Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
HALI YA SIASA ILIKUWAJE TANGANYIKA WAKATI INAUNDWA TANU NA HALI YA SIASA ILIKUWAJE TANZANIA WAKATI INAASISIWA CCM?
Sikujua kama CCM iliasisiwa jana tarehe 5 Februari, 1977 hadi niliposoma kwenye gazeti leo asubuhi. Sijui iweje siku muhimu kama hii inipite. Kusahau huku kukanikumbusha Siku Kuu ya Saba Saba siku TANU ilipoasisiwa Dar es Salaam tarehe 7 Julai, 1954. Hakuna nyumba Dar es Salaam ambayo haikuhusika na TANU kwa njia moja au nyingine hadi uhuru wa Tanganyika ulipotikana tarehe 9 Julai 1961. Chini ya kila paa la nyumba za Kariakoo na kwengineko ipo historia ya TANU.
Naukumbuka mtaa wa New Street ilipokuwapo ofisi ya TANU, Mtaa huu ndiyo sasa unajulikana kama Lumumba Avenue. Nikiwa kijana mdogo nikipita sana mtaa huu kwenda Tuwa Tugawe kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuangalia mpira wa club za mitaa ya Dar es Salaam ya 1960s. Nikiukumbuka uwanja huu wa mpira namkumbuka na Mwalimu Tumu kocha wa New Style moja ya timu kali za mitaani akiwa na ‘’megaphone,’’ ya kienyeji iliyotengenezwa kwa mabati akimuhimiza mshambuliaji wake hodari Kazi afanye nini apate kufunga goli.
Barabara ilikuwa moja nyembamba na pande zote mbili kulikuwa na nyumba zilizoezekwa kwa madebe au makuti. Kwenya kona ya New Street na Kariako ndipo ilipokuwa ofisi ya TANU. Chama cha TANU kiliasisiwa katika hali ya umasikini sana na ofisi yake haikuwa ofisi ya hadhi. Ofisi ya TANU haikuwa na umeme na chumba kimoja alipangishwa Muhindi akifanya shughuli za udobi akifua ngua na kupiga pasi.
Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeandika historia ya TANU siku ilipoasisiwa na yale yalipitika.
Tujikumbeshe:
‘’Joto la siasa lilikuwa katika kiwango cha juu sana wakati wajumbe kumi na saba wa TAA kutoka kwenye matawi majimboni na makao makuu walipokutana mjini Dar es Salaam tarehe 7 Julai, 1954, kujadili katiba mpya ya chama kipya cha siasa - TANU. Jimbo la Mashariki ambalo lilikuwa na wajumbe wengi kushinda yote liliwakilishwa na, ndugu wawili Abulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia, Julius Nyerere na C. O. Milinga; Jimbo la Kaskazini liliwakilishwa na na Joseph Kimalando na Japhet Kirilo; Jimbo la Ziwa liliwakilishwa na Abubakar Kilanga, L. M. Makaranga. Katika wanachama kumi na saba waasisi, tisa kati yao walitoka makao makuu, watano kutoka Jimbo la Ziwa, mmoja kutoka Jimbo la Magharibi na wawili kutoka Jimbo la Kaskazini. Uwakilishi huu wa wajumbe kutoka kwenye majimbo na makao makuu unatoa picha ya hali ya harakati za siasa nchini Tanganyika kabla ya kuundwa kwa TANU.
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TAA ulikuwa na ajenda ndefu. Siku ya kwanza mkutano ulichukua saa matano na nusu. Siku hiyo ilitumiwa kuondoa matatizo yaliyokuwa yakikiathiri chama. Ajenda ya kwanza ya mkutano huo ilikuwa idhinisha kufukuzwa kazi kwa Alexander Tobias aliyekuwa Katibu Mtendaji tangu Juni, 1953. Tobias alikuwa amepoteza majalada na nyaraka muhimu sana za chama zilizokuwa chini ya mamlaka yake kama Katibu Mtendaji.
