Halima Mdee ahoji Uwanja wa CCM Kirumba kukarabatiwa kwa Fedha za Umma (Bungeni Juni 10, 2024)

Halima Mdee ahoji Uwanja wa CCM Kirumba kukarabatiwa kwa Fedha za Umma (Bungeni Juni 10, 2024)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Halima Mdee ahoji Uwanja wa CCM Kirumba kukarabatiwa kwa fedha za umma
Mbunge Halima Mdee amehoji uamuzi wa Serikali kuwa na mpango wa kuuboresha Uwanja wa CCM Kirumba kwa fedha za umma licha ya kuwa Uwanja huo unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Awali, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma (Mwana FA) alisema “Uwanja wa CCM Kirumba ni mmoja wa Viwanja vitano vilivyo kwenye mpango wa maboresho ili kukidhi viwango vya CAF, Wizara ipo katika mazungumzo na mmiliki ili kukubaliana namna ya kugharamia na kuviendesha viwanja hivyo.”

Aidha, amesema Uwanja huo utawekewa taa ili kuweza kutumika wakati wa usiku.

Pia soma
 
Back
Top Bottom