Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Halima Mdee na wenzake 18 wagoma kufika Kamati Kuu ya chama kwa madai ya kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,885
Muda mfupi kabla Kamati kuu CHADEMA kuwahoji wanachama wake walioapishwa kuwa wabunge wa viti maalum, wanachama hao wamesisitiza kutotokea mbele ya kamati kuu wakidai kupokea vitisho toka kwa viongozi na wanachama wa CHADEMA wakihofia usalama endapo watafika ofisi za chama hicho.
--
Awali Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) leo waliandamana katika ofisi za Makao Makuu ya chama hicho zilizopo Kinondoni Dar es Salaam, kushinikiza kutowahitaji wabunge Halima Mdee, Ester Bulaya na wengine walioapishwa viti maalum.

Bawcha.jpg

Updates

PICHA: Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema wakiendelea na kikao hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam cha kuwajadili Halima Mdee na wenzake 18 wanaotuhumiwa kwa usaliti wa chama kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum. #MwanaHALISIDigital https:
20201127_132600.jpg
20201127_132557.jpg
20201127_132553.jpg
20201127_132549.jpg
 
Chama chako hakitambui uchaguzi mkuu uliofanyika October 2020 na kinataka uchaguzi urudiwe. Kama msimamo wa chama ni kurudiwa kwa Uchaguzi, Mnalia haki viti 19 vya Uchaguzi upi?

Maana yake vikao walioka kamati kuu yenu kuazimia kutoutambua uchaguzi na kuweka msimamo wao urudiwe, ninyi mmepuuza vikao hivyo. Hamfai kabisa mnasukumwa na tamaa zenu za madaraka mnarudusha juhudi za chama chenu nyuma kupambania haki za Watanzania.
 
Hadi sasa haieleweki kama kikao hicho kitafanyika ama la kadhalika uhakika wa akidi kutimia unatia shaka.

Ufipa hali ni shwari na kuna vijana wachache wa BAVICHA ambao kimsingi hawatoi taarifa kama kikao kitakuwepo na kitafanyikia wapi zaidi ya kuwataka wanachama wawe na subira.

Ngoja tuone muda ndio msema kweli.

Maendeleo hayana vyama
 
Wewe umasikia kulikuwa na kikao leo?

Hajuna mjumbe aliyrenda hata Mbowe si kina Halina tu.
 
Executive decision
Wawafukuze wote, ccm iwachukuwe nakuwapa uanachama.

Endapo cdm itachelewa ... itarajie maumivu makali na kitadhoofishwa sana.

Ili cdm ibakie juu na heshima, hadhi, weledi na ili iendelee kukubaliana zaidi.

Chama kiwafukuze wote na yule wa mpanda. Wasiichelewe.
 
Wakifukuzwa tu, watakimbilia Mahakamani, Korti itazuia Bunge kuwatimua, Speaker atatii kwa furaha kabisa, watadunda Ubunge mpaka June 2025 huku kesi ikirushwa

Humu katikati Dec 2020 - June 2025 hawa 19 na Kamati kuu watayajenga na kusameheana ili maisha yawe rahisi kwa kila mtu

Hizi ndizo siasa za Tanzania
 
Back
Top Bottom