Hali ya uchafu wa Mazingira Manispaa ya Moshi Kilimanjaro

Hali ya uchafu wa Mazingira Manispaa ya Moshi Kilimanjaro

Hii ndiyo Moshi tuliyoijua miaka 2007
Huyo kiongoozi aliyesema ni wajibu wa wananchi kumkumbusha mtendaji wa mtaa, alitakiwa ang'olewe kwenye hiyo nafasi pamoja na huyo mtendaji wake, ina maana Dr na nurse nao wakumbushwe na wagonjwa, Mwalimu akumbushwe na wanafunzi, hao kama wanalipwa mishahara kwa kusubiri kukumbushwa basi nchi imeshaoza
 
Uongozi wa Moshi Manispaa, ni mbovu, ni uongozi wa kujirusha kwenye media,kumbe utendaji haupo!
 
Mkurugenzi aliyeko ,mikoa aliyozaliwa haihangaiki na usafi.
Kuna watu wametoka mikoa isiyojali usafi.
 
Nimeishi Moshi mpaka 2012, kulikuwa Ku Safi Sana, na ilinijenga mpaka sasa hivi siwezi kudondosha hata Ganda la pipi chini.
Nini kimetokea?
 
Hii ndiyo Moshi tuliyoijua miaka 2007
Huyo kiongoozi aliyesema ni wajibu wa wananchi kumkumbusha mtendaji wa mtaa, alitakiwa ang'olewe kwenye hiyo nafasi pamoja na huyo mtendaji wake, ina maana Dr na nurse nao wakumbushwe na wagonjwa, Mwalimu akumbushwe na wanafunzi, hao kama wanalipwa mishahara kwa kusubiri kukumbushwa basi nchi imeshaoza
kweli mkuu. ameongea kisiasa
 
Ndugu abiria sasa tunaingia moshi tafadhali zingatia sana usafi usitupe wala kutupa takataka hovyo kwani ni kosa kisheria na unaweza kutozwa faini au kifungo

Asante sana kwa kutuchagua ***********
Ni sauti ambayo mpaka leo haijawahi nitoka kutokea kwa mhudumu wa basi
 
Baraza la madiwani, Meya na Mkurugenzi wa mji mjitafakari.
Moshi ilikuwa ndiyo kioo cha usafi wa miji yetu leo ni aibu tupu.
 
Back
Top Bottom