Kulikuwa na tetesi kwamba majalada hayo aliyakabidhi kwa Special Branch baada ya kupewa fedha. Ilikuwa katika siku ya pili ndipo wajumbe walikaa chini kuanza kazi hasa ya kujadili ya kuigeuza TAA na kukifanya chama cha siasa TANU bila ya kuficha madhumuni yake na kutangaza dhamiri ya chama ya kuwatayarisha Waafrika wa Tanganyika kujitawala. Julius Kambarage Nyerere, mwanasiasa mgeni katika TAA pale makao makuu akiwa amejiunga na uongozi wa chama miezi kumi na tano tu iliyopita, alichaguliwa rais wa kwanza wa TANU na John Rupia makamo wa rais.
Ajenda ya kwanza kujadiliwa chini ya TANU tarehe 9 Julai ilikuwa lile suala la uchaguzi wa wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria. Katika mwaka 1950 itakumbukwa kuwa TAA, chini ya uongozi wa Abdulwahid na Dr Kyaruzi iliwakilisha memorandum kwa Gavana Twining kueleza mapendekezo yake juu ya mabadiliko ya katiba. Ilishauriwa kwamba ili kufikia kiwango fulani cha maendeleo ya siasa, ilikuwa lazima Waafrika wapitie utaratibu wa maendeleo hatua kwa hatua kwa kushiriki katika kuitawala nchi yao. Moja ya mapendekezo ilikuwa Waafrika waruhusiwe kuchagua wawakilishi wao wenyewe katika Baraza la Kutunga Sheria.
Ilikisiwa kwamba haya mabadiliko ya hatua kwa hatua yaruhusiwe kuendelea kwa kipindi cha miaka kumi na tatu baada ya hapo Waafrika waruhusiwe kuunda serikali yao wenyewe iliyo huru.Hii ilikuwa ajenda muhimu sana na Abdulwahid na Rupia ambao walikuwa wajumbe wa kamati ndogo ya siasa ya TAA iliyorasimu mapendekezo hayo walieleza mkutano kwa ufupi juu ya upinzani wa serikali katika kukubali mapendekezo hayo. Ilikubaliwa na wote kwa pamoja kuwa suala la kuanzisha kanuni za kidemokrasia katika uchaguzi wa wajumbe kwenye Baraza la Kutunga Sheria lilikuwa muhimu sana na watu lazima wafahamishwe juu ya haki hii.
Ajenda ya mwisho kujadiliwa ilikuwa nafasi ya Malkia juu ya Waafrika wa Tanganyika na mgogoro wa ardhi ya Wameru. Itakumbukwa kuwa mwaka wa 1951 Ally Sykes, akiwa katibu wa TAGSA, alitoa maneno makali dhidi ya serikali ya Uingereza kama mtawala wa Tanganyika. Ally Sykes aliiandikia barua serikali ya kikoloni na kuiomba ijitoe katika utawala wa Tanganyika. Mkutano ulisisitiza kuwa Waafrika wa Tanganyika hawakuwa raia wa Uingereza na kwa hiyo Malkia hakuwa na mamlaka juu yao. TANU ilieleza kuwa iilimtambua Malkia kama kiongozi wa serikali ya kikoloni iliyoonogozwa na Gavana Edward Twining.
Kwa mantiki hiyo basi TANU ilidai bendera ya UNO ipandishwe sawasawa na bendera ya Uingereza ili kuonyesha kuwa mamlaka hizo zote mbili kwa pamoja ndizo zilikuwa zikitawala Tanganyika chini ya udhamini. Serikali ya kikoloni haikutaka kukubali kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya mamlaka mbili. Mwisho wa mkutano Japhet Kirilo alieleza kuhusu mgogoro wa ardhi kule Meru na TANU iliitaka serikali ya kikoloni ama irejeshe ardhi hiyo kwa wenyewe au ilipe fidia.’’
Kuna anaekumbuka hali ya siasa Tanzania mwaka wa 1977 wakati CCM inaundwa?