Halima Mdee: Bawacha vitoto vya juzi

Halima Mdee: Bawacha vitoto vya juzi

IMG-20230516-WA0015.jpg
 
Halima ndee hutufai kabisa katika nchi hii, tunaomba ustaafu siasa wewe ni mbinafsi na wa hovyo kupita kiasi, Watanzania tumekuchukia sana toka ulivyoshikilia kidedea watanzania wasipewe ardhi
CHADEMA ni chama Cha ajabu sana wale wao wanaowaona hawafai ndio huwa vipenzi vya watanzania wapenda Siasa na mabadiriko rejea
Zitto kabwe
Dokta Slaa
Harima mdee
Esta Bulaya
 
Yeyote anayeharibu au anayehujumu haki za watanzania huyo ni adui wetu sote bila kujali chama chake cha siasa wala sauti yake kavu wala umbo au rangi
itakuwa umemaliza masomo na hujapata hata sehemu ua ku volunteer …mnakuwaga Wazalendo sana …ila mkipata kichochoro mnakuwa zaid ya Mchwa kwny rasilimali za Nchi
 
Huyo lucy owenya na grace kihwelu wamewahi kuwa wabunge wa majimbo gani?
 
..kwanini haulizwi ameingiaje bungeni?

..kikao gani cha chama kiliwapendekeza?

..Watz tuna tabia ya kuruhusu na kuvumilia mambo ya kijingajinga na kutouliza maswali ya msingi.
Wao wanajua waliingiaje . Kama ww unapinga, uende mahakamani.
 
itakuwa umemaliza masomo na hujapata hata sehemu ua ku volunteer …mnakuwaga Wazalendo sana …ila mkipata kichochoro mnakuwa zaid ya Mchwa kwny rasilimali za Nchi
Nimefanya kazi miaka 9 taasisi binafsi Tanzania, nikawa mjasiriamali knye kilimo mkubwa kwa miaka 5 , kikanishinda kwa sababu ya mifumo mibaya nikaondoka Tanzania nafanya biashara zangu nje ya nchi kwa miaka 8 sasa tena kwa ufanisi sana . Kwa hiyo nawatetea vijana waliokosa fursa na wanaoishi maisha magumu wakati wana nia na juhudi za kazi
 
CHADEMA ni chama Cha ajabu sana wale wao wanaowaona hawafai ndio huwa vipenzi watanzania wapenda Siasa na mabadiriko rejea
Zitto kabwe
Dokta Slaa
Harima mdee
Esta Bulaya
Yaani hawa kabisa hapa sioni afadhali maana wote wanasikilizia maslahi binafsi tu, Jiwe alimhonga Mdee na wenzake ubunge akawasiliti chadema wote na Watanzania waliowaunga mkono bila kuwa na aibu yeyote , halafu leo mtu anishauri eti nimsikilize
 
Kama mmiliki wa saccos kashindwa mpaka anaomba huruma ya Mama Samia hawa chawa wataweza
 
Aisee natamani hiyo 2025 ifike haraka Hawa wasaliti watupishe. Wanatia sana hasira yaani wanafanya uasi alafu wanaleta ujeuri.

Ndio maana natamani Lissu au Heche wapewe uenyekiti sidhani kama huu utumbo ungelelewa. Yaani ilitakiwa unamkamata mmoja kwa mahojiano yaani ni kipigo mpaka ataje Kila kitu na ramani nzima ilikuaje.

Haya mambo bila kuwa serious tutaendelewa kuchezewa na CCM
 
Wao wanajua waliingiaje . Kama ww unapinga, uende mahakamani.

..waandishi wa habari wanatakiwa wawaulize waliingiaje bungeni.

..waandishi wadadisi na mahiri wangekuwa wameshafanya uchunguzi na kujua nani aliwezesha Halima na wenzake kuingia bungeni.
 
