Hali ya umeme yawa ya matumaini baada ya juhudi za Serikali pamoja na mvua kuanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini

Mvua isiponyesha ni matatizo ya ukame
ila ikinyesha ni juhudi za serikali
 
Katika miradi yote inavyotekelezwa na serikali yetu hakuna mtu yeyote atakayebakia salama ikiwa itabainika kuwa kafuja fedha za umma
Lile daraja la 7b kibiti linafanana na thamani ya fedha? Hatua gani zinachukuliwa?

Mmeishia kuwatumbua waliokuwa watumishi katika serikali ya magufuli ili muweke watu wenu waendeleze upigaji.

Kuna uozo mkubwa sana kwenye miradi ya serikali. Hakuna hatua zinazochukuliwa. Unatuambia nini?
 
Mvua isiponyesha ni matatizo ya ukame
ila ikinyesha ni juhudi za serikali
Juhudi za Serikali zimeonekana kipindi chote Cha ukame kilichotokea hapa nchini,Kama siyo juhudi za serikali hali ingekuwa mbaya zaidi kwa jinsi ukame ilivyokuwa mkubwa mwaka huu
 
Hakuna Atakaye pona ikiwa atabainika kugusa pesa za umma.Tuwe na Imani na serikali yetu
 
Hakuna Atakaye pona ikiwa atabainika kugusa pesa za umma.Tuwe na Imani na serikali yetu
Nimeelewa wewe ni nani.
Lakini iko siku mtakufa tu kama ambavyo watanzania tunakufa kwa stress za ugumu wa maisha na kukosa huduma katika taasisi za serikali.

Shule za serikali elimu imeporonoka mbaya. Ukienda private ada zimepaa mbaya mwaka huu.

Maji ni shida na umeme sisemi.

Mko kwenye kiyoyozi mnasema eti kila kitu kiko sawa.
 
Nani kakutuma wewe. Umeona hali imetengemaa au umetumwa? Kipindi hiki kuacha kuumia shughuli zetu hata kombe la dunia watu wameshindwa kufustilia kwa uzuri
 
Mimi Ni mkulima na nimeona juhudi za serikali katika kutukwamua kiuchumi watanzania,Tumeona namna serikali ilivyojengwa miradi mimgi inayogusa maisha yetu,Tumeona namna uliyoleta mapinduzi makubwa katika secta karibu zote,mfano katika Afya Tumeona namna vituo vya Afya vilivyojengwa nchini kwote mfano majuzi hapa kumejengwa vituo vya Afya 234 ,lakini pia madarasa zaidi ya elfu nane nchini yamejengwa.

Ukienda katika kilimo nako Ni mapinduzi makubwa ambapo bajeti tu imeongezeka na kufikia billioni Mia Tisa na point na kutolewa kwa Ruzuku ya mabillioni ya pesa karibu billion Mia moja hamsini na kupelekea kushuka kwa Bei ya mbolea sokoni mfano mbolea ya DAP msimu uliopita ilikuwa inauzwa shillingi laki moja na 40 lakini msimu huu inapatikana kwa Elfu 70 tu
 
Nani kakutuma wewe. Umeona hali imetengemaa au umetumwa? Kipindi hiki kuacha kuumia shughuli zetu hata kombe la dunia watu wameshindwa kufustilia kwa uzuri
Inawezekana ulikoko lakini niliko Hali imekuwa njema Sana katika suala Zima la umeme
 
Umeshiba keki ya taifa. Andika tu baba. Andika hadi usinzie kwa raha zako.
 
DAP sh 70, 000 wapi?

Hivi mmetuona watanzania hatunazo kiasi hicho?

Kama kweli mmeshusha bei ya mbolea basi ondoeni kodi kwenye miamala na umeme.

Yaani tunanunua mbolea kwa bei ileile halafu mnasema imepungua bei.
 
Mimi nipo Mkoa wa Songwe wilaya moja wapo ambapo nakuhakikishia kuwa umeme katika wiki lots haujasumbua hata kidogo hata napoandika umeme upo
Mkoa wa Songwe Wilaya ipi umeme sio wa mgao labda Ileje maana sijafika huko lakini hapa Tunduma hapa sio mgao ni kero maana umeme unakatika hovyo hovyo Kyela,Rujewa, Chunya,Ubaruku kote mgao mkali
Labda upo Saza kwenye migodi huko sijui hali ikoje lakini Mikoa ninayotembelea kote nakutana na mgao mkali

Tena ningependa kukwambia huko Mkoa wa Songwe,Rukwa,Katavi huko mvua zinanyesha vizuri lakini Mkoa wa Iringa na Dodoma mvua bado ya kusuasua

Kwa hiyo mpaka sasa akuna sehemu yoyote yenye unafuu wa mgao kote kuna mgao mkali wala asikudanganye mtu ndugu yangu
 
Tukiwa na vichwa kama vyako maendeleo yatabaki kuwa ndoto
Uko kwako ndio unaona uo umeme au ngoma
Mbona suala la umeme tulikwisha sahau ila limerudi Tena? Tena kwa kasi ya ajabu? Unasifia Nini tatizo wanaleta wanajidai kutatua?
Tuwe serious na maisha asee
 
Nakukaribisha Mbozi ambako hata muda huu umeme upo na wiki lote hili umeme haujasumbua,niambie Ni sehemu gani kwa Sasa ndani ya wilaya ya Mbozi ambako umeme u asumbua iwe Ni Rwanda mahenje mlowo Vwawa au hata ihanda.
 
Tatizo la umeme halikuletwa na mtu maana sote ni.mashahidi wa namna mwaka huu ukame ulivyo kuwa nchini kwetu
 
DAP sh 70, 000 wapi?

Hivi mmetuona watanzania hatunazo kiasi hicho?

Kama kweli mmeshusha bei ya mbolea basi ondoeni kodi kwenye miamala na umeme.

Yaani tunanunua mbolea kwa bei ileile halafu mnasema imepungua bei.
Mbolea zote za Ruzuku kwa mbolea aina ya DAP no shilingi elfu 70 katika maduka yote yenye kuuza mbolea za Ruzuku ukienda na sms yako ambayo uliletewa baada ya zoezi lile la awali la usajili unapewa mbolea bila shida
 
Mbolea zote za Ruzuku kwa mbolea aina ya DAP no shilingi elfu 70 katika maduka yote yenye kuuza mbolea za Ruzuku ukienda na sms yako ambayo uliletewa baada ya zoezi lile la awali la usajili unapewa mbolea bila shida
Hiyo ruzuku umetoa wewe au ni kodi yangu?
 
Hiyo ruzuku umetoa wewe au ni kodi yangu?
Sasa hapa tunabishana Nini mkuu? Wewe si ulikuwa unapinga kuwa mbolea ya DAP ya Ruzuku haiuzwi kwa elfu 70? Mimi nimekupa utaratibu ambao wakulima tulikuwa tunaufuata kuipata mbolea hiyo na nimegundua wewe hata kilimo huelewi kikoje na mambo yapoje katika secta hii,ndio maana unakuwa mbishi bila sababu ilimradi tu uonekane umepinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…