Losambo
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 2,611
- 868
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
Mdondoaji acha ujinga, rais kwa kauli yake mwenyewe alisema kuwa watumishi wote wa serikali walipwe mishahara kabla ya tarehe 25 ya kila mwezi sijui kama hilo unalikumbuka.
Sasa sijui wakati rais alipotoa kauli hiyo alikuwa out mind? Yote kwa yote nina marafiki zangu waliopo TPDF, TPF,TPS wote mpaka sasa wamekiri kutokupokea mshahara wa mwezi November!!
Nilipododosa zaidi wakasema wanasubiri hundi kutoka hazina ili wapeleke bank.
Hiyo siyo dalili nzuri kwa serikali kuchelewesha mishahara ya watumishi wake.
Swali la msingi kwa nini serikali icheleweshe mishahara ya watumishi wake, inapata faida gani zaidi ya kujinukisha kuwa imefilisika?
Kama kweli serikali inapinga tetesi za kuwa dhoofu kiuchumi haina haja ya kupinga kwa maneno bali kwa vitendo cha kwanza na umuhimu kwa ustawi wa afya yake ni kuwahisha mishahara ya watumishi wake.