Hali yako ya kimaisha ya sasa unaipa methali au msemo upi?

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Kila mtu anapitia ya kwake na kwa muda wake , vitu vingi vinatukwamisha ,vingi vinatujenga vingine vinatuabisha vingine vitupa moyo na furaha.

hivi kwamba hali yako ya maisha ya sasa ungeambiwa utumie methali,Nahau au msemo wowote kuielezea ungetumia METHALI au MSEMO Upi?

kwa Upande wangu mimi hali yangu ya sasa ningetumia

MAJI UKISHAYAVULIA NGUO SHARTI UYAOGE
 
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu.

Mimi huyo niliambiwa nisijaribu jaribu kuwajua wasichana nyumba zao sio nzuri ni giza Mimi nikampinga mama sa hivi nimeenda kumpa mimba mwanamke najuta tena ni single maza kanizidi umri ni soo.
 
Mipango sio matumizi.

Wakati nilivyokuwa mdogo akili yangu ilikuwa changa nilijiuliza kwanini huyu anakuwa tajiri huyu anakuwa masikini!? Nikadhani masikini hawajitumi kumbe la hasha wanapambana na bado wanafeli maisha magumu jamani sijawahi kuona, ni kama nimekataa tamaa.
nimesali sana nimepigana sana lakini kila siku naenda chini zaidi
 
Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu
Mimi huyo niliambiwa nisijaribu jaribu kuwajua wasichana nyumba zao sio nzuri Ni Giza Mimi nikampinga mama sa hivi nimeenda kumpa mimba mwanamke najuta Tena Ni single maza kanizidi umri Ni soo
Ulimwengu unakupa shule hukumskia bi mkubwa
 
Daaah maisha yanafanya watu waabudu hata visivyoabudika

Hata ukisali mungu bado anakusubiri wakati wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…