Hali ya umeme yawa ya matumaini baada ya juhudi za Serikali pamoja na mvua kuanza kunyesha maeneo mbalimbali nchini

Mgao umekuwa mkali zaidi kuliko hapo mwanzo wakati mvua hazijaanza kunyesha...

Sasa hv mpaka saa sita usiku na ni mara mbili au tatu kwa wiki...
Uwe na subira Hali itakuwa njema Kama ilivyo huku niliko maana saiz mvua zimeshaanza kunyesha kwa wingi Sana katika maeneo mbalimbali nchini
 
Unaandika nini wew wakati nipo mkoa wa mwanza mgao upo kama kawaida ukipata umeme usiku mchana hauna, sasa kuimarika kuko wapi
 
Hali ya umeme imerejea wapi wewe kenge maji?Wacha uchawa
 
Mananga kama wewe ndiyo ma-think tank ya CCM. Aibu kubwa. Kazi ya serikali na viongozi wake unadhani ni kununua mashangingi na kupeana Phd za mchongo? Ni vioongozi wajinga kabisa ndiyo watakajitetea kwa ujinga kama huu. Kodi wanayochuwa ni ya nini? Kipindi cha uhuru walikuwa wanakusanya kodi kubwa kama sasa? Nchi inajaza wabunge wa mchongo bungeni fedha za kupanua miundo mbinu zitatoka wapi?
 
Utafi....... wewe
 
Acha utoto dogo, mvua sio jitihada za serikali, bali ni kudra za mwenyezi Mungu. Hata hayo maji mnayosema yamepatikana kwa 100% hapa mjini sio kweli. Yanapatikana bado kwa shida hata kama mgao umepungua, lakini ni huduma isiyoridhisha.
Mkuu huyu Lucas ana shida kwenye kufikiri, hivyo hata usipohangaika naye
 
Tengeneza tatizo alafu ujeuliulitatuwe unavyojuwa ww.ni njia laisi ya kumuibia mtu kilais
 
Wewe upo wapi? Unaishi Zanzibar? Naambiwa huko Zanzibar hakuna mgso.

Huku Tanganyika, hakuna mabadiliko yoyote. Mgao wa umeme ni mkali kabisa. Siku hizi 4 za mwisho, nilikuwa Singida, Tabora, Shinyanga, Geita na Mwanza. Kote ni shida tupu. Umeme unakuja saa 5 usiku, unakatwa saa 2 asubuhi.

Usiwe short sighted, kufikiria kuwa ukisifu sifu Seriksli ndiyo utapata maisha. Fanya kazi, acha uchawa wa Serikali. Musukuma anasema chawa ni mdudu anayeishi kwenye nguo chafu za ndani. Wewe unapenda kuishi huko?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…