KERO Responded Hali ya vyoo Ofisi ya Mabasi ya Shabiby – Dodoma sio salama kwa Watumiaji

KERO Responded Hali ya vyoo Ofisi ya Mabasi ya Shabiby – Dodoma sio salama kwa Watumiaji

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

News Tz1

Member
Joined
Nov 28, 2025
Posts
82
Reaction score
110
Kama inavyofahamika kwa wengi, kampuni nyingi za mabasi jijini Dodoma hutumia ofisi zao kama maeneo ya kusubiri usafiri au kushusha abiria. Hali hii huzifanya ofisi hizo kubeba jukumu la kuhudumia umma. Kwa mantiki hiyo, huduma muhimu kama vyoo zinapaswa kupewa kipaumbele cha juu.

Katika muktadha huo, ni mara ya pili ndani ya kipindi cha hivi karibuni kufika katika ofisi za Shabiby Dodoma (Shabiby Bus Terminal), zilizopo maeneo ya CBE, na kukuta vyoo vipo katika hali mbaya. Hali hii inaweza kusababisha tishio la kiafya kwa abiria pamoja na wananchi wengine wanaofika katika eneo hilo wakiwemo Watoto ambao nao nimeshuhudia wakiingizwa na wakubwa wao kwenda kujisaidia katika vyoo hivyo.
9cd7042f-e405-4859-a475-8db747dae32b.jpeg
Nitoe wito kwa Mamlaka za Afya Mkoa wa Dodoma kuweka utaratibu wa kufuatilia hali ya vyoo katika ofisi za umma na binafsi zinazotumika kuhudumia wananchi. Hatua hii itasaidia kubaini changamoto zilizopo, hususan katika suala la vyoo, na hivyo kusaidia kuzuia athari za kiafya kwa jamii.
25e644c3-3fc6-4286-b897-135e0450ada5.jpeg

photo_2026-01-29_09-08-44.jpg

photo_2026-01-29_09-08-50.jpg

WhatsApp Image 2026-02-20 at 17.11.23.jpeg

Maboresho ya vyoo hapo hapa ~ Uongozi wa Shabiby Bus Terminal waboresha vyoo vya Kituo cha Shabiby Bus Terminal - Dodoma
 
Ila Kuna mambo mengine ya kipumbavu sana. Mtu pesa zote hizo unashndwa kutengeneza vyoo standard kabisa visafi na kuajiri mtu maalum wa usafi kila muda ...******* sana hao jamaa ..ndio mana Mimi matajiri wachaga nawakubali sana
 
Shabiby endelea kupigilia misumali naona mafisadi yameaza kujitokeza adharani.
Upumbavu ni kudhania kua shabiby Yuko na nyinyi maskin kwamba anawasema mafisadi ...na wakati wakitoka hapo wanaenda hotel za bei mbaya ufukweni kugonga cheers na kusema tumeweza kuwachanganya Hawa vidampa. 🚮
 
Na ni kwel mim maskini Sina lolote ndo maana nipo naokotoa makopo ya maji nikapate rizkk
Pole sana. Pambana sana, kama hivyo vyoo kwa macho yako ya nyama unaona viko sawa ...aiseee pambana pambana Bado umaskin una roam around your body and mind.
 
Ila Kuna mambo mengine ya kipumbavu sana. Mtu pesa zote hizo unashndwa kutengeneza vyoo standard kabisa visafi na kuajiri mtu maalum wa usafi kila muda ...******* sana hao jamaa ..ndio mana Mimi matajiri wachaga nawakubali sana
Wafanyabiashara wengi Wabongo na hata Ofisini za umma huwa hawajali sana vyoo vizuri na visafi.
 
Upumbavu ni kudhania kua shabiby Yuko na nyinyi maskin kwamba anawasema mafisadi ...na wakati wakitoka hapo wanaenda hotel za bei mbaya ufukweni kugonga cheers na kusema tumeweza kuwachanganya Hawa vidampa. 🚮
Hayupo Nasi Yule
 
Unataka uwekewe vyoo kama vya nyumbani kwako??

Nenda ukojoe kapande gari usepe.
 
Back
Top Bottom