa hujui (shika hii kauli)
Mimi nina miaka 45, Wewe una umri gani?

Unajua tofauti ya mazingaombwe na mauzauza?

Unajua imani za kishirikina hasa huku Afrika zinasababishwa na nini?

Kama unaweza kusoma soma kitabu cha Padre Yohannes, kinaitwa hakuna binadamu mchawi bali shetani, au kama unajua kiingereza, tafuta kitabu cha Profesa John Mbiti, African Religions and philosophy, unaweza kupata mwanga kidogo..
 
Uso kwa uso nilikutana na jitu refu mti wa mnazi mfupi.
Ilikuwa 2004 saa 5 usiku baada ya mvua kubwa kukatika.
Mijitu hii nadhani si watu wa kawaida.
Niliukadiria urefu wake zaidi ya mita 40 kwendq juu.
Tusipuuze.
Brain ina trick nyingi na unavyofanya kazi kiasi kikubwa binadamu hatujui, unachoona wewe sio sawa anachoona mwingine ingawaje wote mnaangalia kitu kimoja
 
Let say somebody you know interiorly has fallen into the bad land (Being burried), baada ya mazishi na maziko, huna hili wala lile umechil, hujavuta bangi, hujanywa pombe, huna stress za ziada ukitoa maziko, unashangaa mwanga huoooo, unaskia sauti "Shiuuuuu", kuangaza kwa umakini huyoooooo!

Anakutokea akiwa amevaa mavazi meupe peee aina ya kaunda suti ama kanzu, ama yale ya kinaijeria akiwa anakulilia na kukwambia "fulani ndiye aliyepelekea kifo changu" au "kuna 1m ipo ndani, chini ya debe la unga wa mtama, kachukue ukafanyie maisha". Au kuna ile situation ya mnasafirisha maiti kuipeleka usukumani, gari linagoma kuwaka, ila mkielekezea njia ya kwenda Sinza linawaka

Kupitia hili still hamuamini kuwa kuna maisha baada ya kifo? Japo sijawahi kutokewa na mzimu but huwa nasikia kwa watu tu ukiachia mbali bongo movie!

Naombeni kuwasilisha hoja
Vibwengo hivyo
 
Unamaanisha ngongoti?
Kwa sasa nina 67
Pole sana.

Huo umri wewe mzee. Kama umeshazeeka ukiamini ushirikina, hakuna mtu anaweza kukuelekeza tofauti.

Ninasikitika sana maana utaenda kuondoka duniani ukiamini vitu ambavyo havipo, pole sana.
 
Back
Top Bottom