Mama Samia Suluhu Hassan,atapotoshwa na Waheshimiwa mawaziri.
-Dr Kijaji anatoa takwimu za mahitaji ya bidhaa kwa mwaka ukilinganisha na uzalishaji wa ndani,na kuonyesha deficit.
Lakini haji na mikakati ya muda mfupi,muda wa Kati na muda mrefu kumaliza changamoto hiyo
-Dr Kijaji ana lalamika tu, kuhusu wafanya Biashara kupandisha bei ya bidhaa,bila kusema FCC wanafanya nini kuzuia changamoto hiyo.wakati anazo Mamlaka za udhibiti
-Dr Mwigulu anahimiza Wananchi waendelee na kazi iwe covid-19 au vita ya Russia na Ukraine, suala la kujiuliza ni kama watanzania waliacha uzalishaji kutokana na Covid-19 au vita ya Russia?
Ushauri
1)Waheshimiwa mawazi walipaswa kueleza mipango ya Serikali ya muda wa mfupi,muda wa Kati na muda mrefu.
-Kwa mfano :
-kwa kipindi Cha muda mfupi Serikali itapunguza matumizi yasiyo ya lazima na fedha zitakazopatikana kutoa ruzuku kwa waagiza wa mafuta,au
-Serikali kuhamisha fedha kutoka kwenye mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kutoa ruzuku kwa waagizaji wa mafuta.
2). Serikali kuanzisha block farming na kutoa mikopo kwa vijana, security iwe vyeti vyao
3). Serikali kutafuta wawekezaji kwenye sekta ya gasi,kupanua viwanda vya Mbolea nondo na saruji ili kuondoa deficit
4). Serikali kupunguza VAT na Levy inayotozwa kwenye petrol
5) Serikali kukabidhi mashamba makubwa ya Busutu kwa wawekezaji binafsi au kununua Combine harvestor kukodisha kwa vijana wahitimu wetu wa SUA na vyuo vikuu vingine,ambao watawekwa kwenye CAMPs ili kuleta uzalishaji mkubwa
6) Serikali kutafuta masoko ya mazao
7).Kuanzisha viwanda vidogo vidogo au vya kati kwa ajili ya kuchakata mazao na Wabia