Nimefanya kazi miaka 9 taasisi binafsi Tanzania, nikawa mjasiriamali knye kilimo mkubwa kwa miaka 5 , kikanishinda kwa sababu ya mifumo mibaya nikaondoka Tanzania nafanya biashara zangu nje ya nchi kwa miaka 8 sasa tena kwa ufanisi sana . Kwa hiyo nawatetea vijana waliokosa fursa na wanaoishi maisha magumu wakati wana nia na juhudi za kazi
wote humu kupitia story zenu si mnakaa Masaki na Ostybay, mna marafiki zenu Wazungu mlipokutana nao kwny biashara zenu wakashangaa urasimu wa kiserikali

kila mmoja alipiga chini kazi Serikalini akafanya mishe zake na sasa hivi mambo yake poa na ana biashara katika Nchi kadhaa za kusini mwa jangwa la Sahara

sie Wazee wa fitna tukipitia post na comments zako mbili tatu tuna uwezo wa ku draft 80% ya CV yako tukakuachia eneo la jina na tarehe ya kuzaliwa

Wewe ni 'dhoful haaali kichwani hadi mfukoni' na ndio sababu una wenge kwa vitu vidogo vidogo …
 
Niezaliwa Arusha familia ya kati, nimefanya kazi kampuni nzuri tu Tanzania nikaacha nikajitegemea knye kilimo Songea na Rukwa , sijawahi kuishi Dar ninakuja tu knye mikutano na vikao, nimeishi Morogoro, Mbeya na Rukwa na nimejenga kote huko, 2016 Magufuli alipoingia nikaondoka Tanzania nikafungua biashara zangu za utalii na logistic hapa na USA ndo wasifu wangu mdogo sana . SINA MAKUU WALA SIFAKE LIFE . NATETEA SANA WAKULIMA NINAKIPENDA NA NAONA FURSA KUBWA SANA ILA SERA MBOVU NA MIFUMO MIBAYA NDO MAANA NATETEA SANA SERA MPYA
 
Sisi CDM damu damu hatutaki Halima afukuzwe - wanaotaka afukuzwe wataondoka wao
 
Niezaliwa Arusha familia ya kati, nimefanya kazi kampuni nzuri tu Tanzania nikaacha nikajitegemea knye kilimo Songea na Rukwa , sijawahi kuishi Dar ninakuja tu knye mikutano na vikao, nimeishi Morogoro, Mbeya na Rukwa na nimejenga kote huko, 2016 Magufuli alipoingia nikaondoka Tanzania nikafungua biashara zangu za utalii na logistic hapa na USA ndo wasifu wangu mdogo sana . SINA MAKUU WALA SIFAKE LIFE . NATETEA SANA WAKULIMA NINAKIPENDA NA NAONA FURSA KUBWA SANA ILA SERA MBOVU NA MIFUMO MIBAYA NDO MAANA NATETEA SANA SERA MPYA
Wenye pesa hawajitetei sana kwanza muda huo hawana

sijui familia ya kati sijui ya Pembeni achana na hizo

comments zako humu zingetosha kabisa kujua kama mi familia ya kati au ya pembeni
 
Aisee natamani hiyo 2025 ifike haraka Hawa wasaliti watupishe. Wanatia sana hasira yaani wanafanya uasi alafu wanaleta ujeuri.

Ndio maana natamani Lissu au Heche wapewe uenyekiti sidhani kama huu utumbo ungelelewa. Yaani ilitakiwa unamkamata mmoja kwa mahojiano yaani ni kipigo mpaka ataje Kila kitu na ramani nzima ilikuaje.

Haya mambo bila kuwa serious tutaendelewa kuchezewa na CCM
...ndiyo maana tunaendelea kumlilia JPM kwa sababu wajinga wajinga kama hao alikuwa akimalizana nao kwa utaratibu kama unaoutamani.
 
Nani baina yao alianza kuwa mwana Chadema
Whatever, hana justification ya kutoa kauli zile. Ukishakuwa mtu mzima, you have already crossed the line of childhood and you need adult treatment, respect for that matter
 
"....Bawacha wengi wao pale ni vitoto vya juzi kwenye game ambavyo kwa namna vinavyopiga kelele wala sipaswi kuhangaika navyo kwa sababu natambua ngoma ya mtoto huwa kamwe haikeshi."

Mheshimiwa Halima Mdee (MB).

==========

Dar es Salaam. Wakati Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), wakiandamana kina Halima Mdee waondolewe bungeni, mbunge huyo amesema hao ni ‘watoto wa juzi na hawajui alikotoka’.

