Halima Mdee: Mimi pamoja na timu yangu (Wabunge 19) tutabaki kuwa WanaCHADEMA kindakindaki. Tutaenda kuyajenga ndani kwetu

Liverpool uliiombea mabaya msimu ulioisha ila hukufanikiwa.

CCM na CDM wote lao moja tu, sina ninayeweza kumpa dhamana.
Rule of law should be a cornerstone of our nation! Even the persons that have the power to be above the law by instruments, should observe the existence of such instruments as the law itself!

Wenye mamlaka wasitumie mapungufu ya kisheria yanayotoa mianya ya ubabe kuwa wababe. Huo ni ushamba uliopitiliza.
 
Nilitegemea Mdee leo angetuambia yale majina kapeleka Nani na waliopitishwa na kikao gani? Kweli ningemuelewa vizuri
 
Kwa hotuba ya Halima Mdee and Co. Ltd, I am convinced kuwa wameona wapi waliteleza na kweli wana damu ya CDM! let bygones be bygones..........forget past offences or causes of conflict and be reconciled.
Msiwape faida Nyang'au CCM....
Sasa wajiuzulu huo "ubunge" fake ili wasamehewe warudi chamani maisha yaendelee. Huyo aliyepanga mpango huu abaki na aibu na aendelee kutumia nguvu kuwatengeneza wabunge wa upinzani.
 
Wenye mamlaka wasitumie mapungufu ya kisheria yanayotoa mianya ya ubabe kuwa wababe. Huo ni ushamba uliopitiliza.
Mkuu wala siyo ushamba tu bali wanaonekana ni wapumbavu kupindukia! Ndugai anafikri anawakomoa viongozi wa CHADEMA, kumbe anatukomoa sisi raia tusiokuwa na hatua!
 
Mkuu, umeliweka vizuri sana. Nadhani wahusika wachutame tu maana nguo zimewadondoka. Waombe msamaha waukane upuuzi wote uliofanyika. Ni imani yangu watasamehewa na kurudishwa wawe wanachama wa kawaida. Hakuna haja ya kuwataja waliohusika kwa sababu hilo hawataliweza, hili ni kutokana na wahusika kutotaka waanikwe.
 
Mdee anaijua CHADEMA kuliko wewe Kasenene na Tundu Lissu wako. She is gonna be your Party Secretary General or Party Chairperson soon!
 
Mkuu wala siyo ushamba tu bali wanaonekana ni wapumbavu kupindukia! Ndugai anafikri anawakomoa viongozi wa CHADEMA, kumbe anatukomoa sisi raia tusiokuwa na hatua!
Anakukomoa wewe mwenyewe, sio wote.
 
Mdee hakujiandaa kuwa msaliti, woga wa kuteswa na watawala plus tamaa ya pesa vikamfanya Mdee kuingia kwenye mtego wa kuitumikia CCM kwa haraka bila kujua gharama yake.

Leo hii Mdee ni mtumwa wa CCM, ni kama mtu anayejuta kimoyo moyo. Kwa press ya leo, utagundua kabisa kuna kitu hakiko sawa baina ya Mdee na wale waliomtumia kuisaliti CHADEMA. Kuna mambo hayako sawa. Mdee na wenzake ni kama wanajilazimisha kufanya kitu ambacho hata wao hawakiamini.

Mdee amepoteza kujiamini, amepoteza kuaminiwa na ameharibu historia yake.
Kwa uzoefu wangu mdogo, watu kama Mdee wakiwa kwenye sintofahamu hizi, wengi hutamani kufa kuliko kuishi, hatari ya kujiua inamnyemelea...

Sijui kwanini nimeandika mambo haya hapa JF leo hii.
 
mwaka 2010 na 2015 chama kiligomea na kutotambua matokeo ya Urais pekee. Safari hii, 2020 chama kimegomea matokeo yote ya uchaguzi mkuu. Hivyo chama hakitambui chochote kilichotokana na uchaguzi (ikiwamo hizo asilimia za ubunge wa viti maalum).

2015 walipeleka wabunge wa viti maalum? Ni kura zipi zilizotumika kuwapa hizo nafasi! Ama walipinga matokeo ya Rais mteule lakini wakayakubali ya mgombea wao?
 
Pressure itakuwa imempanda sema hajajitambua, namshauri akapime coz lile jasho si la kawaida.
 
Chadema bandia sasa! Yaani Baada ya wapinzani bandia na walionunuliwa sasa kuna aina mpya ya viumbe katika siasa za Tanzania Chadema bandia baada ya wapinzani bandia na vyama vya upinzani bandia vya kina Shibuda, Cheyo, Mrema
 
Chadema bandia sasa! Yaani Baada ya wapinzani bandia na walionunuliwa sasa kuna aina mpya ya viumbe ktk siasa za Tz Chadema bandia baada ya wapinzani bandia na vyama vya upinzani bandia vya kina Shibuda, Cheyo, Mrema
Wachache Sana,watakaokuelewa hapa.
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… hii episode ya leo imenichekesha sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…