Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Umeitwa hujaenda, unataka chama kichukue uamuzi gani? Chama kimekuvua uanachama, kwa nini uingie bungeni kwa amri ya spika? Kama kweli siyo wachumia tumbo, wamwandikie barua spika kuwa wanalazimika kurudi chamani kukamilisha mchakato wa chama.

Kuendelea kuwa mbunge viti maalumu wa CHADEMA ili hali chama kimewafukuza, ni uchumia tumbo tu huo
 
Wewe jamaa ni mwana CCM kwenye akili, sio kama Ndugai aka Jingalao.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
inaitwa MBATA ya utosi kwa MATAGA na Ndugu-aai wao, yaani Mdee kawapiga nje Ndani, i mean Mzee Mdee.
 
Halima Mdee kamvua boxer feminist subwoofer. Bado yupo saaana CHADEMA. Wanaenda kuyajenga. Ubunge wa kikongwa kongwa siyo issue. Issue uanachama.
 
Wapo watakaokulaumu kwa vyovyote utakavyofanya bila ya kujali unalolifanya sasa ni jema au baya, kwa vile mwanzoni ulikosea, utaendelea kuwa mbaya tu siku zote.

Lakini wapo binadamu watakaokulaumu kwa kile ulichofanya wakati huo. Ukifanya vyema, bila ya kujali huko nyuma ulikosea, watakupongeza. Mimi nipo kwenye kundi hili.

Sikupongezi kwa sababu ulienda kuapa kinyume na maamuzi ya chama, sikupongezi kwa sababu umekuwa mbunge wala sikupongezi kwa sababu Ndugai amesema atakulinda. Bali nakupongeza kwa namna unavyokabiliana na tatizo lililopo mbele yako.

Wengi leo walitarajia umseme vibaya Mbowe na CHADEMA. Na hao ndio wanaodhani wamekuwa marafiki zako wapya.

Halima Mdee umeteseka sana kwa sababu ya kupigania haki na demokrasia Tanzania. Umeteseka sana kwa sababu tu umekuwa CHADEMA. Waliokuwa wanakusweka ndani, waliokuwa wanakutengenezea kesi, waliokuvunja mkono, waliokuwa wanakukejeli kwa maneno mengi ya dharau, leo wanajifanya ni marafiki zako.

Kumbuka kuwa mzazi wako hata kama anavaa lubega ni dhahiri ana upendo nawe zaidi kuliko jambazi mwenye jumba la ghorofa hata kama atakutoa kwa baba yako mwenye nyumba ya nyasi akawa anakulaza ghorofani kwenye chumba cha kifahari.

Nakupongeza kwa jinsi ulivyojibu hoja mbalimbali na kuonesha unatambua kuwa ni nani wanaokupenda na nani ni maadui lakini wanasema kuwa ndio walinzi wako. Yaani wauaji na watesaji wako leo wanakuwa walinzi na marafiki zako.

Nakupongeza kwa sababu hukuitusi CHADEMA, hukuitusi Kamati Kuu, hukumtusi Mbowe. Na hapa naipongeza Kamati kuu ya CHADEMA na Mh. Mbowe maana nao hata walipokuwa wakisoma maazimio ya Kamati kuu kuhusiana na Halima Mdee na wenzake, hawakuonesha kejeli wala chuki bali upendo wa dhahiri. Ni kama mzazi anayemchapa mwanae lakini anamchapa kwa sababu anataka abadilike na kuwa mtoto mwema na msikivu zaidi.

Mengine yatabakia katika maamizi ya Chama na ninyi wenyewe, lakini mpaka hapa umevuka kiunzi cha kwanza ambacho maadui wa CHADEMA na Mbowe walikuwa wakikisuburia kwa hamu.

Kwa njia uliyopita, kwa nguvu uliyoiweka, na imani uliyoitengeneza ndani ya CHADEMA, kwa Watanzania na Jamii ya kimataifa, usikubali kuipoteza imani hiyo kwa wepesi kiasi hicho.

Tunafahamu chama kitapitia njia ngumu, viongozi wa CHADEMA watapitia njia ya miiba lakini isiwe sababu ya kujijongesha kwa wadhalimu. Tengenezeni utaratibu, watu wenye mapenzi mema tuchangie kila mwezi ili kukitegemeza chama na watendaji wake. Hakika miongoni mwenu hakuna atakayekufa njaa wala kushindwa kutibiwa alimradi kuwepo utaratibu unaoeleweka.
 
Jibwa kaishapotea lakini bado unapiga miluzi ili iweje?
 
CCM very low... mlishadadia Dr. Slaa mkaishia na aibu baada ya kale ka press mlikoa
mwandalia kudharaulika na wanachi.

Msivyo na busara mkahamia kwa Mashinji..mkaishia na aibu.

Mkajitosa kwa wale wabunge Nasari, Lijuabaridi ; Shilinde na wenzao pia mkaishia kupata aibu ya mwaka..mkaangukia pua.

Sasa kwa kuwa hamna mshipa wa aibu safari hii mmehamia kwa hawa wa dada...sasa hii ndiyo itakuwa aibu ya mwaka hadi nje ya nchi...mataifa watawadharau na hizo mnazoziwinda za Mabeberu mtazisikia tu mtapishana nazo!!
 

CHADEMA nzima ni wachumia tumbo tu kuanzia mwenyekiti
 
Wasiliana na Saccos yako mbona walishazindua kuchangia saccos kupitia digitali mkuu!!?
 
Mdee tokaaaàaaaaaass CHADEMA Yuda mkubwaaaaaaaaa we, saliti lisilo ma aibu, bora askari magereza wangekuvunja mbavu kabisa
 
Mwanzo mzuri waje kwe meza ya maridhiano waombe msahama wajiuzuru ubunge viti maalumu, zipatikane baraka za chama kwenye teuzi zote.
 
Hapa ninachoona ni kwamba, kama wakisema tumekubali maana yake ubunge wameukosa. Mimi mwenyewe lazima niseme ni mwanachama ili niendelee hata kimahakama kuwa mbunge. Kuna maswali mengi kuliko majibu katika hili. Swali kuu, kwanini waliapa na wengine kutolewa magereza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…