Hali ya umeme yawa ya matumaini baada ya juhudi za Serikali pamoja na mvua kuanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini

Huku kwetu umeme sio tatizo
 
Lucas ungeongeza na sifa za ziada za kukamilika kwa ujenzi wa daraja la kisasa lililopo Mbuchi na Mbwera - Kibiti lililojengwa kwa gharama za TZS 7.2Bn serikali hii sikivu na makini!
Katika miradi yote inavyotekelezwa na serikali yetu hakuna mtu yeyote atakayebakia salama ikiwa itabainika kuwa kafuja fedha za umma
 
Mjomba kinachofuata kwako ni kuliwa kiboga tu sasa,sio kwa usifiaji huu.

Una habari hapa nilipo mimi sasa hv umeme umekatika tokea asubuhi?

Hopeless kabisa
Inawezekana ikawa Ni kweli imekatika lakini Hali kwa Sasa Ni ya Matumaini Sana ukilinganisha na awali ,Kama niliko huku umeme haujakatika hovyo ndani ya wiki lots hili
 
Yaani watu wengine jamani au umetumwa??
 
Mgao wa makusudi. Walikuwa wanauza majenereta na sola zao zilizokwama enzi ya mwamba.

Alisema siku akiondoka mgao wa umeme utarejea. Na ikawa kweli.

Magufuli, kifo chako kinatuua na tuliobaki. Mungu akupendelee huko uliko.
Mgao wa umeme uliotokana na ukame mkubwa ambao kila mwenye macho aliushuhudia katika eneo lake na siyo kwamba ulitengenezwa na mtu yeyote Yule .serikali ya Rais Samia haiwezi ikakubali kwa namna yoyote Ile kumuumiza mwananchi kwa Faida ya watu wachache na kuangamiza na kuathiri maisha ya mamillioni ya watanzania
 
Ukame hadi kwenye gesi?
 
Niliko Mimi Hali ya Umeme imeanza kurejea na kuwa ya Matumaini ,mfano kuanzia ijumaa umeme upo muda wote na hata hapa napoandika umeme upo na tunajiandaa kwenda kuangalia mpira baadaye
Wapi ulipo wewe? Mfano Mikoa hii ya nyanda za juu kusini kuna mgao mpaka kero maeneo kama Mbalizi,Songwe,Tunduma huko sio mgao tena bali umeme unakatika hovyo hovyo

Ifakara,Iringa,Makambako nk huko ndio Kuna mgao leo upo kesho aupo Mkoa ambao nimeiona umeme upo karibu siku zote ni Dodoma tu na Ile Mikoa inayotumia umeme wa Genereta kama Rukwa,Katavi nk

Sasa wewe unasema umeme umeanza kulejea katika hali ya kawaida upo Mkoa gani au unaishi sehemu gani?

Tusifie panastahili na tukosoe panapohitajika
 
Aliekwambia tatizo la umeme ni ukame Nani?

Mbona bado umeme unazimika masaaa 12
Mvua ndio zinaanza kunyesha katika maeneo mengi na ndio maana Hali unaanza kuwa njema,.Tatizo litakwisha kabisa mvua zikikolea vizuri na kujaza mabwawa yetu ya kuzalisha umeme,Tuwe na Subira na kuiamini serikali yetu
 
H
Hapana sijatumwa Ila nimesukumwa na Hali nayoiona ya upatikanaji wa umeme mitaani kwetu kwa Sasa ambayo Ni y kuridhisha sana
Yaani wewe jana umeme 12 kamaili aupo mpaka saa 5:40 ndiyo unarudi halafu unaongea nini! Embu acha hizo kama ni uchawa punguza unakoelekea utakua kunguni kabisa.
 
Mimi nipo Mkoa wa Songwe wilaya moja wapo ambapo nakuhakikishia kuwa umeme katika wiki lots haujasumbua hata kidogo hata napoandika umeme upo
 
Mvua ndio zinaanza kunyesha katika maeneo mengi na ndio maana Hali unaanza kuwa njema,.Tatizo litakwisha kabisa mvua zikikolea vizuri na kujaza mabwawa yetu ya kuzalisha umeme,Tuwe na Subira na kuiamini serikali yetu

Uwa nakwambia ww ni chawa ambae hauna details

Unafanya uchawa na kusifia bila kuwa na details za unachokisifia

Shida ya umeme sio ya ukame

Hata mvua inyeshe kama ya elnino bado mgao utakuwepo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…