Hali ya sarafu yetu yazidi kuimarika, pongezi kwa serikali ya Magufuli

Hali ya sarafu yetu yazidi kuimarika, pongezi kwa serikali ya Magufuli

Anaingia madarakani 2015 rate ya dola ilikua 2,160/=!

Nashangaa hiyo 2,315/= mnasema kasaidia nchi nashindwa kuwaelewa!

Rate imepanda kwa shilingi 155/= nzima!

Acheni umama nyie vichaa!View attachment 1058007

Haya ndio mambo yale yale anayofanya kila siku.

Tengeneza tatizo wewe mwenyewe halafu jifanye unalitatua,halafu kula utukufu wote.

Hili swala kalijenga mwenyewe baada ya kuharibu Bureau De Changes zote,bei zikapanda sasa anajifanya kurekebisha na it will not quietly come back to normal..Not at all!

Tunamjua Jiwe!

Anavuruga kwa makusudi kabisa halafu anajifanya kurekebisha with no success!

Nonsense hizi!
Ni kweli wakati JPM anaingia 2015 aliikuta usd 1 = TSh 2160, lakini aliikuta ikiwa inaporomoka kwa kasi
2014-2015.png

Hivyo japokua imeendelea kuporomoka lakini jitihada kubwa zimefanyika kupunguza kasi ya huo mporomoko, na hapo majuzi watu walipojaribu kuihujumu shilingi serikali imechukua hatua za haraka kuhakikisha hali inatengamaa!
 
A
Ni kweli ila hebu aache uwanja sawa wa kufanya siasa bhana!
Binge live amezima ila yeye kila uchwao ata km anaapisha balozi mmoja LiVE!
Hajiamini sijui kwanini!
Ana chuki kubwa na Wakaskazi sijui walimkosea nini na Chadema hata ikiwa mahtuti bado inamtisha sana.
 
Ni kweli wakati JPM anaingia 2015 aliikuta usd 1 = TSh 2160, lakini aliikuta ikiwa inaporomoka kwa kasi
View attachment 1058042
Hivyo japokua imeendelea kuporomoka lakini jitihada kubwa zimefanyika kupunguza kasi ya huo mporomoko, na hapo majuzi watu walipojaribu kuihujumu shilingi serikali imechukua hatua za haraka kuhakikisha hali inatengamaa!

Acha stori miingi!

Kaikuta 2,160/=!

Kutoka hapo leo mwaka wa nne,imekua mbaya zaidi!

Sasa sijui unasema vitu gani ndugu yangu?

Jukumu lake tangu ameingia ofisini day 1 ni kazi yake kuhakikisha haipandi zaidi ya 2,160/= tena sana sana ishuke!

Ndio kazi yake tuliyompa!Sasa wewe unasema ilikua inaporomoka na wakati ameingia ofisini?

Utetezi mwingine unafanya uonekane kituko kabisa!
 
Mi naona wanaoharibu zaidi ni Benki zetu, bei wanayouza ni kubwa sana ukilinganisha na wanayonunua, hii ni tofauti kabisa na nchi nyingine, utakuta kwa dola moja wanapata faida ya zaidi ya sh. 100

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwenye upande wa euro ndo hatari kabisa. The difference is 300Tshs per euro. Binafsi naona kama ni upuzi flani ivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom