BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,767
- 288,340
RUSHWA TUNAILEA
RUSHWA INATULEA
Hali ya rushwa katika chaguzi zetu inatisha kuliko wakati wowote. Jitihada za kupambana nayo zinalingana na ongezeko la rushwa yenyewe, yaani vita imeongeza rushwa badala ya kuipunguza. Hii ni kwa vyama vyote na wagombea wote. Tofauti ni viwango tu. Kwa hiyo ni sahihi kusema tunailea rushwa na rushwa inatulea maana ndiyo inatupatia watawala.
Kitendawili cha rushwa katika uchaguzi ni hiki. Kwamba, wasiohonga hawakubaliki na wanaohonga ndio wanakubalika. Hii maana yake ni kuwa wapiga kura ndilo tatizo kuliko wagombea.
Lakini je, walioshinda kura za maoni walihonga? Je walioshindwa hawakuhonga? Je kuna waliohonga na hawakushinda? Je kuna ambao hawakuhonga na wameshinda?
Kwa nini rushwa katika chaguzi imeongezeka awamu hii kuliko chaguzi zilizopita? Nimesikia sababu zifuatazo:
1. Mfumo unaowapendelea wabunge na madiwani walio madarakani kuendelea na kampeini kwa kisingizio cha kuteleza ahadi na ilani wakati watia nia wageni wakizuiwa.
2. Utitiri wa vyombo vingi vya kushughulikia rushwa ya chaguzi. Hii imevifanya vyombo hivyo kulazimika kujihusisha na siasa na kuchafuliwa na rushwa hizo.
3. Mgongano wa viongozi wa juu wa vyama kuhusu tatizo la rushwa. Wapo wanaoichukia kwa dhati na wapo wanaoichukia kwa kauli tu.
4. Kuruhusu rushwa zinazonufaisha vyama ni kulea rushwa inayonufaisha wagombea.
5. Kukosekana kwa usawa mbele ya sheria (double standard). Uwepo wa kundi teule lisilofungwa na sheria kwa vitendo na kauli wakati wengine wakibanwa na sheria.
6. Kubanwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na msimamo wa serikali na vyombo vya dola kupuuza mitandao ya kijamii.
7. Msimamo hasi dhidi ya demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa kujieleza. Hili linaongeza msongamano wa wagombea katika sehemu moja. Nafasi chache zinagombewa na watu wengi sana. Mwenye dau kubwa ndiye anaonekana.
8. Viongozi wakuu wa vyama kuwa na wagombea wao mifukoni.
9. Matumizi mabaya ya vyombo vya dola. Maeneo mengine ndio mawakala wa kugawa rushwa kwa sababu hawawezi kukamatwa.
10. Uwezeshaji wa mitandao ya simu katika kugawa rushwa. Wagombea wengi walikuwa na namba za siri maalum kwa kugawa rushwa. Kwenye bajeti za wagombea, hata vyombo vimo.
Zinahitajika jitihada za pamoja, za wazi, na zenye nia njema kupambana na rushwa. Takukuru peke yake hawawezi maana wamefungwa mikono na ni sehemu ya mfumo. Chama tawala peke yake hakiwezi kwa sababu kinapata uongozi kupitia mfumo huo huo. Vyama mbadala haviwezi kwa sababu havina ridhaa na vinaikosa kwa sababu ya rushwa.
Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza