Kama Mbowe angeheshimu Demokrasia ndani ya Chama kama ilivyoasisiwa na waasisi wa Chedema kwa ajili ya maendeleo ya nchi kupitia upinzani makini leo Chadema ingekua chini ya Zito Zuberi Kabwe kijana asiye na chembe ya uoga.
Awamu ya Tano ingekua na wakati mgumu sana kwa wananchi.
Hayo uliyoyataja yamesababishwa na serikali yenyewe lakini watanzania hawaoni pa kukimbilia mana Tegemeo lao lilikua ni Chadema na Chadema imekosa uongozi wenye nia ya dhati kulikomboa Taifa hili.
Sasa watu wanaona ni bora upinzani ubaki ndani ya CCM mana huko wanawatumia vizuri wale wenye maono makubwa Toka upinzani.
Leo hii Tundu Lisu akirudi CCM atakua na nafasi kubwa ya kuwa waziri wa Katiba na Sheria au Mwanasheria mkuu wa serikali na kulisaidia Taifa letu kuliko kukaa kwenye Chama kinachoendesha mambo yake kama CCM au kwa ubaya zaidi.
Mbowe alikua na nafasi kubwa ya kuivuruga CCM endapo angejenga Demokrasia ndani ya Chama chake.
Kukubali Demokrasia ndani ya Chama au serikali ni jambo gumu sana na linahitaji na linahitaji kujengwa kuanzia ndani ya vyama ambavyo vinategemewa kuunda serikali .
Sasa He,ndani ya Chadema kuna Demokrasia ?
Hivi Mbowe anaona hasara gani kuwaachia wenzake baada ya muda wake kuusha Mara ya nne sasa?
Hivi angewashukuru watanzania na kuwaomba waendelee kupigania Demokrasia ingekua na tatizo gani?
Angeimarisha chaguzi huru ndani ya Chama mana huko ndiko kipimo cha serikali ya Chedema kilipo lingekua ni jambo LA kuigwa sana.
Demokrasia ina gharama kubwa sana ikiwa ni pamoja na kuachia madaraka wakati bado mtu anayapenda au wananchi bado wanampenda.
Kupendwa kwa Mbowe na baadhi ya wanachama au viongozi wa Chama sio sababu ya kukiuka Miongozo na miiko iliyokuwa imewekwa na waasisi wa Chama.
Kuvuruga katiba na kuondoa kikomo cha uongozi kiliwakera watu wenye maono ndani ya Chama na kukifanya kuwa Chama chenye migogoro ya ndani isiyoisha na inayosulihishwa kwa kufukuzana.
Kufukuzana ni kupunguza nguvu ya Chama na shahidi ni CCM. Kufukuzana kwa Chadema kusilinganishwe na CCM kwani CCM wanasimama na dola kudhibiti wale wanaowafukuza. Na kama sio nguvu ya dola CCM ingeathirika sana na fukuza fukuza japo sio kubwa kama Chadema.
Chadema wasiige tu mfumo wa kufukuzana kwani ni mfano mbaya kidemokrasia. Mtu apewe nafasi ya kujieleza na kusikilizwa na hata kuonywa na sio vinginevyo ndiyo gaharama ya kujenga Demokrasia,uwazi na utawala bora ndani ya Chama na serikali.
Sent using
Jamii Forums mobile app