Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

Hali ya serikali ni tete? Mpaka sasa mishahara kitendawili

Lakini mbona jeshini hakuna upuuzi wa kucheleweshewa mishahara?. Sijui polisi na magereza lakini JWTZ hakuna upuuzi huo kabisa.

Jeshini ni usalama wa Taifa. Usipowalipa wale unahatarisha usalama wa Taifa. Ila wale wasiokuwa na umuhimu wa kuwalinda watawala watangojea pesa ipatikane.
 
Mwezi uliopita walichukua pesa toka TCRA, hawakuwa na namna! Mwezi huu haitawezekana kwa kuwa wakichukua tena TCRA wameonywa kuwa wataiuwa taasisi hiyo, labda wataelekea NSSF au GEPF.

Ambaye atanibishia kuhusu hili la serikali kukopa TCRA na kufilisika naye atakuwa amefilisika kimawazo

Dah! Kikwete Rais bora kuliko waliomtangulia lakini anashindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wa Serikali!!!! Hali inatisha.
 
Nawashangaa sana mnaobisha juu ya serikali hii kutokuwa na mipango madhubuti.Hebu chukulia mfano huu, wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa wanatakiwa kulipwa allowance ya asilimia 25 ya mshahara wake kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.Ajabu ni kwamba hivi sasa tunalipwa asilimia 9 tu ya mshahara wetu.Kila tukidai hilo wanajibu serikali haina fedha.Mwezi huu Novemba allowance hiyo kiduchu imelipwa tarehe 23.Sasa hatujuia mshahara utalipwa lini maana hadi leo hii hakuna kitu kilinachosomeka.Na ukondoo wa wafanyakazi wengi ambao unatokana na kutokuwa na elimu inayostahili ndani ya TMA ndiyo inayofanya wawe wa kusema ndiyo kwa kuogopa kuondolewa kazini.
Ndugu zangu serikali hii ya sasa ni matatizo matupu.Unahitaji kuwa na ujasiri wa namna yake kuitetea mbele ya watu.
 
Hebu chukulia mfano huu, wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa wanatakiwa kulipwa allowance ya asilimia 25 ya mshahara wake kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.

kumbe wenzetu mambo safi,mbona walimu,manesi,waganga hawana allowance?
 
mwezi huu ni deshi tuwe wavumilivu, tusije tukavunja amani ya nchi yetu. poleni sana wafanyakazi
 
wanajf salaam!
hivi ni kweli kwamba hali ya serikali ni tete kiasi cha kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi mpaka sasa?
nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wa umma,nimepata salary slip yapata 4 days now ila hundi ya mshahara haijapelekwa bank,nimemuuliza mhusika w kwa hapa ofisini kwetu anasema serikali haijaleta pesa wao wametoa slip in advance tu.

mwezi uliopita kuna mjumbe wa jf alitoa mada hii mimi sikutilia maanani kwa kuwa mwezi ulopita sisi tulipata mishahara mapema ila sasa nadhani ndio zamu yetu....

duuu napata hofu na muelekeo wa serikali yetu.au ndo ule msemo kuwa 'nchi imeshauzwa?'

nawasilisha.
wewe mleta hii mada utakuwa na mental retaditioon kwa vyovyote vile iwavyo. Leo ni tarehe ngapi?
 
Mwezi uliopita walichukua pesa toka TCRA, hawakuwa na namna! Mwezi huu haitawezekana kwa kuwa wakichukua tena TCRA wameonywa kuwa wataiuwa taasisi hiyo, labda wataelekea NSSF au GEPF.

Ambaye atanibishia kuhusu hili la serikali kukopa TCRA na kufilisika naye atakuwa amefilisika kimawazo

Mungu baba nitaishije mimi? hali ni mbaya sana kwa sasa hadi mishahara ni kitendawili?
 
mwezi huu ni deshi tuwe wavumilivu, tusije tukavunja amani ya nchi yetu. poleni sana wafanyakazi

Tuwe wavumilivu? you must be joking.... tusije tukavunja amani? amani ipi? hivi suala la kutopewa haki yako ya mshahara ambayo unaitegemea kwa 100% for food and everything unasema ni amani? how can we survive?
 
wewe mleta hii mada utakuwa na mental retaditioon kwa vyovyote vile iwavyo. Leo ni tarehe ngapi?
mkuu sijakuelewa,inawezekana wewe ndo una mental retardation.jicheck vizuri
 
...muda huu mke wangu ambaye ni mtumishi wa umma amenpigia simu yuko benki,ameniambia ktk mshahara wake amekuta tsh 100,000 zimekatwa bila kuharifiwa...
 
wanajf salaam!
hivi ni kweli kwamba hali ya serikali ni tete kiasi cha kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi mpaka sasa?
nikiwa miongoni mwa wafanyakazi wa umma,nimepata salary slip yapata 4 days now ila hundi ya mshahara haijapelekwa bank,nimemuuliza mhusika w kwa hapa ofisini kwetu anasema serikali haijaleta pesa wao wametoa slip in advance tu.

mwezi uliopita kuna mjumbe wa jf alitoa mada hii mimi sikutilia maanani kwa kuwa mwezi ulopita sisi tulipata mishahara mapema ila sasa nadhani ndio zamu yetu....

duuu napata hofu na muelekeo wa serikali yetu.au ndo ule msemo kuwa 'nchi imeshauzwa?'

nawasilisha.

sem 2708,

Hivi wewe mpaka sasa huelewi hali ya kiuchumi na utendaji wa serikali yako????
Napenda kunukuu maneno ya mwalimu.''SERIKALI CORRUPT HAIKUSANYI KODI,ITABAKI NI KUFUKUZANA NA WAFANYI BIASHARA WADOGO WADOGO TU''. Huu ni kweli na tunauona kwenye majiji mengi;Dar,Arusha,Mwanza,Mbeya n.k. Polisi ni kufukuzana na Wamachinga tu na kuwapiga mabomu ilhali hakuna KODI INAYOKUSANYWA NA SERIKALI HAINA PESA. Hii ni aibu.

