KERO Hali ya vyoo NaneNane Dodoma nani anatakiwa kuwajibika? Kuna changamoto ya maji

KERO Hali ya vyoo NaneNane Dodoma nani anatakiwa kuwajibika? Kuna changamoto ya maji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

DodomaTZ

Senior Member
Joined
May 20, 2022
Posts
197
Reaction score
233
Hali ya vyoo kwenye maonesho ya Nane Nane yanayofanyika Dodoma ni changamoto, huduma ya maji ni changamoto na kuna vyoo vichache kulingana na wingi wa Watu wanaofika eneo hilo. Kwa tukio kubwa la kitaifa kama hili, ni jambo la kushangaza kuona miundombinu ya msingi kama vyoo ikipuuzwa.
photo_2025-08-07_13-05-40.jpg

photo_2025-08-07_13-05-43.jpg

photo_2025-08-07_13-05-42.jpg
Changamoto hii imeleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaotembelea maonesho haya, hasa wanawake, wazee na watoto. Wengi hulazimika kujizuia kula au kunywa kwa hofu ya kutohitaji huduma ya choo, na wengine hushindia biskuti tu ili waepuke hali hiyo.

Nikiwa sehemu ya wenye banda eneo hili nipo siku ya tatu ni shida tupu, mwaka jana ilikuwa hivi na sasa bado jambo hili limeendelea kupuuzwa kama vile halina umuhimu.

Waandaaji wa maonesho haya wangepaswa kuwa na mipango madhubuti ya huduma za vyoo na maji, hasa ikizingatiwa kuwa kila mwaka tukio hili huvutia maelfu ya watu. Kutoweka kipaumbele kwenye huduma za msingi ni sawa na kudharau afya na utu wa washiriki na wageni wa maonesho.

Ni muhimu kuhakikisha mazingira ya kibinadamu yanazingatiwa. Huduma ya choo na maji si anasa ni haki ya msingi kwa kila mshiriki.
photo_2025-08-07_13-05-44.jpg

Hali ilivyokuwa Mwaka 2024 ~ Waandaaji Nane-Nane Dodoma mliwaza nini? Tunateseka na huduma ya vyoo, ujenzi wa vibanda pia haujakamilika
 
Yani una hoji swala la maji dodoma ? Mji mkuu hauna maji uo una tegemea visima vya chumvi
 
Back
Top Bottom