“Unajua watoto hawatakiwi kunyimwa usingizi, ndio maana siwajibu wengi wanaopiga talalila ‘kelele’ wamenikuta mjomba napiga mzigo pale (Chadema). Wametamani baada ya mzigo kutema, ukishakuwa mkubwa huwezi kuangaika na watoto, wanasema unawaacha,”amesema Mdee.

Mdee aliyewahi kuwa mwenyekiti wa Bawacha kwa nyakati tofauti ameeleza hayo leo Jumanne Mei 16, 2023 wakati akihojiwa na Wasafi TV jijini Dodoma. Katika maelezo yake, Mdee amesisitiza kuwa yeye bado ni Chadema ‘for life’.

Katibu Mkuu wa Bawacha, Catherine Ruge amemjibu kwa kusema sio sahihi kuzungumza kauli kama hizo, hata hivyo, akasema waswahili wana msemo unaosema ‘mfamaji haishi kutapa tapa.’ Ruge amedai Mdee ameonyesha dharau kwa Bawacha kusema waliondamana ni watoto.

“Katika yale maandamano kulikuwa na kina mama ambao Mdee aliwakuta katika chama, wakiwemo Mama Kimaro, Suzan Kiwanga, Grace Kiwelu na Lucy Owenya, Je wakati huo wangesema yeye mtoto hafai kuwa mbunge angejisikiaje? tunaona ni dharau,”amesema Ruge.

Mei 11, mwaka huu viongozi wa Bawacha na wanachama wengi wa Chadema walifanya maandamano yaliyoanzia Posta ya zamani hadi ofisi ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam, kushinikiza Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kuwaondoa wabunge 19 waliofukuzwa uanachama na kupoteza sifa ya kuwa wabunge.

Maandamano hayo yamefanyika wakati kesi ya wabunge hao kupinga kuvuliwa uanachama ikiendelea katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, ambapo inatarajiwa kutajwa tena hapo kesho Mei 17.
Mbunge huyo, aliyewahi kuhudumu ubunge wa jimbo la Kawe kwa miaka 10, amesema yeye ni Chadema ‘for life’, akisema inawezekana kuna watu hawataki arudi katika chama hicho, lakini watake wasitake yeye bado ni Chadema.

“Mimi ni Chadema ‘for life’, tunawasiliana na Chadema seniors (waandamizi), alisema Mdee ambaye aliwahi kuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

Alipoulizwa kuhusu Serikali kutumia fedha kuwalipa yeye na wenzake 18 wanaodaiwa kuwa hawapo kihalali bungeni, Mdee alisisitiza kuwa wapo kihalali bungeni, ndio maana suala lao lipo mahakamani.

“Hivi kweli wakili makini na matata kama Peter Kibatala, hivi kunaweza kusiwe na zuio la mahakama, halafu mahakamani kukapoa? sio rahisi, ni maneno ya barabarani huwa sipendagi kuangaika nayo, ningehangaika nayo leo ningekuwa chizi,”amesema Mdee.

Mdee na wenzake 18 walivuliwa uanachama wa Chadema Novemba 27, 2020 baada ya kubainika katiba na kanuni za chama hicho kwa uamuzi wao wa kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum bila chama hicho kuwapitisha.

Mbali na Mdee, wengine ni Grace Tendega, Esther Matiko, Ester Bulaya, Cecilia Pareso, Hawa Mwaifunga, Jesca Kishoa, Nusrat Hanje, Kunti Majala, Felister Njau, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba na Conchesta Rwamlaza.

Chanzo: Mwananchi
Aache upumbavu, anadhani yeye ni mkubwa kuliko Chama? Ajiandae kisaikolojia, yajayo yanafurahisha.
 
Kama mmiliki wa chama Mbowe anatokwa jasho kwa muziki wa Covid19, hao Bawacha ni kina nani? Halima Mdee endelea kukaza hadi waombe poo.
NB: Halima ni mkubwa kuliko Bawacha + Heche.
Daa ila huyu maza, chadema msimwache! anamapande akikupa unatafuna unashiba...
 
Back
Top Bottom