Ajabu ni pale UNAPOSIKIA POSHO ZA WABUNGE ZIMEONGEZWA KINYEMELA TOKA SH.70,000/= MPAKA SH.200,000/=Kwa walala hoi pesa hakuna lakini kwa WABUNGE NA WAJUMBE WA CC na NEC pesa ipoooo!!Watu wakiambiwa CCM ni ya KUPIGA CHINI hawasikii wala hawaelewi. Kazi ni kwenu!!!

Hiyo ndiyo CCM bwana Chama Cha Mafisadi na Majambazi!

Hilo ni fundisho kwetu Watanzania. Next time tutajifunza zaidi kuwa IKULU si sehemu ya kukimbilia. Kwa hali ilivyo hebu angalia mfumko wa bei na kupanda kwa gharama kwa ujumla bila kusahau kufilisika KWA SERIKALI bado muda kidogo tu serikali itatangaza mfilisi. Kitendo cha serikali kukopa kwenye taasisi zake pamoja na sekta binafsi ki cha aibu. Maana Tanzania tunakila kitu. Cha ajabu tumewekeza kwenye kutorosha twiga, madini na raslimali zingine za nchi huku serikali ikiendelea kuwalinda wahalifu. Siku si nyingi na sisi tutaishia kabisa uwezo wa kukopa na kuwa Greece ya Bongo.
Mliimchagua wenyewe huyo JK last year, subirini mnae huyo hadi 2015. Mtavuna mlichopanda
 
kwa nini kusiwe na tarehe moja na consistency ktk kulipa mishahara?Mara watu walipwe tar. 25,27,30,2, why?????
 
Sasa nimekupata vyema. Uko sahihi lakini naomba nikujuze kitu fulani kuwa hao askari viongozi wao wengi hawana shida kabisa kwa sababu ya marupurupu na ufisadi wanaoufanya.
Kazi yao ni kukilinda chama tawala kwa gharama yoyoye ile!!!!! Askari walio chini wengi ni form 4 hivyo hata vimshahara wanavyopewa wanaona vinakidhi haja lakini wanashindwa kujiuliza kwa nini hawalipwi stahiki zao kwa wakati, mathalani mtu akihama,likizo n.k
Majuzi nilikuwa nasikia Nahodha Shamsi Vwai akisema serikali imelipa 14bill madeni ya Polisi na Magereza ambayi ni mwaka 2007-2009 June. Kwa hiyo ina maana mpaka sasa serikali bado inadaiwa madeni ya 2009 July - 2011 na bado wanaichekea serikali kwa kupiga wananchi na kuzuia maandamano kila kukicha halafu wananchi hao hao ndiyo wanaorudia kwa kuwaomba rushwa na kuwabambikia makosa ya uongo!!!
Inasikitisha sana, naomba siku wakose kabisa mishahara ili viti visikalike huko maofisini.

Wala usiombe polisi na wanajeshi kukosa kabisa mishahara maana taabu na mateso itakuwa kwa wananchi raia. Tutakamatwa barabarani kwa visingizio vya kukiuka sheria za barabara n.k! Watashirikiana na majambazi kutuvamia ili wapate chochote! Serikali isifanye mchezo na mishahara ya watumishi however meagre the salaries may be.
 
Kuna tetesi nimesikia wahadhiri wa vyuo vikuu kama UDSM, Sokoine, IFM, UDOM, manesi na madaktari hawajalipwa mishahara yao hadi leo. Inawezekana kweli serikali imekwama kwani jamaa wanalipwa mshahara mapema sana kushinda taasisi zenginezo ila leo nimesikia hawajalipwa hadi leo.
 
Hebu rekebisha usemi wako, hiyo si tetesi. Itabidi miaka minne iliyobaki Ikulu/serikali itabidi itafute mwekezaji wa kuiendesha.
 
Hebu rekebisha usemi wako, hiyo si tetesi. Itabidi miaka minne iliyobaki Ikulu/serikali itabidi itafute mwekezaji wa kuiendesha.
Kuna jamaa yupo serikalini amenitisha kishenzi, anadai hata wao waliopo NMB hawajapata mishahara ilihali huwa wanapata kabla ya tarehe25 na baada ya siku mbili tatu walio katika mabenki mengine nao hupata. hii inamaana kwamba watu NMB wakipata hata kesho basi walio mabenki mengine watapata zaidi ya tarehe2 mwezi ujao. Sikutegemea kama ipo siku serikali itachoka kiasi hiki kuna watu walio karibu na wahusika wanadai umechukuliwa mkopo lakini kuna makosa ya kiufundi mkopo haujafika kwa wakati.
 
wewe mleta hii mada utakuwa na mental retaditioon kwa vyovyote vile iwavyo. Leo ni tarehe ngapi?

Na leo ni tarehe ngapi?? Utauliza hivyo mpaka tarehe 10 December..................?? Mambo ni mabaya kubali au kataa!!! Watu wanaofanya kazi serikalini wanalijua hili na wanalisema waziwazi. Nyie wajasilia mali mnaopata contract za mizengwe kupitia CCM ndiyo mpo hapa kutetea!! Subirini cheque zitakapoanza kubounce!!
 
Back
Top Bottom