Uchaguzi 2020 Halima Mdee: Natuhumiwa kumchonganisha Gwajima na madhehebu mengine na waumini wake

Uchaguzi 2020 Halima Mdee: Natuhumiwa kumchonganisha Gwajima na madhehebu mengine na waumini wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mgombea Ubunge jimbo la Kawe kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Halima Mdee, amesema kuwa hajakubaliana na maamuzi ya Kamati ya Maadili ambayo yamemsimamisha kutofanya kampeni siku 7 na anaelekea Tume kuwasilisha rufaa yake.

Mdee ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa Kamati ya Maadili ilitoa hukumu bila kumsikiliza wala kusikiliza ushahidi wake aliowasilisha.

“Kwa mujibu wa tuhuma nilizopewa na Chama cha Mapinduzi kuwa namchonganisha Gwajima na madhehebu mengine na waumini wake, nimewasilisha ushahidi mbele ya Kamati ya Maadili lakini hawajataka kunisikiliza”, amesema Mdee.

Mgombea Ubunge Jimbo la Kawe kwa tiketi ya CHADEMA, Halima Mdee amefungiwa kufanya Kampeni kwa siku saba kuanzia Oktoba 12 hadi Octoba 18 kwa madai ya kukiuka maadili ya uchaguzi.
 
Hukumu gani hizo mtuhumiwa kuto sikilizwa ....kwanza gwaji si alijipalia mwenyewe mpk leo yupo hewani akiropoka utopolo wake kuwahusu Roman catholic na Waislam pia ayo makosa ana bebeshwaje mtu mwingine si wakaufute kwanza uko ⏳
 
If you can't take the heat, stay out of the kitchen.....;
Yaani mwanasiasi anaanza kulindwa kwamba asitukanwe au asichonganishwe ?, wanadhani siasa ni nini ?, Mkutano wa Injili ?

This is Bogus, hawa Tume wanaleta mchezo wa ajabu kwa kutumia Kodi zetu ku-finance haya mambo ya ajabu, ajabu.....
 
Wawe wawazi tu kuwa huo ni mchecheto tu. Wanatambua fika uwepo wa Halima Mdee ktk kampeni zake, ungepunguza idadi ya watu wabebwao kwenda kwenye mkutano wa Mzee Baba pale Tanganyika Packers ili waweze kutumbuizwa na kusikiliza mubashara nyimbo za wana Bongo fleva maarufu.
 
Tatizo la adhabu kutolewa na CCM kutangazwa na NEC!
Kwa taarifa yako Kamati ya Maadili inahusisha vyama vyote vinavyoshiriki kwenye uchaguzi wa 2020 ikiwemo Chadema! Sasa kama hata vyama vingine vimeona anastahiri kupigwa ban akubali tu huyo mbunge mstaafu.
 
Mpaka sasa sielewi CCM wamempa Gwajima kwa kutumia vigezo gani ........... Au ni kwa kuwa ni wa kwetu Koromije au kuna jingine....!! cc Pascal Mayalla
Kwa kuwa alipitishwa na uongozi wa CCM hivyo wewe hangaika na Chadema ya CCM hayakuhusu!
 
Gwajima alijichonganisha na madhehebu mengine yeye mwenyewe asimuhusishe Halima
 
Kwa taarifa yako Kamati ya Maadili inahusisha vyama vyote vinavyoshiriki kwenye uchaguzi wa 2020 ikiwemo Chadema! Sasa kama hata vyama vingine vimeona anastahiri kupigwa ban akubali tu huyo mbunge mstaafu.
Toa ujinga wako hapa! Kwa hiyo CHADEMA wamekaa na CCM kumuadhibu Halima? Na tangu lini chama cha siasa kikawa na mamlaka ya kutoa adhabu? Crap!
 
Kwa taarifa yako Kamati ya Maadili inahusisha vyama vyote vinavyoshiriki kwenye uchaguzi wa 2020 ikiwemo Chadema! Sasa kama hata vyama vingine vimeona anastahiri kupigwa ban akubali tu huyo mbunge mstaafu.
Kamati ya Maadili inahusisha CHADEMA, CCM-A, CCM-B, CCM-C, CCM-D, CCM-E, CCM-F, CCM-G etc
 
Back
Top Bottom