Emmanuel Adam14
Member
- Jun 19, 2014
- 54
- 101
Naandika kwa mshangao, kwa masikitiko, na kwa hasira pia.
Yaani wananchi wa Dar es Salaam wanateseka kila siku na huduma ya mwendo kasi, lakini bado baadhi yao wanatetea na kuahidi kupigia kura hii serikali?
Tuambiane ukweli:
Serikali hii imeshindwa kabisa kuendesha mfumo wa usafiri wa mwendo kasi.
Mabasi ni machache, hayana ratiba, hayafiki kwa wakati.Foleni ni kama za kugombea msaada wa chakula kwenye kambi ya wakimbizi.Watu wanasimama masaa mawili wakisubiri usafiri wa mwendo "kasi" ambao haujui maana ya neno kasi.
Na bado kuna watu wanapiga makofi?
Bado kuna watu wanaahidi October tunatiki.Watu wanakimbizana na mabasi kama wanafunzi wa shule ya msingi?.
Hatuombi kila mtu awe na gari.
Tunataka tu huduma ya usafiri wa umma inayoheshimu utu wa binadamu.
Hilo nalo ni gumu?Serikali imepewa kodi, rasilimali, muda — lakini inashindwa kutoa hata huduma ya kuendesha mabasi?
Acha ushabiki wa vyama. Angalia maisha yako ya kila siku.
Je, unaishi kwa heshima?
Je, watoto wako wanapata huduma bora?
Je, unathaminiwa?
Kama majibu ni hapana — basi jibu lako liko kwenye kura.