Hali ya usafi kwenye saluni unayoenda kusuka au kunyoa ikoje?

Hali ya usafi kwenye saluni unayoenda kusuka au kunyoa ikoje?

Dah usafi ndio jambo lilifanya nitafute mtu anaejua kunyoa na kitana basi muda wowote nakua huru kunyoa mataulo hata kwenye saloon kubwa yanakung'utwa tu kufua ni baada ya kuona limechafuka sio kila baada ya mtu kutumia. Na kule walipo na usafi mzuri bai zao zimechangamka sana unakuta kunyoa ni 10k alooo hio bei noma kwangu kwahyo kuliko kuvagaa mataulo machafu bora mwanangu bondeni aninyoe nimpe ganji mambo iishe
Inasikitisha, suala la usafi inabidi liwe la kwanza katika kupata huduma hizi
 
Wakuu,

Naamini wote tunaenda saluni, iwe kusuka au kunyoa, na huduma hii sio kwa watu watu wazima pekee hata watoto pia huenda saluni kutengenezwa nywele, sasa swali ni kwamba hali ya usafi ikoje kwenye saluni unayoenda kupata huduma?

Wanaume, mataulo yanayohudumia wateja yanasafishwa baada ya muda gani? Au ni mwendo wa kukung'uta tu baada ya kumhudumia mteja halafu mwengine anatumia hilohilo? Kwenye vifaa angalau upande wa wanaume wanasafisha na spirit ama sanitaiza japo nayo sijui inaondoa wadudu/uchafu kwa kiasi gani.

Machanuo, mikasi, taulo, sindano nk, kwenye saluni za kike zinasafishwa kabla hajatumia mtu mwingine? Tukumbuke vifaa vinavyotumika vina ncha kali na ni rahisi sana kumuambukiza mtu ugonjwa.

Saluni yako vipi, usafi ni wa hali ya juu au tunamuachia Mungu?
Ni mbaya sana nimejaribu Saloon kadhaa hata zile classic swala la usafi ni duni sana.

Elimu Elimu Elimu
 
Ukweli si saluni tu. Sisi waafrika bado tupo nyuma kuhusu usafi. Ushawahi kuona sehemu za vyakula?

Haya unatoka saluni na mifangasi yako, unaingia bar kupiga supu. Kwenye supu, malimao yamekatwa vipande, yapo kwenye sahani. Unachukua kipande unafinyia kwa bakuli lako,unarudisha kwenye sahani na mifangasi yako ya saluni. Mwenzako anakuja anaendelea ulipoachia.

Unatoka hapo, unaenda kwa mchoma mahindi. Kila mtu akija anashika hindi kwanza ndiyo ajiridhishe. Kila mtu anajua alichoshika huko alipotoka. Wewe una mifangasi ya saluni na si ajabu ushakanda ngano(umekuna pumbu ) kwa kuzibinyabinya kwa miwasho. Na wewe unashikashika kila hindi, unachagua.

Kisha unamalizia kununua mchicha kwa mama mboga. Huu umeletwa ukiwa wazi kwa baiskeli, unaburuzwa kwenye spoku. Mama mboga anauweka chini juu ya kiroba ambacho huwa hakioshwi. Anaunyunyizia maji toka kopo la uhai au afya. Hakuna anaejua kopo limeoshwa lini wala maji yaliyomo yaketoka wapi. Yeye katoboa kwenye kizibo, anabinya maji yanatoka kama mkojo wa kitoto cha kiume kirijali. Mradi mchicha usinyauke.

Siku hiyo hujapitia mijuisi ya kienyeji imejazwa kwenye mibobo ya maji ya uhai.

Ukisikia waafrika hatuugui COVID kuna mengi aisee.
😂😂😂😂😂

Baada ya India nadhani Africa na Tz yetu tunaongoza kwa uchafu na uholela.

Ili uipate huduma safi inatakiwa uilipie hela nyingi sana, sasa huduma ya kawaida tu unatoboa mfuko why?
 
Tulianzaga kunyoa chini ya miembe
Mambo yalikuwa mukide

Ova
 
Wakuu,

Naamini wote tunaenda saluni, iwe kusuka au kunyoa, na huduma hii sio kwa watu watu wazima pekee hata watoto pia huenda saluni kutengenezwa nywele, sasa swali ni kwamba hali ya usafi ikoje kwenye saluni unayoenda kupata huduma?

Wanaume, mataulo yanayohudumia wateja yanasafishwa baada ya muda gani? Au ni mwendo wa kukung'uta tu baada ya kumhudumia mteja halafu mwengine anatumia hilohilo? Kwenye vifaa angalau upande wa wanaume wanasafisha na spirit ama sanitaiza japo nayo sijui inaondoa wadudu/uchafu kwa kiasi gani.

Machanuo, mikasi, taulo, sindano nk, kwenye saluni za kike zinasafishwa kabla hajatumia mtu mwingine? Tukumbuke vifaa vinavyotumika vina ncha kali na ni rahisi sana kumuambukiza mtu ugonjwa.

Saluni yako vipi, usafi ni wa hali ya juu au tunamuachia Mungu?
Aisee hili ni tatizo
Unakuta chanuo,vitana,vichafu
Taulo🙌
Balaa
 
Mm ninae mashine yangu nyumbani tunanyolea familia nzima

Uzuri sinaga mtindo wa kunyoa ni kipara tu

Na wife ndio kinyozi wangu
 
😂😂😂😂😂

Baada ya India nadhani Africa na Tz yetu tunaongoza kwa uchafu na uholela.

Ili uipate huduma safi inatakiwa uilipie hela nyingi sana, sasa huduma ya kawaida tu unatoboa mfuko why?
Yani balaa. Halafu sioni kama tutatoka leo maana hakuna anaeona kama hili ni tatizo. Tz haijalishi mtu ni msomi au la. Tabia zetu kuhusu usafi hasa kwenye huduma hizi kama za vyakula ,kunyoa n.k. zinafanana tu. Tunatofautiana kiasi tu.
 
Back
Top Bottom