Dollar ya marekani au pesa za kigeni haitegemei kushuka kwa miaka mitatu ya ijayo labda mbeleni.
Kwanza hatujitoshelezi kuzalisha wenyewe kwa matumizi yetu ya hapa ndani,hivyo tunanunua bidhaa za fedha nyingi kuliko tunazo uza nje.
Pili Tumetegemea zaidi misaada kutoka nje kuliko mikopo nafuu ya maendeleo kwa sababu hatuna sifa ya kukopeshwa na mtoa msaada yawezekana isilenge kule tunakotaka.
Tatu wawekezaji wa uhakika ambao wangeweza wakaelekeza miradi mikubwa ya maendeleo nchini mara zote wametupiga kisogo sababu ya sera zetu zinazobadirika kama kinyonga labda kama hawana jinsi.
Nne,ni serikali kupanga matumizi makubwa huku mapato yake yakiwa chini,hivyo serikali ufyatua noti nyingi kuliko thamani halisi,ndio mfumuko wa bei na kwa namna hiyo dollar itapaa tuu.
Tano Ukosefu wa uzazi wa mpango,yawezekana watanzania si wavivu wa kutisha lakini mtu mmoja anabeba mzigo mkubwa,kwa hali hii kwa ujumla wake nchi haisongi.