Halima Mdee anastahili tuzo ya heshima ya uzalendo

Halima Mdee anastahili tuzo ya heshima ya uzalendo

Katika mchakato wa kupitisha Mkataba wa Bandari, Halima Mdee alisimama kidete kutetea Maslahi ya taifa katika uwekezaji bandarini.

Halima Mdee hakusimama kama Mpinzani au mwana CHADEMAA bali kama Mzalendo, Mtetezi na Mpenda Nchi na Mlinzi wa Rasilimali za Taifa.

Mchuano ulikuwa mkali baina ya Spika na Mdee pamoja na Mdee dhidi ya wabunge wetu wa CCM. Ukiisikiliza video clips ya mchuano kizalendo, utabaini kwanba Halima Mdee ni Mzalendo na Jasiri linapokuja suala la Maslahi ya Taifa.

Kwakuwa sina Taasisi inayoweza kutoa Tuzo, napendekeza kwenu kwamba tumpe maua yake dada Mdee kwa kumzawadia Tuzo ya Heshima ya Uzalendo.

Kama Taasisi zitaogopa mkono wa serikali, basi sisi wazalendo wa Jamii Forums tutoe Tuzo hii. Ni aibu na usaliti kumuacha Halima bila tuzo katika jambo hili.

Nationalist and Patriotic Award 2023 for Hon. Halima Mdee.

Naomba kuwasilisha.
Hana lolote ilikuwa janja janja tu ya ccm ku-balance story pale bungeni ili ionekane kulikuwa na mjadala mzito kuhusu
 
Halima mdee akabidhiwe chadema Nina hakika ataifikisha mbali, mbowe kachoka Hana jipya.
 
Back
Top Bottom