Hali ya Uchumi na kupanda kwa bei, Waziri Kijaji asema Bei za bidhaa za ndani ni himilivu. Waziri Mwigulu aahidi kupunguza bei mafuta ya kula na gari

Inawezekana hatujayumba kama wenzetu lakini hatuwezi kusema hatujayumba kabisa. Ukweli ni kwamba mfumuko wa bei ni kuonyesha hata sisi tumeyumba. Dunia imekuwa moja

 
Bure kabisa vitu vimepanda wapo wanakula tozo kila sehemu tunakatwa. Hawana shida yeyote watoto wao wako nchi za nje.

Nimejua kwa nini jpm alitakiwa atoweke.
Ccm ni walewale
Hata jpm hakuwa na msaada wowote zaidi ya kufokafoka tu
Jpm alipandisha bei za bidhaa wakati dunia ilikuwa tulivu
Sukari kutoka 1500 hadi 3500 over night
 
Samia ameishaambiwa mapungufu ya huyu waziri wake wa fedha lakini Katia Pamba maskioni . Hapa mnacheza na uhai wa watu na familia zao . Mishahara haipandi na kipato kimepungua lakini bei za mahitaji muhimu zimepanda hivyo kuumiza wananchi!!
Viongozi hamuwezi kuelewa machungu wanayopata wananchi kwasababu kipato chenu kikubwa!!
Haiwezekani na sio busara mawaziri kila siku kuimba tu sababu za kuwa na mfumuko wa bei, wananchi wanataka kuona hatua zinachukuliea zitakazopunguza makali ya mfumuko wa bei!
Njia moja serikali inaweza kusaidia ni kwa kuahilisha miradi isiyokuwa na kipaumbele kwa wakati huu. Serikali isimamishe ununuzi wa zile ndege za ATCL iilizoagiza kwani hivi sasa hali ya uchumi ni tete; nina hakika hao mlikoagiza hizo ndege watawaelewa. Punguzeni pia matumizi ya serikali ya siyo ya lazima kama hizi safari za maV8 kuja Dar. Toka Dodoma kila leo!!

Wananchi wanataka kuona hatua mathubuyu zinachukuliwa kuwapunguzia maumivu na sio kila leo vita ya Putin ndio kisingizio!

Mnataka waandamane ndio mtajua wanaumia?
 
Hii ni aibu kubwa, hivi tuna ardhi ya kutosha tunashindwaje kuzalisha ngano mpaka tunaagiza tani laki nane zote?

Ngano, mbolea, mchele, sukari, mafuta ya kula, hivi kwa serikali makini vyote vinazalishwa hapa hapa TZ kwa kuwa- support wakulima na kuwa na , vipaumbele, sera zenye lengo la kukuza sekta ya kilimo.

Sioni vipaumbele na sera, sahihi, nia ya dhati kuwasaidia na kuwainua wakulima na TZ kujitosheleza kwa chakula na kupunguza imported inflation.

Wao wanafanya kinyume kabisa mfano ni kuondoa ruzuku kwenye mbolea na kuanzisha tozo, kodi lukuki kwa mpigo katikati ya janga la corona. Kama kulikuwa na ulazima kodi zingewezwa kuingizwa taratibu ndani ya miaka mitano wakati uchumi unaimarika.

Wakati mwingine unahisi nia yao ya dhati ni kuwakwamisha na kuwafukurisha wakulima na nchi iwe tegemezi kwa mazao ya chakula au simply they have no ideas how to run a country. Basic, common sense stuffs.
 
 
NI ZAIDI YA AIBU. NATAMANI WANGESHAURIWA HAYA WANGEONGEA WAWILI SIKU YA BONANZA ! NAHISI HATA ALIYEPELEKA VIMEMO VYA HAWA JAMAA WAWILI KUWA MAWAZIRI MUDA HUU KQJIFICHA TOILET
 
Hawa wachumi wa kudesa ni tatizo
Yaani ana thubutu kusema ati viwanda vya mafuta vina zalisha tani laki moja plus, lakini mahitaji ni laki sita plus. Halafu mna zuia mafuta kutoka nje ati mna linda viwanda. Haya ni mawazo ya utopolo..
 
Yaani Mwigulu tangu alivyookotwa kwenye vitundu vya pale LUMUMBA huwa namlinganisha na kindege kimoja kinaitwa JONJO ,Kumbuka alivyo tetea viroba vile vya mto Ruvu eti wale ni wahamiaji haramu,ndo leo anasema eti bei ya vitu ni himilivu haya ni mashairi,ya mpunbavu.
 
Duh, kweli tuna safari ndefu.
Kuna baadhi ya bidhaa mfano za nafaka, karanga, unga, mafuta ya kula, ambazo zinalimwa/ kuzalishwa hapahapa nchini ;lakini bei yake inazidi kupanda kila kukicha.
Ni kweli sababu ziko nyingi. Ila hii isiwe kichaka cha kuficha udhaifu wa kudhibiti mfumuko wa bei kwa serikali ya awamu iliyopo sasa.

Nakumbuka baada ya utawala wa hayati Mkapa, alipoingia JK madarakani, vitu vingi vilipanda bei na kuanzia hapo havikuwahi kushuka. Thamani ya shilingi ilishuka kwa kiwango kikubwa. Serikali itafute mbinu za kuongeza thamani ya shilingi
 
Plan ya serikali kunusuru inflation ni ipi?
 
Mmekula fedha za misaada ya COVID-19 mkadanganya ooh ujenzi wa shule
Kweli zilikuwa kwa ajili hiyo?
 
Huko kwenye stationeries nako sababu ni uviko na vita?
 
Sahivi kila mtu anajipandishia bei tu...utasikia nauli imeongezeka kiasi fulani..

Mamlaka zilizopo hata kupima kiwango cha upandaji bei hakuna..

Huyu mama alitukosea sana kusema kila kitu kitapanda bei
 
Hawa mawaziri wanatuona sie majuha sana,wajieleza kama vile wapo peponi wakila raha,Nchi imewashinda wanabakia kuwa MAZUMARIDI TUUUU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…