Hali ya uchumi je dolla itakuja kupanda au kushuka kwa miaka kumi ijayo

Hali ya uchumi je dolla itakuja kupanda au kushuka kwa miaka kumi ijayo

High Vampire

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2012
Posts
2,915
Reaction score
2,134
hebu wataalamu wa uchumi waje watusaidie je dola itazidi kupanda au itashuka nataka kusevu baadae nije kuuza
 
hebu wataalamu wa uchumi waje watusaidie je dola itazidi kupanda au itashuka nataka kusevu baadae nije kuuza
Dola inaweza shuka baada ya miaka miwili au mitatu ijayo hii ni kutokana na sera zilizopo za kuimalisha uchumi wa ndani, i'm stand to be corrected
 
Kabla yakueleza kipi kitatokea hapo mbeleni unapaswa kwanza kufahamu ni kwanini shilingi yetu kwa sasa imepoteza thamani dhidi ya dolar.

Kuimarika kwa dolar yenyewe ni chanzo cha sasa kinachopelekea shilingi yetu kuonekana inapoteza thamani.

Cha pili ni Tanzania kukosa vyanzo vyakutosha vya mapato ya fedha za kigeni(dolar) kwani kwa sasa tunategemea zaidi Utalii na madini.Kumbuka tunaagiza bidhaa nyingi nje na tunahitaji dolar kwa manunuzi,inapokuwa haba basi thani yake hupanda(The law of demand and supply)

Cha tatu uhitaji mkubwa wa dolar hasa kutokana na bidhaa nyingi tunategeme kuagiza nje hasa kutokana na sisi kukosa viwanda.
Hapa rudi kwenye The law of demand and supply ie kama dolar ikiwa chache wakati inahitajika kwa wingi itagombaniwa na itapanda thamani.

Sera mbovu zakiuchumi,mfano mpaka sasa bado kuna biashara zinafanyika kwa dolar ndani ya nchi eg kuna nyumba zinapangishwa kwa dolar maeneo kama mbezi beach hii huendelea kuongeza uhitaji wa dola ndani ya nchi.Ilitakiwa kupigwa marufuku kufanya biashara kwakutumia us dolar ndani ya nchi.

Je kwa mikakati ya sasa shilingi yetu itaimarika hapo mbeleni?

Tukifanikiwa kwenye viwanda shilingi yetu lazima itaimarika kwani tutakua na akiba yakutosha ya fedha zakigeni kutokana na mataifa mengine kututegemea sisi kununua bidhaa zetu za ndani kutoka viwandani.Wanapokuja nchini itawalazimu kuja na dolar wakifika wana change na kuacha dolar wanachukua tsh ili kufanya manunuzi.

Lakini pia mahitaji ya dola ndani ya nchi yatapungua kutokana na kupunguza kuagiza bidhaa nje ya nchi kwani bidhaa nyingi tutakua tunazalisha wenyewe.
 
Kuanguka au kuimarika kwa dolla itategemea na sera za Tanzania kuunusuru au kuudidimiza uchumi wake na muelekeo wa uchumi wa dunia.
Tanzania inaweza ikawa na sera nzuri sana ila kudorora kwa uchumi wa dunia ukaharibu kila kitu.
Kwahiyo hii mambo haina formula maalumu.
 
Dollar ya marekani au pesa za kigeni haitegemei kushuka kwa miaka mitatu ya ijayo labda mbeleni.
Kwanza hatujitoshelezi kuzalisha wenyewe kwa matumizi yetu ya hapa ndani,hivyo tunanunua bidhaa za fedha nyingi kuliko tunazo uza nje.
Pili Tumetegemea zaidi misaada kutoka nje kuliko mikopo nafuu ya maendeleo kwa sababu hatuna sifa ya kukopeshwa na mtoa msaada yawezekana isilenge kule tunakotaka.
Tatu wawekezaji wa uhakika ambao wangeweza wakaelekeza miradi mikubwa ya maendeleo nchini mara zote wametupiga kisogo sababu ya sera zetu zinazobadirika kama kinyonga labda kama hawana jinsi.
Nne,ni serikali kupanga matumizi makubwa huku mapato yake yakiwa chini,hivyo serikali ufyatua noti nyingi kuliko thamani halisi,ndio mfumuko wa bei na kwa namna hiyo dollar itapaa tuu.
Tano Ukosefu wa uzazi wa mpango,yawezekana watanzania si wavivu wa kutisha lakini mtu mmoja anabeba mzigo mkubwa,kwa hali hii kwa ujumla wake nchi haisongi.
 
hebu wataalamu wa uchumi waje watusaidie je dola itazidi kupanda au itashuka nataka kusevu baadae nije kuuza
dola dhidi ya tsh.
kuanzia '85 mpaka '10 dola inapanda dhidi ya tsh hamna kitakacho badilisha ndani ya miaka tano ujayo
 
Back
Top Bottom