Jean chill
Member
- Apr 8, 2011
- 69
- 20
Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
Ni kweli bandugu kuna jamaa moja ambia mimi salary slip iko pelekwa kwa benki tangia alhamisi lakini napata benki haiko na kitu hata kwa masaa haya..alafu hii jamaa ingine ambia sisi mshahara tarehe 30 kwani kama jana napata 24 alafu leo napata 30 kweli hyo ni mwezi moja au napata mwezi na masiku 6?sasa serekari nalipa sisi kwa masiku 30 ama masiku 36?mimi iko naona bantu leo balipwa baada kwa masiku over 30 days
Nawashangaa sana mnaobisha juu ya serikali hii kutokuwa na mipango madhubuti.Hebu chukulia mfano huu, wafanyakazi wa mamlaka ya hali ya hewa wanatakiwa kulipwa allowance ya asilimia 25 ya mshahara wake kila ifikapo tarehe 15 ya kila mwezi.Ajabu ni kwamba hivi sasa tunalipwa asilimia 9 tu ya mshahara wetu.Kila tukidai hilo wanajibu serikali haina fedha.Mwezi huu Novemba allowance hiyo kiduchu imelipwa tarehe 23.Sasa hatujuia mshahara utalipwa lini maana hadi leo hii hakuna kitu kilinachosomeka.Na ukondoo wa wafanyakazi wengi ambao unatokana na kutokuwa na elimu inayostahili ndani ya TMA ndiyo inayofanya wawe wa kusema ndiyo kwa kuogopa kuondolewa kazini.
Ndugu zangu serikali hii ya sasa ni matatizo matupu.Unahitaji kuwa na ujasiri wa namna yake kuitetea mbele ya watu.
Usibishie kitu usichokijua weye, sometimez uwe unakaa kimya. Serikali ina madeni kibao, hata pesa za kulipia mishahara wafanyakazi haina, imejaa mikopo tu. Madenti wanapolia kwamba hawana mikopo toka HESLB sio kwamba wanatania, serikali imefulia. Sie wazabuni hatujalipwa hadi leo, na wewe unakuja kutuongezea hasira.Fanyeni kazi acheni kupiga umbeya mwisho wa mwezi bado tayari mshaanza kulalama hela ya mwisho wa mwezi. Je mngelikuwa mnafanya kazi katika kampuni binafsi ambapo mshahara hutoka tarehe 30 si mngelia nyie vp!!!!
Mkuu, kama unadhani indicator ya serikali kufilisika si kucheleweshewa mishahara watumishi wa umma basi kwako ni kigezo gani? Tatizo hapa si fluctuation ya mishahara, bali hoja ya kufilisika inachagizwa na serikali kukopa fedha TCRA, Stanbic, CRDB na kwingineko ili kulipa mishahara. Kama kweli hivyo ndivyo, those are indicators of a collapsing govt financially, which may lead to bankrupcy. Hoja ni kwanini serikali ikope kwa ajili ya kulipa mishahara?