Halima Mdee ahoji Uwanja wa CCM Kirumba kukarabatiwa kwa fedha za umma
Your browser is not able to display this video.
Mbunge Halima Mdee amehoji uamuzi wa Serikali kuwa na mpango wa kuuboresha Uwanja wa CCM Kirumba kwa fedha za umma licha ya kuwa Uwanja huo unamilikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Awali, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mwinjuma (Mwana FA) alisema “Uwanja wa CCM Kirumba ni mmoja wa Viwanja vitano vilivyo kwenye mpango wa maboresho ili kukidhi viwango vya CAF, Wizara ipo katika mazungumzo na mmiliki ili kukubaliana namna ya kugharamia na kuviendesha viwanja hivyo.”
Aidha, amesema Uwanja huo utawekewa taa ili kuweza kutumika wakati wa usiku.