Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Baada ya Wabunge 19 kutimuliwa chamani, ahadi yao ya kupewa ulaji mkubwa na heshima kubwa ipo wazi ni suala la muda tu.
Ni wazi Halima Mdee ni kiongozi wa kundi la wanawake walioamua kujipeleka Mjengoni pasipo ridhaa ya chama wala baraka za viongozi wakuu. Ni wazi pia Halima na kundi lake waligushi saini,mihuri na nyaraka za chama ili kufanikisha mpango mzima.Katika nchi zinazo heshimu Katiba,Sheria na Taratibu jambo kama hili kamwe haliwezi kufanyika.
Tanzania ya Dear Leader Dr Magufuli ukiukwaji wa katiba lilikuwa jambo la kawaida sana,hadi wanazuoni na wabobezi wa fani mbali mbali walishakubali na kuona ni utaratibu wa kawaida. Hebu fikiri hata kwa dakika moja Wabunge 19 ambao hawana barua ya chama, hawana baraka rasmi na utaratibu rasmi wa Tume ya Uchaguzi,wanakula kiapo garage na wanatambulika kama wabunge halali wa chama.
Pamoja na ukweli kwamba siasa zimeanza kubadilika tangu Mama ashike hatamu za kuongoza nchi,lakini tayari makosa yalishafanyika chini ya mtangulizi wake. Kwakuwa Halima Mdee kakubali kufa na kamba shingoni lazima waliomtumia hata kama ni nje ya utaratibu wawapatie vijinafasi vya kuendelea kuhemea.
Halima Mdee nafasi ya Ubalozi katika nchi za EU ilikuepukana na fedhea ya kuitwa msaliti ipo wazi kabisa.Wengine nafasi za DC na Katibu Tawala zinawangojea kwa shauku kubwa.
Ngongo kwasasa Uganda.