Leo katika pitapita zangu za huko mashambani, kwakweli wakulima hawana hamu kabisa na kipindi hiki kutokana na bei za pembejeo.
Huyu huyu mkulima akinunua mbolea ya DAP kwa Tshs 105000 bado usafirishaji kuelekea huko pembezoni yaliko mashamba ambako mfuko mmoja wa mbolea unagharimu Kama 5000 mpaka 10000.
Upande wa pili wa shilingi, debe la mahindi ni Tshs 4000 mpaka 5000, yaani mtu akihudhuria kikao cha saa moja ambacho malipo ni Tshs 10000, tayari anaweza kupata debe mbili za mahindi, ambapo shughuli ya kuzalisha debe hizo mbili humchukua muda mwingi mkulima ambao huambatana na uchovu mkubwa.
Kusema kweli Kama taifa tunakoelekea siyo kuzuri, kwanini wakulima wanateseka namna hii?!!!
Yaani mkulima ni amekuwa mnyonge kwelikweli.
Mwisho, ukiongea na wakulima kumi kuhusiana na kilimo, nane watakwambia huyu mama Samia yaani ameshusha bei za mazao yetu hata hatumwelewi kabisa, Bora Magufuli alisema " Wakulima pandisheni bei za mazao yenu, asiyetaka akalime shamba lake " na alisema tutamkumbuka na kweli tumemkumbuka ndani ya muda mfupi sana.