GE2025 "Hali ya Usafiri wa Mwendo Kasi Jijini Dar es salaam: Je, Wananchi Watapiga Kura Kwa Hili?"

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Joined
Jun 19, 2014
Posts
54
Reaction score
101
Naandika kwa mshangao, kwa masikitiko, na kwa hasira pia.

Yaani wananchi wa Dar es Salaam wanateseka kila siku na huduma ya mwendo kasi, lakini bado baadhi yao wanatetea na kuahidi kupigia kura hii serikali?

Tuambiane ukweli:

Serikali hii imeshindwa kabisa kuendesha mfumo wa usafiri wa mwendo kasi.

Mabasi ni machache, hayana ratiba, hayafiki kwa wakati.Foleni ni kama za kugombea msaada wa chakula kwenye kambi ya wakimbizi.Watu wanasimama masaa mawili wakisubiri usafiri wa mwendo "kasi" ambao haujui maana ya neno kasi.

Na bado kuna watu wanapiga makofi?

Bado kuna watu wanaahidi October tunatiki.Watu wanakimbizana na mabasi kama wanafunzi wa shule ya msingi?.

Hatuombi kila mtu awe na gari.

Tunataka tu huduma ya usafiri wa umma inayoheshimu utu wa binadamu.

Hilo nalo ni gumu?Serikali imepewa kodi, rasilimali, muda — lakini inashindwa kutoa hata huduma ya kuendesha mabasi?

Acha ushabiki wa vyama. Angalia maisha yako ya kila siku.
Je, unaishi kwa heshima?
Je, watoto wako wanapata huduma bora?
Je, unathaminiwa?
Kama majibu ni hapana — basi jibu lako liko kwenye kura.
 
Kwa jiji lenye watu zaidi ya milioni sita mwendo kasi peke yake sio jawabu. Waangalie uwezekano wa kuwa na light rail kama walivyofanya Addis Ababa. Na maeneo mengine kuwe na treni za umeme za kawaida. Mabasi peke yake hayatakuja kutosha.

Aidha, Master plans ziwe realistic na ziongoze ukuaji wa jiji.

Amandla...
 
Barabara nzuri mno, mabasi ndo hakuna, yanayopita yamejaa hayasimami vituo vya katikati, ndani hewa ni nzito mno bora wafunue juu, ni kuambukizana magonjwa ya hewa na ngozi tu, joto limezidi , basi likisimama unatamani ushuke, wizi kama wote, viongozi hawapandi hivyo haiwahusu mtajijua wenyewe, sijui hii nchi ina laana gani. Hao wawekezaji waanze tu tupumue.
 
Kwamba mtu asipige kura kisa mwendo kasi? Em Leta Sababu nyingine mkuu.

Mm sijawahi na sitokaa nipige kura, ila kama ningekuwa mtu wa kupiga kura bc hii mada yako isingenifanya niache kupiga kura.

Hata USA hawajamaliza changamoto zote za wananchi wake.
 
Hii nchi hakuna mwenye mipango,sio mkuu wala wasaidizi
Wanafunzi wanateseka mno aisee,ni bora mtu mzima lakin mtoto wa shule saa mbili yuko kituoni na haruhusiwi kuingia kwenye daladala
Ni iukata na sio kutiki October
 
Njia moja ya kukabiliana na hili tatizo I kuhakikisha kuwa maeneo ya makazi yana shule "nzuri" na hivyo kuondoa ulazima wa wanafunzi kutumia vyombo vya moto kwenda shule. Aidha, itapunguza pia haja ya kuwapeleka watoto boarding.

Sio kwa hii serikali ya ccm,tutasubiri sana
Itafika mahala hawa wabunge na madiwani tutawakataa
Inawezekanaje mbunge,diwani ameweka tumbo mahala miaka 5,hakuna kitu amefanya na anakuja kuomba kura tena na anapewa,
 
Ni kutokana na mfumo wetu wa uwakilishi. Mbunge au Diwani ni muwakilishi zaidi wa chama chake kuliko wapiga kura wake. Chama chake kina uwezo wa kusitisha ubunge au udiwani wake wakati wowote kwa kumfukuza kwenye chama. Wapiga kura hawana uwezo huo. Aidha, baada ya mgombea kuteuliwa na chama chake mara nyingi wanachama na wapenzi wa chama hicho wanakuwa hawana jinsi bali kumpigia kura.
Mimi nadhani njia inayoweza kusaidia ni:
1. Kuruhusu mgombea huru. Hii itaruhusu wapiga kura wamchague mbunge wanayemtaka bila kujali chama chake.
2. Mbunge akitoka katika chama chake asipoteze ubunge. Hii itawapa ujasiri wa kubana uongozi wa vyama vyao bila kuhofia kupoteza ubunge wao.
3. Raia wapewe haki ya ku recall mbunge kama idadi ya kutosha itakuwa hairidhiki na utendaji wake. Hatari ya hii ni uwezo wa chama pinzani kulazimisha mbunge awe recalled.

Mapendekezo haya hayatakubaliwa na chama chochote maana vyote vinafaidika na system iliyopo.

Amandla...
 
Wewe unaona huduma ya usafiri wa mwendo kasi ipo sawa mkuu!?
 
Samia hajui kabisa kama Kuna shida ya kusafiri maana yeye hupita na v8 Huku akiwa amesafishiwa njia na policcm wake
 
Sio kwa hii serikali ya ccm,tutasubiri sana
Itafika mahala hawa wabunge na madiwani tutawakataa
Inawezekanaje mbunge,diwani ameweka tumbo mahala miaka 5,hakuna kitu amefanya na anakuja kuomba kura tena na anapewa,
Kwani kura wanapewa na wananchi, au tume inaagizwa kuwatangaza?
 
Ni kweli huu mwendo Kasi ilitakiwa iwe city train,kipindi wanaplani niliwahi kuongea na kiongozi mmoja wa ngazi ya juu nikamwambia tuige wenzetu akasema mwendo Kasi Iko poa,Sasa yalianza mabasi 200 Sasa hivi yanayo fanya kazi ni 60 tu,unategemea Nini Hapo
 
Noma sana
 
Mbele kwa mbele mitano Tena wenzetu wanajenga reli chini ya bahari sisi tung'ang'ana na mabasi kila goti litabigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…