Hali ya kwenye media (TV) ni tete

Hali ya kwenye media (TV) ni tete

Okay..kwahiyo media zinazocheza WCB contents ndo zinazoongoza kwa revenues?

Content ni muziki na umbea tu?..Kwahiyo ITV ikae siku nzima kumuongelea mama dangote?
Media nazo zimelala walichokua wanakifanya 1990s ndio hichohicho wanafanya na kutegemea wapate faida ileile ya miaka hiyo bila kujali mabadiliko ya soko kiuchumi, kijamii, Teknolojia n.k

Wajiongeze buana
 
Taarifa zote zinaanzia JF, hao wenye local TVs wanafanya marejeo tu bila cha ziada.... local channels ni utopolo mtupu.
 
Nilikuwa jana na jamaa mmoja ambaye ni mtangazaji wa kituo kikubwa cha TV bongo ananimbia hali ya kifedha ya media nyingi haswa Tv ni tete,hapo sisemei magazeti ukiondoa yale ya michezo maana yana afadhali.

Anasema afadhali radio bado sponsors wako wengi haswa vipindi vya michezo na vile vyenye contents za uswahilini kama uhondo au leo tena.

Sababu kubwa ni mvuto wa tv kupungua kutokana na social media na kubanwa vitu vya kuandika na kusema haswa vya kisiasa,pia michezo haswa mpira wa miguu imekuwa na nguvu sana kwa hiyo vipindi vya michezo bado havikosi sponsors haswa vya redio maana gharama za kutangaza ni ndogo kuliko tv na wengi wanasikiliza.
Na bado !
 
Media zijikite kwenye habari za umbea
Mf-huyu kamfumania yule,esma kasema kile
Etc na habari waweke ukurasa wa mbele kama tv iwe habari ya kwanza

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Wananchi zaidi ya 84% wanaipenda na kuielewa serikali yao, na wanatamani kupata vitu vinavyowajenga kama mipango ya serikali inavyoelekeza
Kwa hiyo ondoa shaka, hapawezi kuwa ugomvi wa taabu kwa serikali wala umma wa watanzania
Wananchi wamemuacha rais wao asiwe wa kwanza ,akapitwa na Nana.
 
Kipindi cha ufisadi nchi ilichangamka kila kona, bungeni, Ikulu, Uraiani na kwenye Media
 
Nani ataangalia tv ambazo zimebanwa na kuishia kusifu na kumuabudu mtu mmoja?
Nani mwenye akili timamu atafungua channel ten ili kumtizama Humphrey Polepole?
 
Social networks siku hizi ndio kila kitu.
Wamiliki wa tv wafanye utafiti na kuwaletea watanzania vitu ambavyo wanavihitaji kwa sasa
Social networks hazizuiliki lakini pia hazijakuwa threat kwao ila tatizo dunia amebadilika wao wamelala
 
Wamiliki wa tv wafanye utafiti na kuwaletea watanzania vitu ambavyo wanavihitaji kwa sasa
Social networks hazizuiliki lakini pia hazijakuwa threat kwao ila tatizo dunia amebadilika wao wamelala
Hilo ni kweli TV zimekosa ubunifu,wabuni vipindi vitakavyo wafanya watu watizame TV.
 
Back
Top Bottom