ORCA ACE
JF-Expert Member
- Jan 18, 2020
- 1,449
- 1,708
Sio ivyo tu, tumejawa na hofu kubwa, watu wanapotea, watu wanatekwa, watu wanaokotwa baharini wakiwa wameuwawa, watu kupigwa risasi, tunaogopa ata kutumia simu zetu kwan tunakuwa monitored, ni hofu hofu hofu, kweli kuichagua ccm ni kosa kubwa kwan unyama uaendelea tu dhidi yetu
Sasa ni dhahiri kuwa hali ya maisha Tanzania inakatisha tamaa. Ni ngumu mno kiwango cha juu kinachokera na kuumiza.
Pamoja na ulofa mtu aliokuwa nao lakini tangu aamke asubuhi mpaka jioni atakuwa amefuatwa na watu wasiopungua 5 waliomfuata wakiomba mkopo huku yeye mwenyewe pia akiwa katika msako wa mkopo.
Yaani kila mmoja anamfikiria mwenzake labda ana unafuu fulani, kumbe siyo.
Wote tupo kwenye msoto mkali. Miaka 5 ya utawala huu imetufikisha hapa! Sasa wanakuja tena kuomba kura eti wamenunua ndege!
Tuna JAMBO LETU 28/10/2020.